Waziri Mkuu mstaafu na Mbunge
wa Monduli, Edward Lowasa akisalimiana na wanafunzi wa chuo kikuu cha
UDOM waliotoka shule za sekondari za kata, wakati walipofika nyumbani
kwake mkoani Dodoma kutoa shukrani zao kwa hatua waliyofikia kielimu.
Hamida Salum mwanafunzi wa mwaka wa kwanza UDOM, akizungumza kwenye hafla hiyo Juni 25, 2013
Mh. Lowasa katikati, Dkt. Mahanga (Kulia) na Parseko Korne wakiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya wanafunzi hao.
Wanafunzi
wa Chuo Kikuu cha DODOMA, maarufu kama UDOM, ambao walifika hapo
wakitokea zile shule za makabwela (Shule za Kata), wamemtaka Mbunge wa
Monduli na Waziri Mkuu mstaafu, Edward Lowasa, achukue fomu za kugombea
urais 2015 muda utakapowadia.
Pia
wameahidi kujichangisha fedha kwa ajili ya malipo ya fomu hizo endapo
italazimika. Kauli hiyo ya kwanza kutoka kwa makundi na watu wasiokuwemo
ndani ya siasa, ilitolewa Jumatatu usiku nyumbani kwa Lowasa mjini
Dodoma, wakati kundi la wanafunzi hao walipofika kutoa shukrani zao kwa
hatua waliyofikia ikiwa ni matunda ya shule hizo, ambazo muasisi wake ni
mbunge huyo wa Monduli.
“Mimi
ninayofuraha kusimama hapa leo hii, nikiwa mtu tofauti, kwa maana
ninayesoma elimu ya juu, baada ya kufanikiwa ,kuendelea na elimu ya
sekondari kupitia shule za kata pale Kiluvya Dar es Salaam” anasema
Hamida Salum ambaye kwa sasa ni mwanafunzi wa mwaka wa kwanza hapo UDOM.
“Wewe
ni jembe, kama uliweza kusimamia ujenzi wa shule za kata kwa kipindi
kifupi cha miaka 2, ninahakika unaweza kufanya men gi zaidi endapo
utakuwa rais wan chi hii” mwanafunzi mwingine wa mwaka wa kwanza,
Clementina Ophoro alisema, kwenye salamu za mwanafunzi mmoja mmoja
wakati wa utoaji shukrani kwa Lowasa.
Lowasa
wakati akiwa waziri mkuu wa Tanzania, kwenye mwanzoni mwa awamu ya n ne
ya utawala wa rais Jakaya Kikwete, aliweza kusimamia ujenzi wa shule za
kata kote nchini, ili kutoa nafasi zaidi za wanafunzi wa makabwela,
walioishindwa kendelea na masomo kwa sababu mbalimbali ikiwa ni pamoja
na uhaba wa madarasa.
Kwa
sasa shule hizo zimekuwa zikibezwa na watu mbalimbali kwa maelezo kuwa
hazina walimu wa kutosha na uhaba wa vifaa vya kufundishia ikiwemo
vyumba vya maabara.
“Mimi
ninawashangaa watu wanaosema kuwa eti shule za kata hazifai, kwa vile
hazina walimu na vifaa. Haya maneno ni ya kupuuzwa, kwani binadamu
hupaswi kukwepa changamoto za maisha” alisema mwanafunzi mwingine Victor
Mafuru pia wa mwaka wa kwanza.
Wanafunzi
hao wa UDOM waliotoka kwenye shule za sekondari za kata, wameamua
kuanzisha umoja wao kote nchini, ili kuendeleza ndoto za kuhakikisha
kila mwanafunzi wa mtu masikini anapata elimu.
Kwa
kuanzia wanafunzi hao wapatao 600, wameahidi kufundisha bure kwenye
shule za umma, wawapo likizo baadaye mwishoni mwa mwezi huu wa Juni.
Kwa upande wake, Lowasa ambaye alikuwa pamoja na naibu waziri wa kazi na ajira, Dkt. Makongoro Mahanga, mbunge wa Kigoma mjini, Peter Serukamba, na mkuu wa mkoa wa Singida, Parseko Kone, aliwapongeza wanafunzi hao kwa moyo wao wa shukrani na kuwataka wasikatishwe tama na maneno yanayotolewa juu ya ubora wa shule hizo, kwani yeye binafsi anajivunia juhudi zake kupitia sera za chama cha Mapinduzi, zimeweza angalau kutoa wanafunzi wengi kutoka shule hizo kujiunga na vyuo vikuu.
Kwa upande wake, Lowasa ambaye alikuwa pamoja na naibu waziri wa kazi na ajira, Dkt. Makongoro Mahanga, mbunge wa Kigoma mjini, Peter Serukamba, na mkuu wa mkoa wa Singida, Parseko Kone, aliwapongeza wanafunzi hao kwa moyo wao wa shukrani na kuwataka wasikatishwe tama na maneno yanayotolewa juu ya ubora wa shule hizo, kwani yeye binafsi anajivunia juhudi zake kupitia sera za chama cha Mapinduzi, zimeweza angalau kutoa wanafunzi wengi kutoka shule hizo kujiunga na vyuo vikuu.
No comments:
Post a Comment