ADV

ADV

ADVERTISEMENT CORNER

HUDUMA YA KUKATA TICKET ZA NDEGE ONLINE


SOMA HABARI

SOMA HABARI
Showing posts with label EDWARD LOWASSA.. Show all posts
Showing posts with label EDWARD LOWASSA.. Show all posts

Monday, September 16, 2013

LOWASSA ASIMIKWA KUWA CHIFU WA UNYENYEMBE MKOANI TABORA

Waziri Mkuu Mstaafu na Mbunge wa Jimbo la Monduli, Edward Lowassa akivishwa vazi maalum la Kichifu pamoja na kukabidhiwa mkuki na Chifu Mkuu wa Kabila la Unyenyembe, Chifu Msagata Fundikira ikiwa ni ishara ya kumsimika kuwa Chifu wa Kabila hilo, wakati wa Sherehe za Maadhimisho ya Kumbukumbu ya Mtemi Isike Mwanakiyungi aliefariki miaka 124 iliyopita. Sherehe hizo zimefanyika jana kwenye Kijiji cha Itetemya, mkoani Tabora.
Waziri Mkuu Mstaafu na Mbunge wa Jimbo la Monduli, Edward Lowassa pamoja na Chifu Mkuu wa Kabila la Unyenyembe, Chifu Msagata Fundikira wakishirikiana kuweka jiwe la msingi katika eneo litakalojengwa mnara wa kumuenzi Mtemi Isike Mwanakiyungi aliefariki miaka 124 iliyopita.
 
Waziri Mkuu Mstaafu na Mbunge wa Jimbo la Monduli, Edward Lowassa pamoja na Chifu Mkuu wa Kabila la Unyenyembe, Chifu Msagata Fundikira wakiwa kwenye picha ya pamoja na machifu kutoka mikoa mbalimbali hapa nchini walioshiriki kwenye Sherehe za Maadhimisho ya Kumbukumbu ya Mtemi Isike Mwanakiyungi aliefariki miaka 124 iliyopita.

Wednesday, June 26, 2013

WANAFUNZI WALIOSOMA SHULE ZA KATA MPAKA VYUO VIKUU WATOA SHUKRANI ZAO KWA WAZIRI MKUU MSTAAFU EDWARD LOWASSA


 Waziri Mkuu mstaafu na Mbunge wa Monduli, Edward Lowasa akisalimiana na wanafunzi wa chuo kikuu cha UDOM waliotoka shule za  sekondari za kata, wakati walipofika nyumbani kwake mkoani Dodoma kutoa  shukrani zao kwa hatua waliyofikia kielimu.
  Hamida Salum mwanafunzi wa mwaka wa kwanza UDOM, akizungumza kwenye hafla hiyo Juni 25, 2013
Mh. Lowasa katikati, Dkt. Mahanga (Kulia) na Parseko Korne wakiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya wanafunzi hao.

Wanafunzi wa Chuo Kikuu cha DODOMA, maarufu kama UDOM, ambao walifika hapo wakitokea zile shule za makabwela (Shule za Kata), wamemtaka Mbunge wa Monduli na Waziri Mkuu mstaafu, Edward Lowasa, achukue fomu za kugombea urais 2015 muda utakapowadia.

Pia wameahidi kujichangisha fedha kwa ajili ya malipo ya fomu hizo endapo italazimika. Kauli hiyo ya kwanza kutoka kwa makundi na watu wasiokuwemo ndani ya siasa, ilitolewa Jumatatu usiku nyumbani kwa Lowasa  mjini Dodoma, wakati kundi la wanafunzi hao walipofika kutoa shukrani zao kwa hatua waliyofikia ikiwa ni matunda ya shule hizo, ambazo muasisi wake ni mbunge huyo wa Monduli.
“Mimi ninayofuraha kusimama hapa leo hii, nikiwa mtu tofauti, kwa maana ninayesoma elimu ya juu, baada ya kufanikiwa ,kuendelea na elimu ya sekondari kupitia shule za kata pale Kiluvya Dar es Salaam” anasema Hamida Salum ambaye kwa sasa ni mwanafunzi wa mwaka wa kwanza hapo UDOM.

“Wewe ni jembe, kama uliweza kusimamia ujenzi wa shule za kata kwa kipindi kifupi cha miaka 2, ninahakika unaweza kufanya men gi zaidi endapo utakuwa rais wan chi hii” mwanafunzi mwingine wa mwaka wa kwanza, Clementina Ophoro alisema, kwenye salamu za mwanafunzi mmoja mmoja wakati wa utoaji shukrani kwa Lowasa.

Lowasa wakati akiwa waziri mkuu wa Tanzania, kwenye mwanzoni mwa awamu ya n ne ya utawala wa rais Jakaya Kikwete, aliweza kusimamia ujenzi wa shule za kata kote nchini, ili kutoa nafasi zaidi za wanafunzi wa makabwela, walioishindwa kendelea na masomo kwa sababu mbalimbali ikiwa ni pamoja na uhaba wa madarasa.
 
Kwa sasa shule hizo zimekuwa zikibezwa na watu mbalimbali kwa maelezo kuwa hazina walimu wa kutosha na uhaba wa vifaa vya kufundishia ikiwemo vyumba vya maabara.

“Mimi ninawashangaa watu wanaosema kuwa eti shule za kata hazifai, kwa vile hazina walimu na vifaa. Haya maneno ni ya kupuuzwa, kwani binadamu hupaswi kukwepa changamoto za maisha” alisema mwanafunzi mwingine Victor Mafuru pia wa mwaka wa kwanza.

Wanafunzi hao wa UDOM waliotoka kwenye shule za sekondari za kata, wameamua kuanzisha umoja wao kote nchini, ili kuendeleza ndoto za kuhakikisha kila mwanafunzi wa mtu masikini anapata elimu.

Kwa kuanzia wanafunzi hao wapatao 600, wameahidi kufundisha bure kwenye shule za umma, wawapo likizo baadaye mwishoni mwa mwezi huu wa Juni.

Kwa upande wake, Lowasa ambaye alikuwa pamoja na naibu waziri wa kazi na ajira, Dkt. Makongoro Mahanga, mbunge wa Kigoma mjini, Peter Serukamba, na mkuu wa mkoa wa Singida, Parseko Kone, aliwapongeza wanafunzi hao kwa moyo wao wa shukrani na kuwataka wasikatishwe tama na maneno yanayotolewa juu ya ubora wa shule hizo, kwani yeye binafsi anajivunia juhudi zake kupitia sera za chama cha Mapinduzi, zimeweza angalau kutoa wanafunzi wengi kutoka shule hizo kujiunga na vyuo vikuu.

Tuesday, May 21, 2013

KIKWETE AMWAGIA SIFA LOWASA A.K.A "JEMBE"



Rais Jakaya Kikwete amemwagia sifa Waziri Mkuu wa zamani, Edward Lowassa hatua ambayo inaweza kutafsiri mengi katika medani ya siasa nchini.
 Akizungumza na wabunge wa CCM kwenye Ukumbi wa White House Dodoma juzi, Rais Kikwete ambaye pia mwenyekiti wa chama hicho,alisema nguvu za Lowassa pekee zinatosha kushinda uchaguzi mdogo wa kiti cha udiwani Kata ya Makuyuni kilichoko wilayani Monduli.
Kata ya Makuyuni iko wilayani Monduli, ambako Lowassa amekuwa mbunge wake tangu mwaka 1995.
Habari za kutoka ndani ya kikao hicho zinaeleza kuwa Rais Kikwete alitoa kauli hiyo kuhusu kampeni za uchaguzi huo wa Makuyuni, baada ya kuwa ametoa ruksa kwa makada wa chama hicho wanaotaka urais kuanza kujipitisha pitisha miongoni mwa wanachama wa chama hicho. 
Lowassa anatajwa kuwa miongoni mwa wanaCCM wanaotaka kumrithi Rais Kikwete kwenye Uchaguzi Mkuu mwaka 2010.
“Sina tatizo na pale Makuyuni, najua muscles (misuli) za Mzee Lowassa zinatosha kutupa ushindi; au vipi mzee?”alidokeza mmoja wa wabunge wa CCM akimnukuu Rais Kikwete.
Uchaguzi wa Udiwani Kata ya Makuyuni unaotarajiwa kufanyika Juni 16, mwaka huu, utakuwa wa ushindani mkali kati ya CCM na Chadema ambao historia yao kisiasa mkoani Arusha ni ya uhasama. 
Katika uchaguzi huo, unaofanyika baada ya kifo cha Abdillah Warsama (CCM), chama hicho kitatetea nafasi yake kwa kumsimamisha Godluck Lerunya na Chadema ni Japhet Sironga. 
Mbali na Kata ya Makuyuni, uchaguzi wa udiwani mkoani Arusha utafanyika pia katika Kata za Kaloleni, Themi, Kimandolu na Elerai, kutokana na waliokuwa madiwani wa kata hizo (Chadema), kufukuzwa na chama chao.
“Mnaweza kuchafuana leo, kesho mkapata mgombea mwenye nundu nyingi na mabandeji kila mahala, halafu mkapata shida kumnadi,” alisema.
Siyo mara ya kwanza kwa Kikwete kumsifia Lowassa kwani aliwahi kufanya hivyo mwaka jana huko Longido wakati akikabidhi ng’ombe.
Pia aliwahi kumsifia wakati wa kampeni za uchaguzi za mwaka 2010 wakati Kikwete alipomwelezea Lowassa kama Mbunge makini na kuwaomba watu wa Monduli kumchagua tena.

Hata hivyo, alipoulizwa kama baada ya kuruhusiwa kuanza kujipitisha kwa wanaCCM kama anataka kuwania urais, Lowassa alijibu kupitia watu wake wa karibuni kuwa asingependa kuzungumzia suala hilo hasa baada ya Rais kutoa kauli hiyo.
Kutangaza nia ruksa
Rais Kikwete aliwaeleza wabunge hao kuwa si kosa kwa watu kutangaza nia ya kugombea nafasi mbalimbali za uongozi ikiwamo urais mwaka 2015.

“Wabunge na mawaziri wenye nia ya kutangaza nia ya kugombea urais wawe huru, kwani hiyo ni haki yao, isipokuwa wafanye kwa wema bila kukivuruga chama na kuwagawa wanaCCM katika makundi. Sioni tatizo watu kujipitisha. Sisi sote hapa tulijipitisha. Lakini tufanye hivyo kistaarabu bila kuvurugana.”'

Aliwaagiza wabunge wa chama hicho kwenda majimboni mwao kusikiliza kero za wananchi badala ya kusubiri wakati wa uchaguzi.
Kauli ya Membe
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bernard Membe ambaye naye anatajwa kuwa miongoni mwa wagombeaamewataka waandishi waache kuandika kila siku habari za urais na badala yake waandike mambo ya maendeleo. 


Akizungumza na waandishi wa habari jana baada ya kukutana na mabalozi wa nchi zinazoendelea kuhusu Mkutano wa Smart Partnership, unaotarajiwa kufanyika nchini, Membe alisema ni vizuri yakaandikwa mambo ya maendeleo na si kila wakati kuandika mambo ya urais.

“Mkutano kama huu nchi kama Kenya watauripoti vizuri na kwa undani hivyo mfanye hivyo si kila kitu urais 2015,”alisema Membe.

 Mkutano huo utaanza Mei 28, hadi Juni Mosi na utajadili jinsi gani sayansi na teknolojia vinaweza kutumika kuzikwamua kiuchumi.

CHANZO: MWANANCHI
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...