ADV
SOMA HABARI
Wednesday, July 3, 2013
Hatimaye demokrasia isiyoeleweka imemwondo rais Morsi madarakani
Jeshi la Misri limempindua rais Mohamed Mosri kwa kile lilichoeleza kuwa ni utawala ambao haukuweza kutimiza matakwa ya wananchi wote wa Misri. Katiba ya nchi hiyo imevunjwa na kesho asubuhi ataapishwa rais wa mpito hadi uchaguzi mwingine utakapofanyika. Maelfu na maelfu ya waandamanaji waliokuwa wameweka kambo Tahrir Squire wamelipuka kwa shangwe na furaa kubwa baada ya habari hizi kuwafikia, wakati huo huo, wafuasi wa Morsi wamebaki wakiduwaaa kwa mshangao kuona rais wao aliyechaguliwa kwa kufuata kanuni zote za kidemokrasia, na kwamba mwaka mmoja tu hautoshi kupima uwezo wa rais huyo ambaye hakuwa na uzoefu wa siasa, Haijulikani kama Morsi atapinga hatua hiyo na yeye kuwaeleka mafuasi wake mitaani au atakubali yaishe. Kuna uwezekano mkubw akwa wananchi wa Misri kuingia katika vita vya wenyewe kwa wenyewe kama hali haitakuwa shwari haraka.
Haya demokrasia ya watu, na watu na kwa ajili ya watu itaendeleea kujidhihirisha.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment