Mandla Mandela.
|
Mjukuu wa kiume wa Mzee Nelson Mandela amepewa masaa
mawili (yaliyoishia leo saa 9 alasili) awe amefukua mabaki ya miili mitatu ya
ndugu zake na kuyarejesha kwenye kiwanja cha maziko cha familia hiyo au
atahukumiwa kifungo jela baada ya kuwa ametuhumiwa kuhamisha makaburi kinyume
cha sheria.
Mandla Mandela
alipewa chini ya masaa 24 na mahakama mjini Mthatha kurejesha miili ya watoto
watatu wa rais huyo wa zamani wa Afrika Kusini kwenye kijiji cha Qunu, ambako
Mandela alikulia.
Ndugu 16 wamempeleka
Mandla mahakamani baada ya kuzika upya mabaki ya miili ya watoto wa baba huyo
wa taifa mwenye miaka 94 kwenye eneo alilozaliwa la Mvezo mwaka 2011.
Ndugu wa Mandela
wanadai Mandla Mandela hakupata ruhusa au hata kuwataarifu wanafamilia wakati
alipochukua uamuzi huo.
Baba huyo wa taifa
alishasema tangu awali kwamba anataka kuzikwa huko Qunu, ambako watoto wake
walizikwa kwenye makaburi ya familia, na mahali ambako aliishi baada ya
kustaafu kama rais.
Kwa mujibu wa
vilivyomo kwenye wosia wake ambao umechapishwa, angependa kuzikwa kwenye kaburi
la gharama nafuu katika bustani ya kumbukumbu nyumbani kwake - mahali ambako
hapo awali alisema panabeba kumbukumbu za maisha yake ya utotoni.
Wiki iliyopita
mahakama hiyo ilitoa amri ya mpito kwa miili hiyo kuhamishwa takribani kilomita
14 kutoka Mvezo kwenda Qunu.
Lakini Mandla, ambaye
ni chifu wa Mvezo, sasa anapinga amri hiyo.
Inaaminika kwamba
Mandla alihamisha miili ya binti mkubwa wa Mandela, Thembi, ambaye alifariki
kwa ajali ya gari mwaka 1969, Magkatho, ambaye alifariki kwa ukimwi mwaka 2005
na Makaziwe, ambaye alifariki kwa homa ya uti wa mgongo akiwa na umri wa miezi
minane tu mwaka 1948, katika jaribio la kujipatia fedha wakati babu yake
atakapofariki.
Aliripotiwa kwamba
kuhamisha miili hili ni sehemu ya hila zake kuhakikisha Mandela anazikwa ndani
ya kituo cha wageni alichojenga kilichomgharimu Pauni za Uingereza milioni 4.
No comments:
Post a Comment