Mabaki ya watoto watatu wa mzee mandela wakizikwa upya kwenye makaburi ya familia katika kijiji cha Qunu
Sehemu ya Makaburi ya familia ya Mandela Msafara ukipeleka mabaki wa miili ya watoto wa Mzee mandela
Mandela mara baada ya kuachiwa huru na makaburu
Mandela akiwa amepunzika kijijini kwao Qunu
Madla Mandela, mjukuu wa Mandela anayedaiwa kuleta vurugu katika familia ya Mzee Mandela
Mkanganyiko mkubwa umetokea kwenye familia ya mzee Mandela hata kabla hajafa kutokana na kile kinachoelezwa kuwa ni kugombania mali za urithi za Mzee Mandela hata kabla hajafariki dunia. Mkanganyiko huo ulianzushwa na mjukuu wa Mandela Madla Mandela ambaye pia ni chifu wa Qunu alipohamisha masalia ya miili ya watoto wa mzee Mandela na kuyaweka katika eneo aliloliandaa yeye kwa manufaa yake katika eneo la Mvezo kilometa 30 kutoka eneo la Qunu. Madla Mandela alifanya hivyo bila kuwashirikisha wanandugu wengine wa familia mwaka 2011. Hii ilipelekea wanandugu 16 wa familia ya Mzee mandela kufungua kesi mahakamani kuomba miili hiyo irudishwe mahali pake asilia jambo lililofanyika jana kwa amri ya mahakama.
Mandela mwenyewe ambaye kwa sasa yu mahututi hospitalini, katika wosia wake alitaka azikwe kijijini kwake Qunu sehemu ambayo alikulia akiwa mdogo.
Wanawe Mandela wametaka baba yao atakapofariki basi azikwe pamoja na wanawe.
Hata wazazi wa mzee Mandela mama yake, Nosekeni na baba yake, Mphakanyiswa nao wamezikwa katika eneo hilo
Mjukuu huyo ambaye ndiye anayeonekana kuwa mwanasiasa pekee katika uzao wa mzee Mandela, aliondoa miili ya watoto wa Mandela, mtoto wake wa kwanza wa kioume Thembekile aliyefariki mwaka 1969, kichanga cha miezi tisa Makaziwe aliyefariki mwaka 1948, na baba mzazi wa Mandla mwenyewe Magkatho ambaye alikufa kwa ukimwi waka 2005.
No comments:
Post a Comment