Meya
wa jiji la Arusha amefyatuka na kuwataka wanasiasa kuwapelekea wananchi
maendeleo na kuachana na kauli za kumuondoa meya huyo na malumbano
yasiyo na tija kwa wakazi wa jiji la Arusha kwani utaratibu wa kanuni
na sheria zipo wazi na hazihitaj malumbano kwakuwa yupo kisheria.
Akizungumza
na waandishi wa habari kwenye ofisi za Halmashauri ya Jiji la Arusha
Meya huyo Gaudency Lyimo alikuwa akijibu swali aliloulizwa kumekuwepo na
malumbano ya muda mrefu kiasi cha kupachikwa majina kuwa meya wa
kichina huku wanasiasa wakijinadi kuwa ataondoka kwenye kiti hicho baada
ya uchaguzi mdogo uliopita mjadala wa meya hauna tija kwa wakazi wa
jiji hilo.
Meya
Lyimo amesema kuwa wakati huu si wa kulumbana bali ni wakati wa
kuwaletea wananchi maendeleo kwani siku hazirudi nyuma na wanaofikiri
mawazo hayo wanakosea kwani kila nchi inasheria na kanuni walizojiwekea
na hata halmshauri inaongozwa kwa mujibu wa sheria hivyo suala hilo lipo
kisheria .
Lyimo
amewataka wanasiasa wanaopita kuhoji uhalali wa meya huyo kuwa
ataondoka wana ndoto za mchana kwani yeye yupo kisheria na kanuni
zinazoendesha halmashauri hapa nchini huku akiwataka madiwani
waliochaguliwa kuweka mbele maslahi ya wakazi wa jiji na kuwaletea
maendeleo.
Malumbano
hayo yalianzishwa baada ya uchaguzi mdogo wa udiwani kwenye jimbo la
Arusha kwa chama cha Demokrasia na Mandeleo (CHADEMA)kudai kuwa muda wa
meya huyo unahesabika kwani idadi yao au koramu inatosha kumuondoa meya
huyo.
Huku
vyombo mbali mbali vya habari vikiripoti kuwa meya akalia kuti kavu
ndipo waandishi walipoamua kumhoji meya huyo kupata msimamo wake kwenye
suala hilo.
No comments:
Post a Comment