ADV

ADV

ADVERTISEMENT CORNER

HUDUMA YA KUKATA TICKET ZA NDEGE ONLINE


SOMA HABARI

SOMA HABARI

Wednesday, July 3, 2013

MISRI-"NI DEMOKRASIA LAKINI SI KWA MAPENZI YA WAKUBWA"


Raia wa Misri wamejikuta katika mgawanyo mkubwa na mbaya zaidi kuliko ule uliopelekea kumwondoa Mubaraka madarakani.  Wakati wa kumwondoa Mubaraka wananchi wote waliungana na kuandamana mitaani kwa siku kadhaa hadi pale Mzee Mubaraka alipoona hakuna njia zaidi ya kuachia madaraka kwa jeshi.
Ni hapo chama chenye msimamo mkali wa kiislamu "Muslim Brothehood" kikajikuta ndicho chama pekee kilichokuwa kimejiimarisha ingaawa kwa siri kutokana na kupigwa vita ndani na nje.
Muslim Brothehood ilifanya juhudi zote na kufuata demokrasia na kuchaguliwa kidemokrasia lakini hata baada ya kuchaguliwa, Dunia "Wakubwa"  waliupokea ushindi huo wa "demokrasia" kwa shingo upande. Watabiri wa mambo waibashiri kuwa utawala wa Morsi hautadumu, na kweli sasa Morsi anaelekea kusikojulikana. Sababu hazikosekani, Ohh utawala mbovu, oh utawala wa mabavu, oh uchumi mbovu, "kweli ndani ya mwaka mmoja unaweza kufanya yote hayo?
Hii ndiyo demokrasia. Demokrasia ya kweli ni ile inayokubaliana kwa dhati na "bwana wakubwa" hata kama kuna madudu kiasi gani bado wataiita demokrasia. Hata ukifuata misingi yote ya demokrasia "if you are a wrong person in place you will always be evicted by any means. Chambo ni wananchi na damu zao na damu za ndugu zao. Je definition ya demorasia itabaki kuwa "A system of government by the whole population or all the eligible members of a state, typically through elected representatives".?
Nahisi kuna maana nyingine ya demokrasia tusioifahamu wengi na hatuna budi kufanya

1 comment:

  1. Sijakuelewa unaposema bila 'kukubaliwa na wakubwa', ingekuwa viruri basi ukawataja hao wakubwa na ukatoa uthibitisho wa jinsi wanavyosaidia hayo mapinduzi.

    ReplyDelete

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...