Daladala lenye namba za usajili T 741 AEG baada ya kuhama njia na kuparamia mtaro uliopo jirani na bucha eneo la Mwenge.
Daladala lenye namba za usajili T 741 AEG linalofanya safari zake
kati ya Temeke na Mwenge asubuhi hii nusura liingie katika bucha iliyopo
maeneo ya Mwenge jijini Dar katika barabara iendayo Afrika Sana.
Daladala hilo lilisaidiwa na mtaro uliopo mbele ya bucha hiyo baada ya
dereva wake kushindwa kuliongoza na kuhama barabara. Kwa mujibu wa
mashuhuda waliokuwa eneo la tukio, daladala hilo halikuwa na abiria na
hakuna mtu aliyejeruhiwa.
No comments:
Post a Comment