Wanariadha wawili kati ya
wanariadha wenye kasi kubwa duniani -- Tyson Gay, kutoka Marekani na
Asafa Powell wa Jamaica -- wamepatikana na kosa kutumia madawa ya
kusisimua misuli.
Gay, ambaye ni mwanariadha wa pili kwa kuwa na
kasi kubwa ya kukimbia katika mbio za mita mia moja, amesema anajiondoa
kwenye mashindano ya dunia ya riadha yanayotarajiwa kufanyika mjini
Moscow mwezi ujao.
Asafa Powell, ambaye alishikilia rekodi ya mbio za mita 100 hadi ilipovunjwa na Usain Bolt mwaka 2008, amekanusha kuwa alitumia dawa hizo makusudi.
Mwanariadha mwenzake wa Jamaica Sherone Simpson pia amepatikana na hatia ya kuzitumia dawa hizo za kusisimua misuli.

BBC SWAHILI
No comments:
Post a Comment