ADV

ADV

ADVERTISEMENT CORNER

HUDUMA YA KUKATA TICKET ZA NDEGE ONLINE


SOMA HABARI

SOMA HABARI

Wednesday, August 14, 2013

Bilionea Erasto Msuya azikwa. Jeneza lake linatumia remote control kufunguliwa na kufungwa.

  
ments

IMG-20130812-WA0011

Mchungaji Abeli Msuya na mkewe wakitoa sala mbele ya jeneza la marehemu.




Familia ya marehemu katika ibada ya kumwaga marehemu Erasto Msuya iliyofanyika  Jumatatu huko  Sakina Arusha.
IMG-20130812-WA0006
Dada wa marehemu Erasto Msuya  katika ibada ya kumwaga marehemu kaka yake Erasto Msuya nyumbani kwake Sakina Arusha
IMG-20130812-WA0008
Ndugu jamaa na marafiki wakiwa na majonzi.
IMG-20130812-WA0010
Mchungaji Mwanga akitoa neno katika ibada hiyo.
IMG-20130812-WA0007
 
 Hapa utaratibu wa kutoa heshima za mwisho kwa mwili wa Maremu Erasto Msuya.


 Hii ndio nyumba ya milele ya bilionea Erasto Msuya ikiandaliwa.
MIRERANI zikiwa ni siku takribani sita zimepita tangu mfanyabiashara wa madini ya Tanzanite aliyefahamika kwa jina la Erasto Msuya kupigwa risasi zaidi ya ishirini na kufariki dunia papo hapo katika eneo la Bomang'ombe karibu na njia panda ya KIA (Kilimanjaro International Airport). Kifo hicho kilichokua na utata mkubwa na kupelekea watu wengi kujiuliza maswali mengi yasiokua na majibu. Jana ilikua ni siku ya mazishi ya mfanyabiashara huyo ambaye kutokana na kuwa alikua akiishi jijini Arusha maeneo ya kwa Iddi ilibidi juzi jumatatu wafanye utaratibu wa kuuga mwili wa marehemu nyumbani kwake na jana Jumanne kwenda kuzikwa Mirerani katika kijiji cha Kairo. 
       Msiba wa Erasto ulikua ni gumzo kubwa sana na watu wamekiri hawajawai kuona msiba kama huu maana kilichokua kikiwashangaza watu ni jeneza lililokua likifunguliwa kwa rimoti, na pia ni mazishi yaliyokua na watu wengi sana. Kila kona kulikua na minong'ono ambayo ilikuwa ikizungumzia utata wa kifo chake. Kamati ya maandalizi ya mazishi wakishirikiana na ndugu, jamaa na marafiki walijitahidi sana kuhakikisha kila kitu kinakwenda sawa maana haikuwa kazi rahisi kuweza kumudu kuhakikisha usalama wa wingi wa watu uliokuwepo katika mazishi ya Erasto. 

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...