Jeshi
la Polisi Tanzania limetoa majina na ratiba ya usahili kwa vijana
waliomaliza kidato cha nne mwaka 2012 na waliomaliza kidato cha sita
mwaka 2013 ambao wamechaguliwa kufanya usaili kabla ya kujiunga na
Jeshi la Polisi.
Mikoa, vituo na tarehe za usaili zimeoneshwa kwenye jedwali hapa chini:
NA
|
MIKOA
|
KITUO CHA USAILI
|
TAREHE ZA USAILI
|
MUDA WA USAILI
|
1
|
KILIMANJARO NA TANGA | OFISI YA RPC TANGA | 02-04 /09/2013 | 08:00 ASUBUHI -16:00 JIONI |
2
|
MANYARA NA ARUSHA | OFISI YA RPC ARUSHA | 06-09 /09/2013 | 08:00 ASUBUHI -16:00 JIONI |
3
|
RUVUMA NA NJOMBE | OFISI YA RPC NJOMBE | 12-14 /09/2013 | 08:00 ASUBUHI -16:00 JIONI |
4
|
IRINGA NA MBEYA | OFISI YA RPC MBEYA | 16-18 /09/2013 | 08:00 ASUBUHI -16:00 JIONI |
5
|
RUKWA NA KATAVI | OFISI YA RPC RUKWA | 20-23 /09/2013 | 08:00 ASUBUHI -16:00 JIONI |
6
|
MTWARA NA LINDI | OFISI YA RPC MTWARA | 26-28 /09/2013 | 08:00 ASUBUHI -16:00 JIONI |
7
|
KIGOMA | OFISI YA RPC KIGOMA | 02-04 /09/2013 | 08:00 ASUBUHI -16:00 JIONI |
8
|
MWANZA NA MARA | OFISI YA RPC MARA | 06-09 /09/2013 | 08:00 ASUBUHI -16:00 JIONI |
9
|
GEITA NA KAGERA | OFISI YA RPC GEITA | 12-14 /09/2013 | 08:00 ASUBUHI -16:00 JIONI |
10
|
SHINYANGA NA SIMIYU | OFISI YA RPC SHINYANGA | 17-19 /09/2013 | 08:00 ASUBUHI -16:00 JIONI |
11
|
TABORA NA SINGIDA | OFISI YA OCD NZEGA | 21-24 /09/2013 | 08:00 ASUBUHI -16:00 JIONI |
12
|
MOROGORO NA DODOMA | OFISI YA RPC DODOMA | 26-28 /09/2013 | 08:00 ASUBUHI -16:00 JIONI |
13
|
DSM NA PWANI | DSM POLICE ACADEMY | 01-03 /10/2013 | 08:00 ASUBUHI -16:00 JIONI |
Muhimu:
- Mwombaji anaruhusiwa kufanya usaili kwenye kituo chochote cha usaili kilicho karibu naye kulingana na tarehe zinavyoonesha kwenye jedwali hapo juu ili mradi tu awe amejiridhisha kuwa ni miongoni mwa walioitwa kwenye usaili. Jeshi la Polisi halitahusika na lawama yoyote ile kwa mtu atakayekwenda kwenye kituo cha usaili hali ambapo jina lake si miongoni mwa walioitwa kufanya usaili.
- Mwombaji aliyeitwa kwenye usaili aje na vyeti vyake vyote vya masomo [(Academic Certificate(s)/Results slip(s) & Leaving certificate(s)], nakala halisi ya cheti cha kuzaliwa (Original Birth certificate). Hati ya kiapo cha kuzaliwa haitakubalika.
- Mwombaji awe na namba ya simu itakayotumika kumjulisha endapo atachaguliwa..
- Kila mwombaji aliyeitwa kwenye usaili atajigharamia usafiri, chakula na malazi kwa muda wote wa zoezi la usaili. Pia waombaji waje na kalamu za wino kwa ajili ya usaili wa kuandika.
Ni muhimu sana kwa kila mwombaji kuzingatia muda wa kuanza usaili.
No comments:
Post a Comment