ADV

ADV

ADVERTISEMENT CORNER

HUDUMA YA KUKATA TICKET ZA NDEGE ONLINE


SOMA HABARI

SOMA HABARI

Wednesday, August 28, 2013

Mtanzania mwingine akamatwa tena na madawa ya kulevya ya mamilioni ya fedha huko Dubai


Photo of a woman caught with Dhs3 million of drugs.Photo: Yahoo! News
 
Mwanamke mmoja raia wa Tanzania amekamatwa katika uwanja wa ndege wa Dubai akiwa na madaawa ya kulevya katika begi lake akitokea Brazil.  Mwanamke huyo  aliwaambia maafisa wa police wa Dubai kuwa alialalikwa na alipewa ofa na mumewe kwenda Brazil kupumzika kwa miezi mitatu.
Lakini akiwa katika mapumziko yake hayo, rafiki ya mume wake alimwomba amsaidie kupeleka mabegi yake Tanzania. Katika mojawapo ya mabegi hayo Police wa Dubai walikuta madawa ya kulevya yenye uzito wa kilo tatu wenye dhamani ya mambilioni ya pesa. 
Hivi karibuni Watanzania wengi hasa vijana wamekuwa wakikamatwa wakisafirisha madawa ya kulevya katika kiwango cha juu kabisa. Vijana wengi wanaenda Bondeni kwa ajili ya kutumika kama punda wa kubebea mizigo hiyo ya matajiri ambao huwa hawaonekani wala kujulikana. Limekuwa jambo la kawaida kwenda Airport kupokea miili ya vijana wetu wanaofia huko South na wengi wakiwa katika harakati hizo hizo za biashara ya unga. 
Kusoma, kutafuta ajiram kujiajirim na kufanya kazi halali kwa bidii ndiyo njia pekee ya kujikwamua katika wimbi la umaskini. Biashara ya madawa ya kulevya ni njia ya mkato isiyo sahihi na ina madhara kwa muuzaji, msambazaji na mtumiaji.
Habari ya biashara haramu ya madawa ya kulevya Tanzania imeendelea kutikisa vichwa vya habari sehemu mbalimbali duniani. Hii ni aibu kwa Taifa letu, ni hatari kwa kizazi hiki na kizazi kijacho. Vijana fursa zipo nyingi za kilimo na biashara. Soko la ndani ni kubwa sana. Ardhi ni kubwa sana, tuchangamkie fursa za "kilimo kwanza" ambazo wenzetu wa eshia wanazichangamikia na kukopa matrekta kisha kuja kutulimishia sisi kwa hela nyingi. Katika vikundi tunakopesheka. Tusisubiri ardhi ichukuliwe yote na Wakenya na Warwanda na Wazomali halafu sisi tuje kuwa vibarua wao. Kama wageni wanaziona fursa nyingi hapa na wanamiminika kila siku kuja kuishi na kuomba uraia Tanzania, kwa nini sisi hatuzioni? Tunatafuta njia za mkato tuuuu! "Easy come easy go" Tufanye kazi kwa bidii tuache bla bla, tuache siasa chafu, tuache vijiwe visivyokuwa na maana. Hata waliomaliza vyuo vikuu, kupata shahada haina maana ni lazima tu uajiriwe, ina maana una upeo na uwezo mkubwa zaidi wa kupambanua fursa zilizopo na kuzichangamikia. Si ajabu utamaliza shahada halafu ukaenda kufuga samaki, kuku wa mayai, kuku wa nyama, ng'ombe.. kulima, kufanya biashara ya mazao au biashara nyingine itakayokupa tija. Nawajua watu wengi (nikiwemo mimi) waliokataa dhana ya kuajiriwa hata kama wana vigezo na kuamua kujiajiri wenyewe na sasa wana maendeleo makubwa.
Taifa letu halitajengwa na biashara haramu ya madawa ya kulevya bali litabomolewa vipande vipande.
 
--
A cross-post from Yahoo! News — A woman caught with Dhs3 million of drugs in her suitcase claims she was unwittingly being used as a mule by her husband, Dubai Police said.

The Tanzanian woman was arrested at Dubai International Airport in transit to her home country from Brzail. She claims her husband arranged for her to go on a three-month trip to Brazil so that she could unwind.

However, she told officers that while on holiday, a friend of her husband asked her to take some bags back to Tanzania. She was arrested in Dubai after officers at the airport became suspicious of her behavior. They found 3kg of cocaine in her luggage, worth Dhs3 million.

“She claimed that her husband got her in trouble as he offered her a relaxing trip to Brazil and she went for three months. Her husband’s friend asked her to deliver the bags to her husband in Tanzania,”an official in anti-narcotics said. The suspect has been referred to public prosecution.

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...