Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib
Bilal, akimsindikiza Rais wa Burundi, Pierre Nkurunzinza, wakati
akiondoka kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere leo,
baada ya kumaliza mapumziko yake ya siku tatu nchini.
Rais
wa Burundi, Piere Nkurunzinza, akiagana na baadhi ya maofisa wa Ofisi
ya Makamu wa Rais, waliofika uwanjani hapo kumsindikiza leo, baada ya
Rais huyo kumaliza mapumziko yake ya siku tatu nchini. Kushoto ni Makamu
wa Rais, Dkt. Mohammed Gharib Bilal.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib
Bilal, akiagana na Rais wa Burundi, Pierre Nkurunzinza, wakati
akiondoka kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere leo,
baada ya kumaliza mapumziko yake ya siku tatu nchini.
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal
na viongozi wengine, wakimuaga Rais wa Burundi, Pierre Nkurunzinza,
wakati akiondoka kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere
leo, baada ya kumaliza mapumziko yake ya siku tatu nchini.
--
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Mohammed Gharib Bilal
leo Alhamisi Agosti 29, 2013 amekutana na Rais Pierre Nkurunzinza katika
hoteli ya Hilton Double Tree na kufanya naye mazungumzo. Rais
Nkurunzinza alikuwa nchini kwa siku tatu kwa mapumziko na ameelezea
kufurahishwa kuwapo Tanzania na akaeleza kuwa Tanzania na Burundi ni
nchi zenye uhusiano wa kipekee na kwamba uhusiano huo umekuwepo na
utaendelea kuwepo kwa miaka mingi ijayo.
Kwa
upande wake Mheshimiwa Makamu wa Rais Dkt. Bilal alimueleza Rais
Nkurunzinza furaha yake kwa yeye kuchagua Tanzania kuwa sehemu ya
mapumziko yake na familia yake na kwamba Tanzania inazo fursa nyingi za
kitalii hali ambayo imewafanya viongozi wa nchi mbalimbali kupenda kuja
hapa. Makamu wa Rais alimtakia safari njema Rais Nkurunzinza na
kumueleza kuwa uhusiano wa nchi zetu unatufanya kuwa ndugu hivyo
anakaribishwa tena hapa nyumbani Tanzania.
Imetolewa na:
Ofisi ya Makamu wa Rais
Agosti 29, 2013, Dar es Salaam
No comments:
Post a Comment