Kufuatia tukio la wizi lililotokea leo katika benki ya Habib African iliyopo
Kariakoo jijini Dar es Salaam na kuibiwa zaidi ya shilingi milioni 900
za Tanzania, Jeshi la Polisi limetangaza dau la shilingi milioni moja
kwa mtu yeyote atakayefanikisha kukamatwa kwa majambazi yaliyofanya
hicho kitendo. Majambazi hayo yaliyokuwa yamevaa sare za Jeshi la Polisi yalivamia benki hiyo na kupora Dola za Kimarekani 181,885 sawa na shilingi milioni 293.9
za Tanzania. Pia yalipora jumla ya shilingi milioni 700 za Tanzania na
kufanya jumla ya fedha zilizoibiwa kuwa shilingi milioni 993.9.
No comments:
Post a Comment