Kamanda wa Polisi mkoa wa Katavi
Dhahiri Kidavashari akiinua juu Pasi iliyokuwa ikitumiwa na matapeli
kuwatapeli wananchi wa mji wa mpanda mkoa wa katavi na wametiwa nguvuni
kwenye nyumba ya kulala wageni ya Vatikani Mjini MPANDA
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Katavi
Akiinua juu zana zilizokuwa wakitumiwa na mtandao wa matapeli kutoka
mwanza sumbawanga na mpanda vilivyokata na jeshi la polisi na
kusmbalatisha mtandao huo
Waliokaa
kwa huzuni ni baadhi ya matapeli wanajiita waganga wa jadi wakiwa chini
ya ulinzi wapolisi ofisi ya kamanda wa polisi mkoa wa katavi
wakituhumiwa kwa kuwatapeli wananchi wa mji wa mpanda wakiwa mbele ya
kamanda wa polisi na mkutano wa waandishi wa habari hawapo pichani.Picha Zote na Kibaavida Kibada Kat
---
Na Kibada Kibada, Katavi
POLISI
mkoani Katavi imeubaini mtandao wa matapeli uliojitanua katika
mkoani humo pia katika mikoa ya Rukwa na Mwanza kwa kuwatia
nguvuni vinara wake akiwemo mwanamke mmoja wakituhumiwa kutapeli
watu kwa kujifanya wanatoa huduma za uganga wa jadi pasipo kuwa
na kibali .
Kamanda
wa Polisi mkoani hapa , Dhahiri Kidavashari aliwataja vinara wa
matandao huo wa kitapeli kuwa ni pamoja na Issa Hassan(42) ,Hussein
Hassan maarufu Rwango (38) wakiwa wakazi wa jijiji la Mwanza,na
Magreth Bakari (45) mkazi wa Mtaa wa Nsemlwa mjini Mpanda mkoani
Katavi Charles Mwelela (38.)akiwa ni mkazi wa sumbawanga mkoani Rukwa.
Alibainisha
hayo jana wakati akizungumza na waandishi wa habari ofisini
kwake huku akiwaonesha watuhumiwa hao wanne pia tunguli zao
wanazodaiwa kuzitumia kutapeli wananchi mbalimbali nchini ambapo
Agosti 26 mwaka huu , saa tano usiku watuhumiwa hao walikamatwa
katika Mtaa wa Mji mwema mjini hapa katika nyumba ya kulala wageni
iitwayo Vatikani .
Miongoni
mwa tunguli hizo alizozioensha kwa waandishi wa habari na baadhi
ya maofisa wa polisi ni pamoja na ndege aliyekaushwa ambaye
hutumika kwa kuwafanya wanaume watii kila kitu wanachoamriwa na
wake zao ikiwemo kupika hadi kufua nguo za wake zao .
Pia
alionesha unga mweupe ambao watuhumiwa hao walikuwa wakitumia
kuwalevya watu kwa kuwawekea kwenye vileo na kuwaibia fedha zao
zote kisha hutokomea kusikojulikana pia wamekutwa wanawatapeli
watu kwa kuwadanganya kuwa wana pasi ya Mjerumani ambayo ni feki
ambao inauzwa kwa zaidi ya milioni 20 kwa madai kuwa ina uwezo wa
‘kuzalisha “mabilioni ya fedha .
Kwa
mujibu wa Kamanda huyo watuhumiwa hao wanadai kuhusishwa na
matukio ya kitapeli ambapo baadhi ya wafanyabiashara kadhaa
wametapeliwa mamilioni ya fedha baada ya kuwekewa unga mweupe
wenye uwezo wa kumlaza mtu kwa saa kadhaa kabla hajazinduka .
“Uchunguzi
wa awali wa kipolisi umebaini kuwa watuhumiwa hawa hutapeli watu
kwa mtindo wa kuwapa madawa ya kulevya na muda mwingine huwa
wanawatapeli watu kuwa wana pasi ya Mjerumani ambayo ni
feki na kuwataka watoe fedha zao pasipokujua kuwa wanatapeliwa’
alisisitiza Kamanda Kidavashari .
Kwa
mujibu wa Kamanda watuhumiwa hao watatu wa kiume wanadaiwa kukaaa
kwenye vyumba vya nyumba mbalimbali za kulala wageni wageni
mjini hapa wakisubiri wateja wao huku mtuhumiwa huyo wa kike
anakuwepo nje akitafuta wateja kutoka kona mbalimbali za mjini
hapa .
“Mwanamke
huyo awapatapo wateja hao huwapeleka kwenye vyumba walimo
watuhumiwa wa kiume kwa ajili ya kutapeliwa akijifanya kuwa naye
pia ni mteja kama wao……. Bahati mbaya sana kutokana na jinsia yake
ya kike ni rahisi mno kumuamini bila kuwa na hofu naye kwa ni
wanawake wachache wanaojihusisha katika matukio ya kitapeli mjini
hapa” alisema .
Kwa
mujibu wa Kidavashari watuhumiwa hao wote wanatarajiwa kufikishwa
mahakamani wakati wowote mara tu uchunguzi wa awali wa kesi yao
utakapokamilika.
No comments:
Post a Comment