Usher akiwa na mwanaye

Jumba la Usher Raymond

Bwawa ambalo mtoto wake alikwama

Moja ya gari ghali la Usher Raymond
Nyumba yake katika video
Mtoto wa kwanza wa Usher Rymond, Usher Raymond V, amelazwa katika chumba cha wagonjwa mahututi baada ya kukwama kwa muda katika bwawa la kuogelea la nyumbani kwao Juzi Jumatatu tarehe 5.
Mtoto huyo alifikwa na mkasa huo wakati akicheza na na shangazi yake wakati alipoamua kupiga mbizi ndani na bwawa la kuogelea kuchukua mdoli wake aliyekuwa amezama humo.
Wakati akijaribu kumwokoa mdoli wake, mkono wake ulinasa katika chekecheke inayochuja maji chini kabisa ya bwawa na hivyo kumfanya dogo huyo ashindwe kurudi juu. Baada ya shangazi yake kuona mtoto harudi kwa wakati aliamua kumfuata huko chini lakini naye alishindwa kumnasua na wakati huo mtoto alikuwa akiendelea kukosa hewa na kunywa maji. Ndipo shangaza alipoamua kupiga mayowe kuomba msaada.
Wafanyakazi wawili wa kiume waliokuwa ndani ya jumba hilo walitoka na kuzama ndani ya bwawa na kumnasua mtoto huyo ambapo wakati huo alikuwa katika hali mbaya kabisa. Alifanyiwa huduma ya kwanza ijulikanayo kwa kitaalamu CPR kabla hajakimbizwa hospitalini ambapo alipelekwa moja kwa moja katika chumba cha wagonjwa mahututi. Asher (baba) mwenyewe aliweza kufika kwa wakati na kufanikiwa kuondoka na mwanaye kwenda hospitalini.

Unakumbuka pia kwamba Usher ana mtoto mwingine wa miaka minne ambaye aliachwa na mama yake waliyeachana Tameka foster, mtoto aitwaye Naviyd Ely Raymond.
Huu ni mkasa mwingine umemtokea nyota huyo baada ya mtoto aliyekuwa akimlea (wa mke wake Foster) aitwaye Kile Glover kupata ajali ya majini mwaka jana Julai, na kufariki dunia.
No comments:
Post a Comment