ADV

ADV

ADVERTISEMENT CORNER

HUDUMA YA KUKATA TICKET ZA NDEGE ONLINE


SOMA HABARI

SOMA HABARI

Wednesday, August 7, 2013

Mwanamke amdanganya Trafiki juu ya kifo cha baba yake kukwepa faini


 

Mwanamke mmoja wa huko New Hampshire USA ameonja joto ya jiwe baada ya uwongo wake kuvaliwa njuga na Trafiki aliyeifanya kazi yake zaidi ya kawaida. Mwana mama huyo aliondolewa barabarani baana ya rada ya trafiki  Cummings kunasa gari yake ikienda mwendo wa 82 MPH wakati eneo lile lilitakiwa speed ya 65 MPH.
Baaya ya Trafiki Commings kushikilia leseni yake, mwanamke huyo aliyeonekana katika hali ya majonzi alimwambia trafiki kuwa ana baba yake hospitalini, anaugua kansa hatua ya nne na kwamba mapigo yake yalikuwa yakipiga mara sita tu kwa dakika hivyo alikuwa akiwahi kumwaga kabla hajafariki dunia. Kwa hali ya huzuni aliyokuwa nayo trafiki Commings alimrudishia leseni yake haraka na kumruhusu aende kumwaga baba yake kabla hajakata roho.
Hata hivyo, trafiki Christopher J. Cummings aliamua kumuuliza amtajie jina la baba na hospitali aliylazwa, mwanamama Williams bila kusita alitaja. Baadaye trafiki Commings alipiga simu hospitalini kuuliza mgonjwa yule lakini aliambiwa hakuna mgonjwa mwenye jina hilo pale hospitalini. Commings alifadhaaika sana kuona kwamba binadamu anaweza kujiweka katika hisia za huzuni kiasi kile na zaidi kudanganya kiasi kile. Trafiki Commings hakuishia hapo, aliamua kuingia kwenye mtandao na kutafuta taarifa za Carley Williams, ndipo alipogundua kuwa jina la baba yake alilitaja lilikuwa kwenye listi ya watu waliokufa tangu mwaka 2008, kwamba baba yake alishafariki kitambo lakini Carley akaamua kutumia jina hilo la marehemu kana kwamba bado yuko hai na ndiyo anakaribia kukata roho. Afande yule anayefanya kazi yake inavyostahili aliendelea kumpekua Carley kwenye mtandao na kugundua pia kwamba gari lile alilokuwa akiendesha lilishafutiwa usajili.
Jumapili iliyopita Commings akamfuata Carley nyumbani kwake na kumwonyesha cheti cha kifo cha baba yake, Carley aliangalia chini kwa aibu lakini bado anaendelea kukataa kuwa yule sio baba yake ila mjomba wake. Hata hivyo afande Commings alimwambia kwamba hakumjia kwa kosa lile la udanganyifu ingawa lilimuumiza sana, ila amekuja kumkamata kwa kosa la kuendesha gari lililoondolewa kabisa kwenye usajili wa magari. Carley Williams alipelekwa kituo cha polisi cha Nashua kwa kosa la kuendesha gari lisilosajiliwa.
Trafiki Commings anasema kwamba alishazoea kudanganywa na wavunja shera za barabarani na mambo mengine alikuwa anayachukulia poa tu lakini hili la Carley limekuwa kubwa na limemsumbua sana kichwa kuona ni kwa namna gani binadamu anaweza utumia uongo tena unaohusisha marehemu kukwepa mkono wa sheria.


No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...