ADV

ADV

ADVERTISEMENT CORNER

HUDUMA YA KUKATA TICKET ZA NDEGE ONLINE


SOMA HABARI

SOMA HABARI

Wednesday, August 28, 2013

WAKAZI WENGI WA MBEZI BEACH TEGETA NA WAZO WABOMOLEWA MAKAZI YAO KUPISHA BOMBA LA MAJI

 

dawasa_7af8f.jpg
   
Baa maarufu ya Samaki Samaki iliteketea kwa moto wakati wakiwa katika harakati za kubomoa kupisha ujenzi wa bomba la maji

Wakazi wa Mbezi Beach, Tegeta na Wazo katika Manispaa ya Kinondoni wamelalamikia kazi ya ubomoaji wa nyumba zao ili kupisha utandazaji wa bomba la majisafi la Mamlaka ya Majisafi na Majitaka Dar es Salaam (Dawasa), kwamba inafanywa kwa ubaguzi.Hata hivyo, ilielezwa kuwa Dawasa ilitoa siku 14 kwa wakazi hao kubomoa nyumba zao zipatazo 400 kupisha mradi huo wa bomba utakaogharimu Sh120 bilioni.
Dawasa imelaumiwa kutokana na baadhi ya nyumba za vigogo na watumishi wa Serikali kuachwa licha ya kuwekewa alama ya X kuashiria zinatakiwa kubomolewa.
Mwandishi wa Mwananchi aliyekuwa eneo la tukio, alishuhudia baadhi ya wananchi hao wakidai kuwa moja ya nyumba ambayo imeachwa ni ya ndugu wa mmoja wa vigogo wa Serikali.
Wakizungumza kwa nyakati tofauti jana huku ubomoaji ukiendelea, mmoja wa waathirika wa bomoabomoa hiyo, alilalamikia ubomoaji kufanyika kibaguzi.
Juma Shaaban alisema: "Ninashangaa kuona tunabomolewa nyumba zetu huku nyumba zao zinaachwa,"Ninaweza kukuonyesha nyumba ya ndugu yake kigogo (anamtaja) imewekewa X, lakini chakushangaza haijabomolewa, hii tulalamike."alisema.
Mkazi mwingine wa Tegeta, Khamis Ramadhani alisema: "Tunashangazwa na bomoabomoa hii kufanyika bila hata kutupa muda wa kuhamisha mali zetu."
Katika hatua nyingine, bomoabomoa inayoendelea ilisababisha hitilafu ya umeme na kusababisha moto ulioteketeza Baa maarufuya Samaki Samaki.
Moto huo ulitokea Saa 4 asubuhi na kusababisha watu kujaa na kufungwa barabara kwa muda ili kuzima moto huo kabla ya magari ya kuzima moto kuwasili eneo la tukio
MWANANCHI

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...