Meli ya kivita ya Marekani ikiwa tayari na ndege zake na makombora yake kusbiri amri ya kuishambulia Syria.
Shambulio la gesi ya sumu lililofanyika tarehe 21 August Jijini Damascus alfajiri wakati watu wakiwa wamelala ni la kwanza kutokea tangu lile la mwaka 1988 wakati Saddam Hussein alipowanyunyizia gesi ya sumu Wakurdi na kuua maelfu. Rais Obama anasema kuwa, Asaad asipoadhibiwa, ni hatari kwa viongozi wengine wa kiimla kutumia gesi wakijua kwamba hakuna atakayewafanya kitu. Pia ni hatari kwa nchi jirani zinazoizunguka Syria.
Ufaransa inatarajia pia kujiunga na Marekani katika kumwajibisha rais Assad. Uingereza ambayo ilikuwa imeshajiandaa ilijikuta iliwekwa pembeni baada ya wabunge wanaopinga mpango wa kuishambulia Syria kijeshi kushinda hivyo Uingereza kujitoa.
Urusi ambaye ni mshirika mkubwa wa Assad na ndiye anayemuuzia silaha imekuwa ikipinga matumizi yeyote ya nguvu huko Syria na kwamba Assad asingeweza kutumia sumu kwa wananchi ake. Rais Putin amewaambia waandishi wa habari kwamba huenda waasi waliitumia sumu hiyo ili Assad aweze kushambuliwa.
Wafanyakazi wa Umoja wa mataifa wameshaondolewa na nchi mbalimbali zimewaasa raia wake kutembelea Syria na Lebanon.
Huko Syria kwenyewe, wananchi wamekuwa na hofu nyingine, siyo hofu ya kushambuliwa na vikosi vya rais Assad au waasi bali ni hofu ya kulipuliwa na makombora mazito ya Marekani. Kijana mmoja aliyeonakana amebeba begi alikuwa akihaha ni wapi ataficha document zake maana hajui ni wapi palopo salama. "Do I put them in my parents' home? My in-laws? At work? I don't know which area is safer, I don't know where to hide them,"
Madaktari pia wamejiandaa kukabiliana na hali yeyote itakayojitokeza hasa kama itatokea kuwa gesi ya sumu itatumika dhidi ya watu
Wakati huo huo waasi wanaopigana kuiangusha Serikali ya rais Assad wamepokea ujio wa makombora ya Marekani kama baraka kwao na sasa wanaandaa mashambulizi sambamba na ya marekani ili waweze kukamata maeneo ambayo yatakuwa yamelipuliwa na marekani, ingawa Obama anasema si kazi yake kubadilisha utawala nchini Syria bali kumpa adhabu bwana Assad.
Wakati rais Assad akisaidiwa na Washia wenzake kama Iran na Hesbolaa, waasi wa Syra ambao ni Wasuni wanasaidiwa na Nchi nyingine za kiarabu kama Saudi, Quarter, Jordanm Uturuki....
Hata hivyo makundi ya waasi ambayo yameelekea kumpiga sana Assad ni makundi ya Alqueda ambayo yamezifanya nchi za Marekani na za Magharibi kuogopa kutuma silaha kwa waasi wa Syria wakihofia huenda zikaingia mikononi mwa makundi hayo hatari.
No comments:
Post a Comment