Mhe. Membe akitoa shukrani kwa Baraza
la Usalama la Umoja wa Mataifa kupitia Mabalozi hao kwa kulaani mauaji
ya Mwanajeshi wa Tanzania yaliyotokea huko Mashariki mwa DRC tarehe 28
Agosti, 2013 kwa kushambuliwa na kundi la Waasi la M23 wakati Kikosi
cha Kulinda Amani cha Umoja wa Mataifa (MONUSCO)kwa kushirikiana na
Majeshi ya Serikali ya DRC na Force Intervention Brigade (FIB) wakilinda
amani. Anayesikiliza kwa makini ni Mhe. Alfonso Lenhardt, Balozi wa
Marekani hapa nchini.
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano
wa Kimataifa, Mhe. Bernard K. Membe (Mb.) akizungumza na Mabalozi
wanaowakilisha nchi zao hapa nchini ambao pia nchi zao ni Wanachama wa
Kudumu wa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa (Permanent 5) kuhusu
hali inayoendelea Mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC).
Mhe. Membe pia aliwapa taarifa za kuitishwa kwa Mkutano wa Dharura wa
Wakuu wa Nchi na Serikali wa Nchi za Ukanda wa Maziwa Makuu (ICGLR)
utakaofanyika mjini Kampala, Uganda tarehe 5 Septemba, 2013 kuhusu DRC.
Nchi tano wanachama wa Baraza la Kudumu la Usalama la Umoja wa Mataifa
ni China, Marekani, Ufaransa, Uingereza na Urusi. Mkutano na Mabalozi
hao umefanyika Wizarani tarehe 30 Agosti, 2013.
Balozi wa China hapa nchini, Mhe. Lu
Youqing (kushoto) akitafakari jambo wakati wa mazungumzo yao na Mhe.
Membe (hayupo pichani). Wengine ni Mkurugenzi wa Idara ya Ushirikiano wa
Kimataifa katika Wizara ya Mambo ya Nje, Balozi Celestine Mushy (kulia)
na Afisa kutoka Ubalozi wa China.
Balozi wa Uingereza hapa nchini, Mhe.
Diana Melrose (wa tatu kushoto) akiwa na Wajumbe kutoka Urusi, Ufaransa
na Marekani wakati wa Mkutano wao na Mhe. Membe (hayupo pichani) kuhusu
hali nchini DRC.Picha na Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa
No comments:
Post a Comment