Wachezaji wa Baraca wakishangilia pointi tatu (HM)
Lionel Messi akifunga bao
Lionel Messiamejibu mapigo ya mpinzani
wake, Cristiano Ronaldo wa Real Madrid baada ya kuifungia hat-trick
Barcelona katika ushindi wa 4-0 dhidi ya Ajax katika mchezo wa Kundi H
Ligi ya Mabingwa Ulaya, Uwanja wa Nou Camp.Muargentina huyo pamoja na kufunga mabao matatu peke yake usiku, pia alitengeneza bao la nne lililofungwa na Gerard Pique.
Haikuwa bahati yao, Ajax kwani walikosa hadi penalti baada ya kipa Victor Valdes kuokoa mkwaju wa Kolbeinn Sigthorsson.
Messi alifunga mabao yake katika dakika za 22, 55 na 75, wakati Pique alifunga dakika ya 69.
Kikosi cha Barcelona kilikuwa: Valdes, Alves, Pique/Bartra dk80, Mascherano, Adriano, Busquets, Fabregas/Xavi dk72, Iniesta, Sanchez, Messi, Neymar /Pedro dk72.
Ajax: Vermeer, van Rhijn, Denswil, Moisander/van der Hoorn dk73, Blind/Schone dk78, Poulsen, de Jong/Serero dk59, Duarte, Bojan, Sigthorsson na Boilesen.
Chanzo: binzubeiry
Katika michezo mingine matokeo ni
Schalke 3-0 Steaua
Milan 2-0 Celtic
Atlético 3-1 Zenit
Austria Wien 0-1 Porto
Chelsea 1-2 Basel
Marseille 1-2 Arsenal
Napoli 2-1 Dortmund
No comments:
Post a Comment