Msemaji wa Jeshi la Ulinzi la
Wananchi wa Tanzania (JWTZ) Meja Erick Komba akiongea na waandishi wa
habari leo katika ukumbi wa mikutano uliopo makao makuu ya Jeshi
hilo jijini Dar es Salaam kuhusu ushiriki wa Tanzania katika operesheni
ya ulinzi na amani katika nchi ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo
(DRC). Tanzania ni moja kati ya nchi tatu zilizopeleka kikosi chake
nchini DRC ikiwa ni sehemu ya SADC standby brigade inayotoa mchango wake
katika Jeshi la Umoja wa Mataifa (MONUSCO) na kinafanya kazi chini ya
Force Commander huku majukumu yake yakiwa ni kuzuia waasi kujitanua,
kuvunja nguvu ya waasi na kuwapokonya silaha makundi yote ya waasi.
Kulia ni Mkurugenzi wa Idara ya Habari (Maelezo) Assah Mwambene.
Mkurugenzi wa Idara ya Habari
(Maelezo) Assah Mwambene akiongea na waandishi wa habari jinsi baadhi ya
vyombo vya habari vinavyoandika taarifa
zisizo sahihi kuhusu ushiriki wa majeshi ya Tanzania katika
operesheni ya ulinzi na amani katika nchi ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya
Congo (DRC) ikiwa ni sehemu ya SADC standby brigade inayotoa mchango
wake katika Jeshi la Umoja wa Mataifa (MONUSCO) . Kushoto ni Msemaji wa
Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) Meja Erick Komba.
Mkurugenzi wa Idara ya Habari
(Maelezo) Assah Mwambene (kulia) akimuonyesha kitu Msemaji wa Jeshi la
Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) Meja Erick Komba wakati wa mkutano
na waandishi wa habari uliofanyika leo katika ukumbi wa mikutano
uliopo makao makuu ya JWTZ jijini Dar es Salaam. Mkutano huo uliongelea
juu ya ushiriki wa Tanzania katika operesheni ya ulinzi na amani katika
nchi ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC).
Mwandishi wa Habari na Mpiga picha
Mwandamizi wa kituo cha Televisheni cha channel 10 Kibwana Dachi
akiuliza maswali wakati wa mkutano uliofanyika leo katika ukumbi wa
mikutano wa Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) jijini Dar
es Salaam. Mkutano huo uliongelea juu ya ushiriki wa Tanzania katika
operesheni ya ulinzi na amani katika nchi ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya
Congo (DRC). Wanaomsikiliza kwa makini ni Msemaji wa JWTZ Meja Erick
Komba (kushoto) na Mkurugenzi wa Idara ya Habari (Maelezo) Assah
Mwambene(kulia).Picha na Lorietha Laurence-Maelezo
--
Simu
ya Mdomo : DSM 22150463
Sanduku la Posta 9203,
Telex :
41051 DAR ES SALAAM, 06 Sep
Ushiriki wa
Tanzania katika Operesheni ya Ulinzi wa Amani nchini DRC, unatokana na mgogoro kati ya Serikali DRC na waasi hususan
kikundi cha waasi cha M23. Mgogoro huo ulianza mwezi Aprili 2012 ambapo kikundi
cha M23 kilijitoa katika Jeshji la serikali ya DRC na kuanzisha mapigano hali
iliyopelekea hali ya usalama nchini DRC kuwa mbaya.
Kufuatia
hali hiyo mbaya ya usalama, wakati wa kikao cha International Conference on the
Great Lakes Region kilichofanyika tarehe 12 Julai 2012 mjini Addis Ababa,
Ethiopia, Mhe. Rais Joseph Kabila aliwasilisha ombi kwa Wakuu wa Nchi za Maziwa
Makuu ambazo Rwanda, Uganda, Tanzania, na DRC akaomba nchi wanachama wa Maziwa Makuu
zisaidie kuwapokonya silaha waasi wa M23.
Wakuu wa
nchi za Maziwa Makuu walikubaliana na ombi hilo na kutoa maelekezo kwa Mawaziri
wa Ulinzi ambao walikutana tarehe 01 hadi 2 Agosti 2012 na kujadili maelekezo ya Wakuu wa nchi za
Maziwa Makuu. Mawaziri wa Ulinzi walikubaliana
kuwa ni muhimu kwa vikundi vyote vya Waasi (ADF, FDLR na M23) kushughulikiwa
na wakawasilisha mapendekezo yao kwa Wakuu wa Nchi za Maziwa Makuu.
Tarehe 7 Agosti
2012, Wakuu wa nchi za Maziwa Makuu walikutana tena mjini Kampala, Uganda na
kupanga mkakati wa kuanzishwa kwa ‘Neutral
Intervention Force (NIF)’ na nchi wanachama wa Nchi za Maziwa Makuu
zikaombwa kuchangia askari watakaounda ‘Neutral
Intervention Force (NIF)’ ambapo Tanzania iliombwa na ikahadi kuchangia
kikosi kimoja. Kikao hiki kilitoa maelekezo ya hatua inayofuata kwa Mawaziri wa
Ulinzi wa Maziwa Makuu.
Tarehe 7
hadi 8 Sep 2012, Mawaziri wa Ulinzi wa
maziwa Makuu, walikutana na kujadili utekelezaji wa uanzishwaji wa ‘Neutral Intervention Force (NIF)’.
Wakaunda ‘Military Assessment Team (MAT)’ kufanya tathmini ya tishio. Timu hiyo
ililifanya tathmini na kuwasilisha taarifa yake kwenye kikao cha Mawaziri wa
Ulinzi kilichofanyika tarehe 25 Oktoba 2012 mjini Goma, DRC na baadaye taarifa
hiyo iliwasilishwa kwa Wakuu wa Nchi za Maziwa Makuu ambao waliagiza
kushirikishwa kwa nchi wanachama wa Jumuiya ya maendeleo kusini mwa Afrika (SADC),
Umoja wa Afrika(AU) na Umja wa Mataifa(UN) ili kufanikisha mkakati huo.
Nchi
wanachamma wa SADC na Nchi za Maziwa Mkuu kwa pamoja walikubaliana na
kupendekeza SADC Standby Brigade ipelekwe DRC kama ‘Neutral Intervention Force (NIF)’. Kufuatia ridhaa hiyo nchi
wanachama wa SADC ziliombwa kuchangia ambapo nchi mbalimbali wanachama
zilikubali kuchangia, lakini Umoja wa Mataifa(UN) ilizipitisha nchi za
Tanzania, Afrika Kusini na Malawi kuchangia askari nguvu ya Brigedi moja kuunda
NIF ya MONUSCO.
Aidha, Umoja
wa Mataifa mwezi Januari 2013 uliridhia mapendekezo ya Wakuu wa Nchi za Maziwa
Makuu na Nchi wanachama wa SADC ya kuundwa ‘Neutral Intervention Force (NIF)’ na kupelekwa DRC. Kufuatia idhini
hiyo tarehe 28 Machi 2013, Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa lilipitisha Azimio (Resolution) namba 2098 (2013) na
kutoa jukumu maalumu la ulinzi wa amani nchini DRC, likijumuisha ushiriki wa Neutral Intervention Force (NIF) kama
sehemu ya MONUSCO, na ikaitwa ‘Force
Intervention Brigade (FIB)’ ambayo kikosi cha Tanzania ni sehemu ya Brigade
hiyo.
Kwa mantiki
hiyo ieleweke kwamba, Kikosi cha Tanzania kilichopo DRC ni sehemu ya SADC
standby brigade iliyotoa mchango wake katika Jeshi la Umoja wa Mataifa
(MONUSCO). Kinafanya kazi chini ya Force
Commander, MONUSCO na majukumu yake ni:
- Kuzuia waasi kujitanua (Prevention of Expansion)
- Kuvunja nguvu za waasi (Neutralization)
- Kuwapokonya silaha makundi yote ya waasi.
Kwa
kuzingatia kuwa kikosi chetu kiko chini ya majeshi ya Umoja wa Mataifa ya
MONUSCO, inamanisha kuwa Operesheni hiyo ni ya Umoja wa Mataifa, Tanzania haipigani na M-23 na haina tatizo na Rwanda kuhusiana na Operesheni hiyo na
ridhaa ya kikosi chetu kwenda DRC ilikubaliwa pia na Rwanda, nchi ambayo ni
mwanachama wa nchi za Maziwa Makuu. Aidha, Rwanda imesaidia sana kwa kuruhusu
kikosi cha Tanzania kupitisha watu, vifaa na zana katika nchi yake kupeleka
DRC.
Imetolewa
na:
Kurugenzi ya Habari na Uhusiano
Makao Makuu ya Jeshi.
Dar
es Salaam.
No comments:
Post a Comment