Katika hali isiyo ya kawaida mamba mkubwa mwenye futi 8 amezua tafrani
baada ya kuingia chini ya kitanda cha Mkurugenzi wa hoteli moja ya
kitalii iitwayo Humani iliyopo pembezoni mwa mto Turgwe huko nchini
Zimbabwe na kukaa zaidi ya masaa 8.
Mr Whittall, ambaye ni mkurugenzi wa hoteli hiyo alisema kuwa mamba huyo
aliingia kwa siri chumbani kwake na kukaa chini ya kitanda chake usiku
na kugundulika asubuhi ya siku iliyofuata.
Alisema kuwa mamba huyo alitoka nyuma ya pori lililopo karibu na hoteli
hiyo ambapo hata yeye alipoamka hakumuona na alining’iniza miguu yake
huku mamba huyo akiwa chini ya kitanda ambapo alitoka kwenda kupata
kifungua kinywa kwenye mgahawa wa hoteli hiyo.
Inaelezwa kuwa mamba huyo aligundulika na mfanyakazi aliyekuwa akifanya
usafi katika chumba hicho na kupiga mayowe yaliyomshtua Mr Whittall
ambapo alitoka mbio kwenda kushuhudia kulikoni na kumkuta mamba huyo
akiwa chini ya kitanda chake kumbe alilala naye kwenye chumba hicho
usiku mzima.
Mamba ni wataalam wa kujificha na ndiyo maana hunusirika kuuwawa na
wanyama wengine hususani binadamu hata wakiwa nje ya maji,alisema Mr
Whittall.
Na huweza kutulia sehemu moja kwa muda mrefu bila kugundulika na myama
yoyote hivyo kumtambua inakuwa ni vigumu hiyo ni kutokana na maumbile
yao yalivyo na hukimbilia ndani ya vichaka au kuingia kwenye nyumba kama
hotelini hapo kufuata joto hasa katika kipindi cha mvua na baridi kali
na alipenda kukaa chini ya kitanda hicho kwasababu kulikuwa na joto.
Mkurugenzi huyo alilazimika kuwaita wafanyakazi wengine ambao
walisaidiana kumuondoa mamba huyo kutoka kwenye chini ya kitanda na
kumtupa kwenye bwawa la hoteli hiyo.
No comments:
Post a Comment