ADV

ADV

ADVERTISEMENT CORNER

HUDUMA YA KUKATA TICKET ZA NDEGE ONLINE


SOMA HABARI

SOMA HABARI

Wednesday, September 25, 2013

UGAIDI KENYA: ALIYESHUHUDIA AELEZA KILA KITU




Wananchi waliokuwa ndani ya jengo la Westgate wakiokolewa.

Hicks alikuwa katika studio moja iliyopo maeneo hayo akitoa picha alizozawadiwa wakati wa harusi yake ili aziweke kwenye fremu wakati magaidi hao walipoanza kufyatua risasi na kuwaua kiasi cha watu 39 katika kipindi cha nusu saa, kwenye tukio baya zaidi la kigaidi kuwahi kutokea katika historia ya Kenya.

Alisema baada ya kusikia milio ya risasi, alikimbia kuelekea kwenye jengo hilo akiwa na kamera yake ndogo, wakati akimsubiri mke wake, Nichole Sobecki, ambaye pia ni mwandishi na mpiga picha amletee kamera yake kubwa kwa ajili ya kuchukua picha za tukio hilo.

Mtoto akiokolewa kutoka Westgate.

“Nilipotoka pale studio, sikuelewa sawasawa nini kilichokuwa kikiendelea kwa sababu kulikuwa na watu wengi waliokuwa wakikimbia kutoka ndani. Nilikwenda ndani na katika dakika moja niliweza kuona watu wakiwa wamepigwa risasi miguuni au tumboni na walikuwa wanasaidiwa na wenzao. Hali hiyo ilidumu kwa muda wa nusu saa.

“Eneo hili ndilo la bei mbaya zaidi hapa Nairobi, lina maduka makubwa (shopping centers) ambayo yana hadhi kama za nchi za Kimagharibi, kuna majumba ya sinema, super market na casino. Nimewahi kufika hapa kwa hiyo ninafahamu jinsi kulivyo kwa ndani,” alisema.


Alisema tangu mwanzo alipenda kuingia ndani akiwa na walinzi na alifanya hivyo baada ya kuwakuta katika mlango wa dharura uliokuwa ukitumiwa na watu waliokuwa wamejificha kuwakwepa magaidi hao. Kuanzia hapo, alisema askari waliingia ndani na kuanza kuingia kila duka kuwatafuta wauaji hao.

Mmoja wa majeruhi.

“Ninaiona picha yote ya pale, niliweza kuona miili mingi imelala chini, wengine wakiwa wamelaliana pembeni ya pale walipokuwa wakila. Ilionekana kila unapotazama kulikuwa na maiti. 

Wanajeshi hawakujua ni wapi wale magaidi walipokuwa kwa hiyo waliendelea kuwatafuta. Kuna nyakati tuliweza kushuhudia wakitupa mabomu au kupiga risasi. Katika majengo hayo, kuna maeneo mengi ambayo wangeweza kujificha au kuanzisha mashambulizi,” alisema shuhuda huyo ambaye alikaa na askari hao ndani ya jengo hilo kwa muda wa saa mbili.

“Ilikuwa ni muhimu sana kuwa nao, walikwenda kutoka eneo moja hadi lingine, wakati mwingine wakikimbia, wakati mwingine wakipekua katika kila kona, yaani ilikuwa ni operesheni hasa ya kijeshi.


“Kwa jinsi nilivyoona, walikuwa na kazi kubwa mbili. Moja ni kuwatafuta magaidi walipo na ya pili ni kuwatoa nje ya jengo raia waliokuwa wamejificha katika maeneo mbalimbali.


 Kulikuwa na raia wengi sana waliokuwa katika maduka, ndani ya kumbi za sinema, kwenye saluni na hotelini. Kila tulipopita, tuliwakuta watu wengi wakiwa wamejificha na wakiwa na hofu kubwa.”

Alipoulizwa kama kwa muda wote huo aliweza kumwona gaidi yeyote, akiwa hai au mfu, alisema hakumuona, zaidi ya majeruhi wengi na kiasi cha maiti kumi au 12.


Wanajeshi wakiwa tayari kuwakabili magaidi.

Mwandishi huyo alisema alichokiona, ni kitu kibaya na kwamba ni afadhali kwa mtu kuandika habari za vita vinavyoendelea Syria, Afghanistan au eneo jingine lolote kuliko ilivyokuwa Nairobi siku hiyo.

“Jambo kama hili linapotokea ni hatari kubwa na ni hatari zaidi kuliko kuwa Afghanistan au Syria au eneo lolote lenye vita duniani. Ukiwa huko utajua wapi uliposimama, nafasi uliyopo kati yako na mpiga risasi. Hili lilikuwa ni tukio la mauaji ya raia wasio na silaha, siyo vita. Hawa magaidi waliingia pale na kuwaua watu, wanawake na watoto, mtu yeyote aliyejitokeza mbele yao, hii siyo vita.”


Tyler Hicks, mzaliwa wa Sao Paulo, Brazil, ambaye ni mpiga picha, mwaka 2009, alishinda tuzo ya kimataifa baada ya kufanya kazi nzuri ya kuandika habari zilizokuwa zikiendelea za kigaidi katika nchi za Afghanistan na Pakistan.


Jumamosi iliyopita, wapiganaji wa kundi hilo ambalo linasakwa na majeshi ya Kenya katika ardhi ya Somalia yaliko maskani yao, walivamia katika jengo hilo na kuanza kufyatua risasi ovyo, kabla ya kuwateka watu wengine na kuwafungia eneo moja.


Tokea wakati huo, idadi ya vifo vya watu imekuwa ikiongezeka. Magaidi hao wanaodhaniwa kuwa kati ya kumi na 15, wakiwa na silaha nzito, haijulikani kitu gani watakifanya, hasa kwa kuwa wamezingirwa na vikosi mbalimbali vya usalama vya Kenya.


Baada ya siku mbili za sintofahamu miongoni mwa raia wa Kenya, hasa wakazi wa Jiji la Nairobi, ghafla juzi mchana kulisikika milio ya risasi na milipuko ndani ya jengo hilo, ambalo lilielezwa kuwa magaidi hao walikuwa wapo katika ghorofa za tatu na nne.


Baadaye moshi mkubwa ulionekana hewani, kufuatia mlipuko mkubwa ambao hata hivyo, ulidaiwa kutokana na magaidi hao kuwasha magodoro yaliyomo kwenye maduka hayo huku mapambano baina ya vyombo vya usalama na magaidi hao yakiendelea.


Askari wengi walionekana wakizunguka na kukimbia katika eneo hilo

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...