Rais
Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akiwa amembeba motto Paulo Muhangwa muda
mfupi baada ya kuzindua shule ya Msingi Ntulya wilayani Misungwi,Mkoani
Mwanza
Rais
Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akipanda mti wa kumbukumbu muda mfupi baada
ya kuzindua rasmi Shule ya msingi Ntulya,iliyopo kata ya Mondo, Wilayani
Misungwi,Mkoa wa Mwanza.
Rais
Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akisalimiana na bvaadhi ya watoto
waliohudhuria sherehe za ufunguzi wa Shule ya Msingi Ntulya,katika kata
ya Mondo,wilayani Misungwi
Rais
Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akisalmiana na baadhi ya wauguzi katika
hospitali ya wilaya ya Misungwi wakati wa uzinduzi wa huduma ya X Ray
katika hospitali hiyo
Rais
Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akiangalia ngoma za utamaduni wakati
alipowasili katika Wilaya ya Misungwi Mkoani Mwanza kuanza ziara ya
kikazi
Rais
Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akipata maelezoi katika hospitali ya wilaya
ya Misungwi wakati wa uzinduzi wa huduma ya X Ray katika hospitali hiyo.Picha na IKULU
--
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa
Jakaya Mrisho Kikwete amesema kuwa kazi kuu na kipimo halisi cha kiongozi
bora na hodari ni jinsi kiongozi anavyohangaikia maendeleo ya wananchi,
ubunifu wake wa kuwaongezea wananchi mapato na kujali kumaliza kero
zao.
Aidha, Rais Kikwete amesema kuwa kazi ya madiwani
nchini haiwezi kuwa ni kupokea posho za vikao ama kupima na kujigawia
viwanja bali iwe ni kupambana na umasikini wa wananchi ambayo ndiyo
kazi waliyoomba wakati wanatafuta kura za kuwa madiwani.
Vile vile, Rais amewataka madiwani wote nchini kutumia
haraka na ipasavyo fedha zinazotolewa kwa ajili ya ujenzi wa barabara
ndani ya halmashauri zao na siyo kuziweka hadi mwisho wa mwaka wa fedha
na kulazimika kuzirudisha kwenye Mfuko wa Barabara.
Rais Kikwete ameyasema hayo jana, Ijumaa, Septemba
6, 2013, wakati alipopokea Taarifa ya Maendeleo ya Wilaya ya Misungwi
wakati alipoanza ziara ya siku tano katika Mkoa wa Mwanza kukagua na
kufungua shughuli na miradi ya maendeleo.
Akiuliza maswali na kutoa maelekezo wakati Ripoti
hiyo inawakilishwa na Mkuu wa Wilaya ya Misungwi, Bibi Mariam Lugaija
kwenye Shule ya Sekondari ya Misungwi, Rais Kikwete amewaambia viongozi
wa Wilaya hiyo na wa Mkoa wa Mwanza:
“Kazi muhimu na uhodari wa kiongozi unathibitishwa
na jinsi kiongozi huyo anavyopambana kupunguza umasikini wa wananchi
na anavyobuni mbinu za kuongeza mapato ya wale anaowaongoza.”
Ameongeza Rais Kikwete: “Kila kiongozi lazima awe
na uchungu wa maendeleo na tamaa ya kuleta mabadiliko kwa wananchi wao.
Kazi ya kiongozi ni kuhangaika na maendeleo ya wananchi.”
Akionyeshwa kutoridhishwa na kiwango cha uongozi
cha baadhi ya madiwani mkoani humo, Rais Kikwete amewaambia viongozi
hao: “Kazi ya madiwani haiwezi kuwa kupima na kugawa viwanja. Mliomba
kazi ya udiwani ili kuwatumia wananchi na kuwaletea maendeleo. Nyie
madiwani hamuwezi kuendelea kuwasibiri TASAF kuwaletea wananchi wenu
maendeleo. Hii ni kazi yenu.”
Ameongeza kuelekeza Rais Kikwete: “Kazi yenu haiwezi
kuwa ni kusubiri posho ya vikao na kupokea mishahara bure. Lazima muwe
na tamaa ya maendeleo ya wananchi wenu.”
Aidha, aliwakumbusha kuwa Serikali inatoa fedha nyingi
kwa halmashauri kwa ajili ya ujenzi wa barabara kwenye halmashauri hizo,
lakini madiwani wanashindwa ama kuchelewa kuzitumia fedha hizo kujenga
barabara hadi mwaka wa fedha unamalizika.
“Hili nalo halikubaliki. Kwa sababu Serikali inawapa
fedha nyingi, lakini nyie hamzitumii kwa wakati na fedha hizo zinarudishwa
kwenye Mfuko wa Barabara.”
No comments:
Post a Comment