
Katibu Mkuu wa Chadema Dr.Wilbrod Slaa akipokelewa na viongozi wa Chuo Kikuu cha Central piedmont

Mitambo
maalum inayotumika katika mafundisho ya viwandani. Hii ni kwa ajili ya
kuwafundisha wanafunzi wanaochukua kozi ya kuendesha mashine viwandani.

Katibu Mkuu wa Chadema Dr.Wilbrod Slaa akitizama kwa umakin jinsi mitambo hii ya kisasa inavyofanya kazi kati hiki chuo

Katibu Mkuu wa Chadema Dr.Wilbrod Slaa
akionyeshwa jinsi mitambo ya kisasa inayotumika katika mafunzo
inavyofanya kazi. Hii karakana ndiyo inayotumika kuwatayarisha vijana
kuwa wabunifu na kuweza kijiajiri

Katibu Mkuu wa Chadema Dr.Wilbrod Slaa akiwa kwenye maongezi na Rais wa Chuo cha Piedmont


Katibu Mkuu wa Chadema Dr.Wilbrod Slaa pamoja na viongzi wa juu wa Charlotte Chamber of commerce kwenye picha ya pamoja baada ya kufanya maongezi ya ushirikiano wa kibiashara.Picha Zote na Chadema
---
Leo asubuhi Katibu mkuu wa
Chama cha Demokrasia na Maendeleo Mh. Wilbrod Slaa Washington DC
kuelekea jimbo la North Carolina ambako amelakiwa na Rais wa Chuo cha
Piedmond Community College yenye jumla ya campuses 16. Na jumla ya
wanafunzi 85,000
Piedmont Community College ndio
moja ya Community colleges bora zaidi Marekani, na imekuwa
ikitayarisha wanafunzi mahiri kwenye eneo la engineering.
Lengo kubwa la kiongozi huyu
maarufu nchini kukutana na Rais wa Chuo, ni kujifunza siri ya mafanikio
ya chuo hicho, kwa ajili ya kuwawezesha wanafunzi wa kitanzania
kufanya vizuri zaidi kwa lengo kubwa la kutayarisha rasilimali watu.
Dr. Slaa pamoja na chama cha Chadema, wanaamini kwamba, ili kuliokoa
taifa, lazima elimu ipewe nafasi ya kwanza
Kadhalika, Dr. Slaa na Rais was
chuo kikuu cha Pedmont walikubaliana kuanzisha program maalum
itakayowawezesha vijana wa kitanzania na wakimarekani kuanzisha urafiki
utakaoziwezesha chuo hicho maarufu kufanya kazi kwa ukaribu na vyuo
vya kitanzania. Vyuo vya kitanzania vitanufaika zaidi hasa kutokana na
technologia ya kipekee ambayo hipo chuoni hapo.
Baada
ya miaka 52 ya ufisadi na kuuzwa kwa rasilimali za nchi, elimu duni,
umasikini wa kupindukia, huku taifa likiendelea kuwa omba omba Dr. Slaa
pamoja na Chama Cha Demokrasia na Maendeleo imeamua kutafuta njia
mbadala ya kuleta ukombozi karibu na wananchi. Chadema imeanza kutafuta
mbinu za kumkomboa mtanzania kutoka kwenye ufukara. Lengo la Chadema ni
kutengeneza mamilioni ya ajira ambazo makampuni mengi yako tayari
kuyazalisha kama Chadema itatengeneza mazingira mazuri ya wao kuwekeza.
Katibu Mkuu wa Chadema Dr.Wilbrod Slaa
amemaliza ziara ya siku moja carolina na kuondoka kuelekea Atlanta
georgia ambako atakutana na viongozi wa shirika la Coca-Cola, AT&T
pamoja UPS
No comments:
Post a Comment