ADV

ADV

ADVERTISEMENT CORNER

HUDUMA YA KUKATA TICKET ZA NDEGE ONLINE


SOMA HABARI

SOMA HABARI
Showing posts with label Dr. Wilbard Slaa. Show all posts
Showing posts with label Dr. Wilbard Slaa. Show all posts

Monday, October 7, 2013

Muendelezo wa Ziara ya Katibu Mkuu wa Chadema Dr Wilbrod Slaa Nchini Marekani Atembelea Chuo Kikuu Cha Tiba cha Alabama

 Katibu Mkuu wa Chadema Dr.Wilbrod  Slaa akiongozwa na Professor ambaye pia ni dean msaidizi
 Katibu Mkuu wa Chadema Dr.Wilbrod Slaa akielekezwa kwenye chumba cha Mikutano na rais wa chuo cha tiba
 Katibu Mkuu wa Chadema Dr.Wilbrod Slaa na Dean wakiwa kwenye maongezi ya kufanya kazi pamoja
Katibu Mkuu wa Chadema Dr.Wilbrod Slaa akipewa maelekezo na rais wa chuo cha Tiba
Katibu Mkuu wa Chadema Dr.Wilbrod Slaa pamoja na viongozi wa Chuo cha Tiba
---
Akiwa anaendelea na ziara yake nchini Marekani, siku ya ijumaa katibu mkuu wa chama cha demokrasia na maendeleo Chadema Dr. Wilibrod Slaa alitembelea Chuo kikuu cha tiba cha Alabama ambako alilakiwa na viongozi wa juu wa chuo hicho

Sunday, October 6, 2013

Katibu Mkuu wa Chadema Dr Wilbrod Slaa Apata Mapokezi ya Makubwa Kwenye Ufunguzi wa Mchezo wa Mpira Maarufu Kama American Football Nchini Marekani


 Msafara wa Katibu Mkuu wa Chadema  Dr. Wilbrod Slaa ukiwasili uwanjani
  Moja ya Viongozi wa Juu Nchini Marekani akisalimiana na Dr Slaa
 Mshindi wa Nobel Peace Price na Katibu Mkuu wa Chadema Dr. Slaa ndani ya Chumba cha watu mashuhuri wakijadili neno
 wakiwa katika chumba cha watu mashuhuri. Baadhi ya watu mahuhuri kama yeye hawakujizuia kwenda kumsalimia. Akifungua mchezo wa leo,Katibu Mkuu wa Chadema Dr. Slaa alirushwa moja kwa moja na moja ya luninga kubwa zaidi nchini marekani
Katibu Mkuu wa Chadema Dr. Slaa akibadilishana mawazo na baadhi ya viongozi ya Masenators walioalikwa kujumuika naye
 Viongozi Mashuhuri wakiwa uwanjani kabla ya mchezo kuanza. Katibu Mkuu wa Chadema Dr. Slaa ndiye mgeni Rasmi. Hapa ni chumba maalum cha rais kwa ajili ya wageni mashuhuri
Uwanja ukiwa umefurika wapenzi wa mpira takribani laki moja.Picha na Chadema
----
Ni mara ya kwanza kwa kiongozi wa kiafrika kupewa mapokezi makubwa ambayo Dr. Slaa ameyapokea katika ufunguzi wa mchezo wa mpira maarufu kama American football. Dr. Slaa alialikwa na Chancellor pamoja na Rais wa chuo kikuu cha Alabama kuwa mgeni rasmi katika mchezo huo baina ya Alabama na Georgia State. Kiongozi huyo wa Chadema alipokewa na viongozi wa ngazi mbali mbali wa kitaifa na wa jimbo la Alabama

Akimkaribisha Katibu Mkuu wa Chadema Dr. Slaa katika chakula cha asubuhi iliyoandaliwa kwa ajili yake, Chancellor wa chuo hicho, amemfananisha Dr. Slaa na Nelson Mandela kutokana na juhudi zake za kupambana ufisadi nchini Tanzania. “

Tunajua jinsi polisi wanavyowaua raia na kuwakamata wapinzani” alisema kiongozi huyo. Kadhalika kiongozi huyo amemsifu Dr. Slaa kutokana na msimamo wake, sera zake za kulikomboa Tanzania kutoka katika umasikini licha ya chama chake kutungiwa kesi za ughaidi.

Kwa upande wake, wakiwa kama moja ya vyuo vikuu nchini marekani, wako tayari kufanya kazi kwa ukaribu na Dr. Slaa hasa katika sekta ya elimu. Wamemuomba ajisikie nyumbani na kufurahia mchezo wa American football.

Kwa unyenyekevu Dr. Slaa aliwashukuru governor, na viongozi wengine kwa kuwa wakarimu sana kwake na mkewe na watu wa Tanzania. Amefurahishwa jinsi wamarekani wanavyokuwa na hamasa na kuipa kipaumbele michezo.

Nimejifunza kwamba michezo ni moja ya mbinu ya kuiunganisha taifa hasa tunapokuwa na changamoto nyingi kama za kwetu alisema Dr. Slaa. Kadhalika amesema kwamba, chama chake cha Chadema ina sera ya kukuza vipaji kupitia taasisi za michezo nchini Tanzania na siyo kuwaleta Makocha wa kigeni, mmoja baada ya mwingine na kuwapeleka Ikulu kula pilau na kupiga picha.

Nilichojifunza ni kwamba, lazima nirudi na ujumbe kwa watanzania kuweka mifumo endelevu ya michezo kuanzia shule za misingi hadi vyuoni. Nilichoona hapa ni mfano wa kuigwa alimalizia Katibu Mkuu wa Chadema Dr. Slaa

Friday, October 4, 2013

Katibu Mkuu wa Chadema Dr.Wilbrod Slaa Aendelea na Ziara Yake Ya Kikazi Nchini Marekani Ya Kutafuta Ufumbuzi Wa Tatizo La Kiuchumi,Makampuni Makubwa Nchini Marekani Yaahidi Maelfu ya Ajira


 Katibu Mkuu wa Chadema Dr.Wilbrod  Slaa akipokelewa na viongozi wa Chuo Kikuu cha Central piedmont
 Mitambo maalum inayotumika katika mafundisho ya viwandani. Hii ni kwa ajili ya kuwafundisha wanafunzi wanaochukua kozi ya kuendesha mashine viwandani.
 Katibu Mkuu wa Chadema Dr.Wilbrod  Slaa akitizama kwa umakin jinsi mitambo hii ya kisasa inavyofanya kazi kati hiki chuo

Friday, May 24, 2013

Dr. Slaa sasa anaweza kumuoa Josephine Mushumbusi baada ya kushinda rufani iliyotolewa na mumewe wa zamani

 
Mume wa zamani wa Mushumbusi
 

Katika taabu na raha, katika magonjwa na shida   umpende na kumheshimu siku zote za maisha yako

  Katibu Mkuu wa Chadema Dr Wilbrod Slaa akiwa na Josephine Mushumbusi
---
HATIMAYE Mahakama ya Wilaya ya Kinondoni, imetupilia mbali rufaa iliyokuwa imekatwa na aliyekuwa mume wa Josephine Mushumbusi( KWA  SASA  NI  MCHUMBA WA DR. SLAA) , Maimbo baada ya kuiona rufaa hiyo haina msingi wowote kisheria.
 
Hukumu hiyo ya rufaa ya  madai ya ndoa Na.32/2012 ilitolewa leo na Hakimu Aniseth Wambura ambapo alisema mahakama yake imefikia uamuzi huo wa kuitupa rufaa hiyo kwasababu haina mantiki ya kisheria.
 
Hakimu Wambura alisema mahakama yake imekubalina na hukumu iliyotolewa Aprili 2012 na Mahakama ya Mwanzo Sinza katika kesi ya madai talaka iliyokuwa imefunguliwa na Mushumbusi anayetetewa na wakili wa kujitegemea Philemon Mutakyamilwa  dhidi ya Maimbo ambapo mahakama hiyo ya chini ilitangaza kuwa hakukuwa na ndoa baina ya watu hao kwasababu Maimbo alikuwa ni mzinzi, simwaminifu katika ndoa yake na alikuwa akimtesa mkewe.
 
“Baada ya mahakama yangu kusikiliza hoja za mwomba rufaa na mjibu rufaa ,mahakama hii imefikia uamuzi wa kukubali hoja za Mushumbisi kuwa kwa tabia ile ya mbaya ya uzinzi na ukosefu wa uaminifu katika ndoa yake hapakuwepo na ndoa baina yao hivyo mahakama inatangaza kuwa hukumu ya mahakama ya Mwanzo Sinza ambayo iliivunja ndoa hiyo ilikuwa hukumu sahihi “alisema hakimu Wambura.
 
Akizungumza na mwandishi wa habari hizi baada ya kutolewa kwa hukumu hiyo wakili Mutakyamilwa alisema amefurahishwa na hukumu hiyo kwani mahakama imetenda haki  kwasababu kesi hiyo ya madai ya talaka ilikuwa na msukumo wa siasa chafu zilizokuwa na lengo chafu la kumchafulia jina mteja wake(Mshumbusi) ambaye kwa sasa ni mzazi mwenzie Katibu Mkuu wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Dk.Wilbroad Slaa.
 
KWA  HIYO, KWA  SASA  DR. SLAA   NA  MPENZI  WAKE  W ANAWEZA  KUOANA..!!!
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...