

Ankara Uturuki, Sultan Kosen, raia wa Uturuki mwenye urefu wa futi nane na mwenye rekodi ya Guiness ya kuwa mtu mrefu kuliko wote duniani, amefunga ndoa na mwanamke wa Syria mwenye urefu wa meter 1.75. "Siwezi kuelezea furaha niliyokuwa nayo leo" alisema Sultan mwenye umri wa miaka 31 wakati akisherehekea harusi yake na Mervi Dibo mwenye umri wa miaka 20.
Harusi yao ilifanyika jumapili iliyopita huko Syria.Suti ya bwana harusi ilishonwa kwa kutumia kitambaa cheusi chenye ukubwa mwa meter 6.
No comments:
Post a Comment