Baadahi
ya watalii kutoka Israel wakifanyiwa ukaguzi katika uwanja wa ndege wa
Kilimanjaro (KIA) kabla ya kupanda ndege kurejea kwao Isreal.

Na Geofrey Tengeneza
Kundi
la watalii 150 kutoka Israel limemaliza ziara yake ya siku hapa nchini
na kuondoka kurejea nyumbani kupitia uwanja wa ndege wa Kilimanjaro
baada ya ziara yao waliyoilezea kuwa ni ya mafaniko makubwa.
Waisrael
hao walifika nchini kwa ndege maalumu ya watalii ya shirika la ndege la
Israel (ELAL) ambayo ilizianza rasmi safari zake za moja kwa moja
kutoka Tel Avivi Israel kuja KIA Tanzania tarehe 29/11/2013. Miongoni
mwa watalii hao walikuwemo watu kumi (10) wenye ulemavu wa aina
mbalimbali, na wandishi wa habari saba (7) kutoka vyombo mbalimbali vya
habari vya Israel yakiwemo magazeti maarufu, kituo cha televisheni cha
channel 10 ambacho ndiyo kikubwa nchini Israel na kituo cha televisheni
cha channel 2. Watalii ishirini na wanne (24) kati ya hao 150 wakiwemo
walemavu wote kumi, walikuja mahsusi kwa jili ya kupanda mlima
Kilimanjaro huku wapiga picha wa televisheni ya channel 10 wakipiga
picha tukio hilo la aina yake. Walemavu hao kumi walifanikiwa kupanda
mlima Kilimanjaro hadi katika kituo cha Gilman. Watalii wengine
waliosalia 126 walitembelea Hifadhi ya Taifa ya Manyara, Hifadhi ya
Taifa Serengeti, Kreta ya Ngorongoro na baadae visiwa vya Zanzibar.
Akizungumza
na wandishi wa habari katika uwanja wa ndege wa Kilimanjaro (KIA,
Mkurugenzi wa Kampuni ya utalii ya Safari Company ya nchini Israel
iliyoratibu safari hiyo Bibi Ronit Hershkovitz amesema ziara hiyo pamoja
na hatua ya shirika la ndege la Israel kuanzisha safari za moja kwa
moja kuja KIA kutafungua milango ya Tanzania kuanza kupokea idadi kubwa
ya watalii kutoka Israel. Amesema ziara hiyo imekuwa ya kihistoria
kwani wamefurahishwa sana na upekee wa vivutio vya utalii vilivyopo
hapa nchini “ndugu zangu wa Israel wamefurahia sana na kushangazwa na
uzuri wa vivutio vya kitalii vya Tanzania. Kwa mfano makundi ya simba
kule Serengeti, wanyama maarufu watano (the big five) na mlima
Kilimanjaro vimewasisimua sana” alisema bibi Hershkovitz.
Naye
Meneja Bodi ya Utalii Tanzania (TTB) mkoani Arusha Bw. Willy Lyimo
aliwashukuru watalii hao toka Israel kwa kuja kutembelea vivutio vya
Tanzania na akawataka wakawe mabalozi wema wa Tanzania nchini kwao. “
Mmejionea kwa macho yenu na kukiri uzuri wa vivutio vyetu, tunaomba
mkawaambie ndugu zetu waisrael kuwa tunawakaribisha sana, na tunapenda
kuwahikishia kuwa Tanzania ni nchi salama kabisa na yenye amani tele”
alisema Bw. Lyimo.
Safari
maalumu za watalii (charter flights) za shirika la ndege la Israel
zitafanyika kila juma ya mwezi April, Mei, Julai, Agosti, Septemba na
Desemba, hii ikimaanisha kuwa kutakuwa na safari nne kila mwezi
uliotajwa hapo.
No comments:
Post a Comment