
Nelson Mandela Rais wa ANC1962, kabla ya kifungo.
Mwaka
1962 Nelson Mandela kwa siri na bila ruhusa aliondoka nchini Afrika
Kusini na kutumia miezi saba akisafiri katika nchi mbalimbali barani
Afrika.
Chama
cha African National Congress, ambacho kilipigwa marufuku na serikali
ya ubaguzi wa rangi nchini humo, kilikuwa ndio tu kimeanzisha tawi lake
la kijeshi lililojulikana kwa jina la Umkhonto we Sizwe.
Ziara
hiyo ya Mandela ilikuwa ni kupata kuungwa mkono kisiasa na kifedha
kutoka nchi za bara la Afrika, na kutafuta nchi ambazo zitakuwa tayari
kutoa mafunzo kwa wapiganaji wake wanaojiunga na jeshi hilo, ikiwa ni
pamoja na yeye mwenyewe. Alipata mafunzo ya kijeshi nchini Morocco
kutoka kwa askari wa Algeria, waliokuwa wakitumia ardhi ya Morocco kama
kituo cha kupambana na utawala wa kikoloni wa Ufaransa.
Na
mafunzo mengi yalifanyika nchini Ethiopia. Fekadu Wakene ni kanali
mstaafu wa jeshi nchini Ethiopia ambaye alipewa jukumu la kutoa mafunzo
ya mbinu za kivita kwa Nelson Mandela.
Kanali Wakene anasema wakati huo hawakujua namna alivyofika hapo na sababu ya kuja kwake.
"Lakini
tulipata maelekezo kutoka kwa viongozi wetu. Mkuu wangu wa kazi alikuwa
Jenerali Tadesse Birru. Aliniita na kunitambulisha kwa mgeni na
nilimpatia mafunzo.
Tulifanya
mafunzo katika mambo mbalimbali kama vile kuhujumu miundo mbinu na
kutega milipuko. Namna ya kushambulia na namna ya kujificha au kuendesha
mambo chini kwa chini. Na namna ya kuteketeza kundi la adui.
Tulikuwa tukifanya mafunzo ya nadharia mchana na usiku tulifanya mazoezi kwa vitendo."
Kanali
huyo, anamwelezea Mandela kuwa alikuwa mwanafunzi imara sana na
msikivu. Alifuata mafunzo vizuri na alikuwa ni mtu mwenye mvuto wa
kupendwa. Huwezi kujizuia, bali kumpenda.
Anasema nje ya kazi alikuwa mwenye furaha, mtu mcheshi na wakati wa kazi alizingatia kile alichokuwa akikifanya kwa wakati huo.
Mandela alikuwa jasiri na msikivu.
"Kimwili
alikuwa mtu mwenye nguvu sana na aliyejengeka. Lakini, wakati mwingine
wa mafunzo, alikuwa mbele ya kile kilichofundishwa. Japokuwa nia yake
ilikuwa nzuri lakini kilichokuwa kikifanyika kilikuwa cha hatari. Wakati
mwingine tulimzuia kidogo kwa sababu za kiusalama.
Kanali Wakene anasema hawakufahamu mpaka baadaye kabisa waliposikia kuhusu Rais Nelson Mandela na habari yake.
"Nakumbuka
kusikia kuhusu kuachiliwa kwake kutoka gerezani. Wakati huo ulikuwa wa
furaha kubwa. Kila mahali mjini Addis, kila mtu alishangazwa na kufurahi
habari zilipoeenea za kuachiliwa kwake."
Kwa
upande mwingine kiongozi mpigania uhuru katika nchi jirani ya Zimbabwe,
Rais Robert Mugabe naye anaeleza jinsi alivyomfahamu Nelson Mandela.
Rais
Robert Mugabe wa Zimbabwe amemwelezea marehemu Nelson Mandela kama
kinara wa wanyonge na dhamira yake ya ukombozi itaendelea kuenziwa
nchini Zimbabwe.
Katika
ujumbe wake wa rambirambi kufuatia kifo cha rais wa kwanza mweusi wa
Afrika Kusini aliyechaguliwa kwa njia ya kidemokrasia, rais huyo wa
Zimbabwe amemwelezea Mandela kama mpigania haki.
Mandela
amefariki dunia akiwa na umri wa miaka 95 nyumbani kwake mjini
Johannesburg baada ya kuugua kwa muda mrefu akisumbuliwa na maambuzi
katika mapafu na atazikwa tarehe 15 Desemba 2013.
Rais
Mugabe jana alimtumia rambirambi rais Jacob Zuma akisema, "kwa niaba ya
serikali na wananchi wa Jamhuri ya Zimbabwe na chama tawala cha Zanu-PF
na mimi mwenyewe, ningependa kuelezea masikitiko makubwa kutokana na
kifo cha mhimili mkuu wa ukombozi wa Afrika, mpigania uhuru na rais wa
kwanza wa Afrika Kusini huru na ya kidemokrasia, Bwana Nelson Rolihlahla
Mandela kilichotokea Desemba 5,2013.
Maisha
ya kisiasa ya Bwana Nelson Mandela, ni kielelezo cha kutukuta na
kitabakia kuwa nguzo ya uadilifu. Sio tu alikuwa kinara wa harakati za
ukombozi wa mtu mnyonge bali pia alikuwa mnyenyekevu na kiongozi ambaye
hakuonyesha ubinafsi katika kuwatumikia watu wake. Bwana Mugabe anasema
wanaungana na taifa zima kuomboleza kifo cha Bwana Mandela.
Marehemu Nelson Mandela daima atabakia katika akili zetu kuwa mpigania haki.
No comments:
Post a Comment