ADV

ADV

ADVERTISEMENT CORNER

HUDUMA YA KUKATA TICKET ZA NDEGE ONLINE


SOMA HABARI

SOMA HABARI

Tuesday, December 3, 2013

Netanyahu ampa Papa Francis zawadi ya kitabu cha kumbukumbu ya mataso ya Wayahudi waliyofanyiwa na Wakatoliki wa Spain karne ya 15



 Israeli Prime Minister Benjamin Netanyahu meets with Pope Francis

Papa Francis akipokea kitabu alichopewa kama zawadi na Waziri mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu katika Baktaba ya Papa huko Vatican jana


Jana Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu ametembelea Papa Francis katika Makao yake huko Vatikan. Kwa mujibu wa shirika la utangazaji la DPA Netanyahu alimletea Papa Francis zawadi mbalimbali lakini zawadi iliyozua maswali mengi ni kitabu  kinachohusu uteswaji wa Wajahudi huko Uhispania kiitwacho "The Origins of the Inquisition in Fifteenth-Century Spain,"
Kitabu hiki kiliandikwa na baba yake Netanyahu miaka ya nyuma na kinaelezea jinsi Wahispania walivyowatesa, kuwachoma moto na kuwasulubisha Wayahuni ambao walikataa kuingia katika Ukristo (ukatoliki) Kitabu hiki kinaeleza bayana mateso hayo na na kueleza jinsi Wayahudi wengine walivyoamua kuwa Wakatoliki lakini wakawa wanashika dini yao ya Kiyahudi kwa siri. Mates ohayo yaliendelea hadi Papa Innocent wa IV alipopiga marufuku juu ya mates ohayo.
Baba mzazi wa Netanyahu, mzee ben-Sayuni Netanyahu aliyefariki mwaka jana tu akiwa na miaka 102 alikuwa akifundisha katika chuo kikuu ya Kiebrania na chuo kikuu cha Cornell.
Mzee huyu ingawa anatofautiana kisiasa na mwanae lakini ndiye aliyemtengeneza mwanae katika siasa zake kali.Hivyo, zawadi ya Netanyahu kwa Papa Francis inaweza kuonekana watazamaji kama ni hasira ya kimya kimya au ni ukumbusho tu wa maovu yaliyofanywa na kanisa hilo miaka ya nyuma kwa Wayahudi.
Hiki ni kitabu ambacho Waziri mkuu Netanyahu anakipa uzito wa hali ya juu si tu kwa kuwa kimeandikwa na baba yake bali pia kinaeleza ukweli kuhusu Wayahudi walivyoendelea kuiheshimu dini yao kwa siri. Kitabu hiki kinaeleza ukweli k uwa Wayahudi waliteswa si kwa sababu ya dini yao bali hasa kwa sababu ya ubaguzi wa rangi na wivu kutokana na maendeleo waliyokuwa nayo. Hili linajidhihirisha mamia ya miaka baadaye huko wakati wa mauaji yajulikanayo kama Hlocaust.
Netanyahu amempa Papa Benedict sanamu ya Mtume Paul. Mtume Paul ana nafasi kubwa sana katika mahusiano ya dini hizi mbili za zamani (Judaism &Catholicism) kwa kuwa yeye ni kiungo muhimu sana. Mtume Paul alikuwa Myahudi aliyehakikisha mafundisho ya dini ya kiyahudi yanafuatwa na aliongoka na kuingia Ukatokilikakiwa katika harakati za kuwatesa wakristo wakati huo.



carved oak  period oak   16th century  
Sanamu ya Mtakatifu Paul

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...