Papa Francis akipokea kitabu alichopewa kama zawadi na Waziri mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu katika Baktaba ya Papa huko Vatican jana
Jana Waziri Mkuu
wa Israel Benjamin Netanyahu ametembelea Papa Francis katika Makao yake huko
Vatikan. Kwa mujibu wa shirika la utangazaji la DPA Netanyahu alimletea Papa
Francis zawadi mbalimbali lakini zawadi iliyozua maswali mengi ni kitabu kinachohusu uteswaji wa Wajahudi huko Uhispania
kiitwacho "The Origins of the Inquisition in
Fifteenth-Century Spain,"
Kitabu hiki kiliandikwa na baba yake
Netanyahu miaka ya nyuma na kinaelezea jinsi Wahispania walivyowatesa,
kuwachoma moto na kuwasulubisha Wayahuni ambao walikataa kuingia katika Ukristo
(ukatoliki) Kitabu hiki kinaeleza bayana mateso hayo na na kueleza jinsi
Wayahudi wengine walivyoamua kuwa Wakatoliki lakini wakawa wanashika dini yao
ya Kiyahudi kwa siri. Mates ohayo yaliendelea hadi Papa Innocent wa IV
alipopiga marufuku juu ya mates ohayo.
Baba mzazi wa Netanyahu, mzee
ben-Sayuni Netanyahu aliyefariki mwaka jana tu akiwa na miaka 102 alikuwa
akifundisha katika chuo kikuu ya Kiebrania na chuo kikuu cha Cornell.
Mzee huyu
ingawa anatofautiana kisiasa na mwanae lakini ndiye aliyemtengeneza mwanae
katika siasa zake kali.Hivyo, zawadi ya Netanyahu kwa Papa Francis inaweza kuonekana watazamaji kama ni
hasira ya kimya kimya au ni ukumbusho tu wa maovu yaliyofanywa na kanisa hilo
miaka ya nyuma kwa Wayahudi.
Hiki ni kitabu ambacho
Waziri mkuu Netanyahu anakipa uzito wa hali ya juu si tu kwa kuwa kimeandikwa
na baba yake bali pia kinaeleza ukweli kuhusu Wayahudi walivyoendelea
kuiheshimu dini yao kwa siri. Kitabu hiki kinaeleza ukweli k uwa Wayahudi
waliteswa si kwa sababu ya dini yao bali hasa kwa sababu ya ubaguzi wa rangi na
wivu kutokana na maendeleo waliyokuwa nayo. Hili linajidhihirisha mamia ya
miaka baadaye huko wakati wa mauaji yajulikanayo kama Hlocaust.
Netanyahu amempa Papa
Benedict sanamu ya Mtume Paul. Mtume Paul ana nafasi kubwa sana katika
mahusiano ya dini hizi mbili za zamani (Judaism &Catholicism) kwa kuwa yeye
ni kiungo muhimu sana. Mtume Paul alikuwa Myahudi aliyehakikisha mafundisho ya
dini ya kiyahudi yanafuatwa na aliongoka na kuingia Ukatokilikakiwa katika
harakati za kuwatesa wakristo wakati huo.

Sanamu ya Mtakatifu Paul