
Mkurugenzi
wa Masoko wa Kampuni ya Bia ya Serengeti (SBL), Ephraim Mafuru (wa pili
kulia) akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam.
Pamoja naye ni Meneja Masoko wa SBL, Allan Chonjo (wa pili kushoto).

Mkurugenzi
wa Masoko wa Kampuni ya Bia ya Serengeti (SBL), Ephraim Mafuru (wa
kwanza kulia) akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es
Salaam. Pamoja naye ni Meneja Masoko wa SBL, Allan Chonjo (kushoto).

Meneja
Masoko wa Kampuni ya Bia ya Serengeti (SBL), Allan Chonjo (wa pili
kushoto) akizungumza na wanahabari leo jijini Dar es Salaam. Pamoja naye
ni Mkurugenzi wa Masoko wa SBL, Ephraim Mafuru (wa pili kulia)

Mkurugenzi
wa Masoko wa Kampuni ya Bia ya Serengeti (SBL), Ephraim Mafuru (wa
kwanza kulia) akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es
Salaam.

Meneja
Masoko wa Kampuni ya Bia ya Serengeti (SBL), Allan Chonjo (wa pili
kushoto) akizungumza na wanahabari leo jijini Dar es Salaam. Pamoja naye
ni Mkurugenzi wa Masoko wa SBL, Ephraim Mafuru (wa pili kulia)

Meneja
Masoko wa Kampuni ya Bia ya Serengeti (SBL), Allan Chonjo (wa pili
kushoto) akionesha kizibo cha bia ambacho ndani yake kutakuwa na zawadi
au namba zitakazotumwa na mteja kwa wanahabari leo jijini Dar es Salaam.
Pamoja naye ni Mkurugenzi wa Masoko wa SBL, Ephraim Mafuru (wa pili
kulia)


Shamrashamra ya Uzinduzi wa promosheni ya Shinda safari kwenda nchini Brazil,kupitia pia ya Serengeti

Shamrashamra ya Uzinduzi wa promosheni ya Shinda safari kwenda nchini Brazil,kupitia pia ya Serengeti

Baadhi
ya mabalozi wa Bia ya Serengeti wakionesha shoo kwa wananchi baada ya
uzinduzi wa Shinda safari kwenda nchini Brazil,kupitia pia ya Serengeti

Baadhi
ya wafanyakazi wa SBL na wananchi wakishuhudia Uzinduzi wa promosheni
ya shinda safari kwenda nchini Brazil,kupitia pia ya Serengeti
uliofanyika leo.

Uzinduzi wa promosheni ya shinda safari kwenda nchini Brazil,kupitia pia ya Serengeti uliofanyika leo.
Na Thehabari.com
*Zaidi ya milioni 700 Kushindaniwa Kupitia Bia ya Serengeti
KATIKA
mpango mwingine wa kutambua thamani ya wateja, Kampuni ya Bia ya
Serengeti (SBL) leo imezindua kampeni ya kufaidisha wateja ambapo baadhi
ya wateja watashinda safari iliyolipiwa kwenda nchini Brazil, hii ikiwa
ni moja kati ya zawadi nyingi nyingine zitakazoshindaniwa. Kampeni hii
imeanza tayari na itaendelea kwa muda wa kipindi cha miezi mitatu wateja
kujishindia.
Akizungumza leo jijini Dar es Salaam na wanahabari, Mkurugenzi wa Masoko wa SBL, Ephraim Mafuru alisema wateja wanaweza kushiriki mara nyingi watakavyoweza huku kukiwa na zawadi za fedha shs milioni 100 zitakazotolewa kwa wateja watakaoshinda. Alisema mteja anaweza kujishindia kuanzia kiasi cha shs 5,000 hadi shs 10,000 na bia ya bure ambayo mtu atashinda papo hapo. Akifafanua zaidi alisema mtumiaji atakapofungua bia ya Serengeti, chini ya kizibo atakuta namba ambazo atazituma kwenda namba 15317 na papo hapo zawadi itaonyeswa kwenye ujumbe mfupi atakaopokea. “…Kampeni hii kama kampeni za hapo awali, itakuwa inasimamiwa na Bodi ya Michezo ya Kubahatisha Tanzania. Washirika wengine ambao watakuwa wanahakiki uaminifu wa zoezi zima ni PWC na Push mobile,” alisema Mafuru. Uzinduzi huo uliofanyika katika kiwanda cha Bia cha Serengeti Dar es Salaam leo asubuhi, Mkurugenzi wa Masoko, Mafuru pia aliongeza kuwa promosheni hiyo si tu kwa ajili ya kuongeza mauzo ya bidhaa yao lakini bali kuwatunuku wateja kwa kupendelea bidhaa za SBL. “Katika shughuli zetu zote, tunapenda kuwa karibu sana na jamii inayotuzunguka. Tunajaribu kuangalia kwa makini na kujua mahitaji yao. Ingawa hatuwezi kushughulikia mahitaji yote wanayohitaji, tunahakikisha chochote tunachofanya kinagusa maisha ya wateja wetu. Tunashiriki katika shughuli mbalimbali ambazo zitaboresha maisha ya kila raia. Kuanzia mipango ya kijamii mpaka shughuli zinazohusu bidhaa zetu, kama hii iliyotuleta hapa leo,” alisema Mafuru. Aidha, SBL imeanzisha promosheni mapema katika mwaka 2014 kwa kuwa kuna shughuli nyingi zimepangwa mbeleni mwaka huu zote zikilenga kuwashukuru na kuwaonesha dhamana wateja wake. Aliongeza kuwa watumiaji wa bia ya Serengeti wamecheza nafasi kubwa sana katika ukuaji wa bidhaa hiyo ambao ni wa kasi. Pia ilijizolea tuzo za DLG za ubora wa bidhaa mara tatu na imekuwa moja kati ya bia zinazokubalika zaidi nchini kwa ubora.
“Tunashuhudia
promosheni nyingi kwenye soko letu, na zote zikiwa na nia ya kuongeza
mauzo bila kujali nini kinashindaniwa. Hiyo ni tofauti kwa kampuni ya
bia ya Serengeti, kwetu sisi zawadi ni ile itakayogusa na kubadili
maisha ya mshindi kwa mtazamo chanya. Zawadi yetu kubwa itakuwa safari
ya Brazil ambayo washindi wetu watapata uzoefu wa kusafiri daraja la
kwanza na kukaa Brazil huku gharama zote zikilipiwa, kwa washindi wetu
itakuwa ni safari isiyosahaulika “. Aliongeza Bw. Mafuru.
Naye, Meneja Masoko wa
Kampuni ya Bia ya Serengeti, Allan Chonjo akifafanua zaidi alisema kwa
sasa SBL imejipanga na wateja hawata pata kikwazo chochote katika kupata
zawadi zao. “…Nirahisi tu we nunua chupa ya bia ya Serengeti, angalia
chini ya kizibo, ukipata picha ya bia ina maana unapata bia ya bure na
unaichukua papo hapo. Ukipata tarakimu 6 za kipekee, unazituma kupitia
ujumbe mfupi wa tarakimu hizo kwenda nambari 15317 na utapata ujumbe
papo hapo wenye majibu yafuatayo: kwamba umeshinda, umekuwa mshindi wa
fedha taslimu kati ya shs 5,000 na shs 10,000 , ambayo mteja atatumiwa
kupitia M-Pesa au atapata ujumbe mfupi kushukuru kwa kushiriki na
kutamtaka kuendelea kushiriki,” alisema Chonjo.
Aidha
alisema kwa mteja kushiriki tu atakuwa ameingia kwenye droo ambayo
unaweza kujishindia safari ya brazil, king’amuzi cha Azam na Ipad. Hata
hivyo gharama za kutuma ujumbe mfupi katika shindano hilo ni sawa na
gharama ya kutuma ujumbe wa kawaida na unaweza kushiriki kupitia mtandao
wowote. Safari ya Brazil itakuwa kati ya mwezi wa sita na saba mwaka
2014. Kwa maelezo zaidi fuatilia ukurasa wa kijamii wa facebook wa bia
ya Serengeti.
Kunywa kwa tahadhari. Inauzwa kwa wenye miaka 18+, Kampuni ya bia ya Serengeti ni kampuni tanzu ya kampuni ya EABL/ DIAGEO.Kwa maelezo zaidi wasiliana na Mkurugenzi wa Mawasiliano na Mahusiano, Evans Mlewa evans.mlewa@diageo.com; Simu +255 784 990440 au tembelea tovuti ya DrinkQ.com
No comments:
Post a Comment