TAARIFA YA
MHE. BERNARD K. MEMBE (MB.), WAZIRI WA MAMBO YA NJE NA USHIRIKIANO WA KIMATAIFA
ATAKAYOITOA KWENYE MKUTANO NA WAANDISHI WA HABARI UTAKAOFANYIKA IDARA YA HABARI
(MAELEZO) TAREHE 20 FEBRUARI, 2014.
1.
KUCHAGULIWA TENA KWA TANZANIA KWENYE BARAZA LA AMANI NA USALAMA LA UMOJA WA
AFRIKA (AU)
Tanzania
imechaguliwa kwa mara ya pili mfululizo kuwa Mjumbe wa Baraza la Amani na
Usalama la Umoja wa Afrika (PSC) kwa kipindi cha miaka miwili kuanzia mwaka huu.
Tanzania ilichaguliwa kwa mara ya kwanza katika Baraza hilo mwaka 2012.
Miongoni mwa sababu muhimu zilizopelekea Tanzania kuchaguliwa kwa mara
nyingine kwenye Baraza la Amani na Usalama la Umoja wa Afrika ni pamoja na:-
a. Heshima
iliyojijengea kimataifa, hususan katika utatuzi wa migogoro ya kikanda kama ile
ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) na Madagascar;
b. Tanzania
imekuwa mstari wa mbele kuchangia vikosi vya kulinda amani kwenye maeneo
mbalimbali yenye migogoro kama vile Darfur, DRC, Lebanon n.k;
c. Kuaminika
kwa vikosi vya Tanzania vinapopelekwa kulinda amani kwa sababu ya ujuzi,
nidhamu na kujituma.
TANZANIA
YAJIJENGEA HESHIMA
Mbali na
kupata fursa adimu ya kushughulikia moja kwa moja masuala nyeti ya amani na
usalama Barani Afrika, uanachama wa Baraza la Amani utaijengea Tanzania heshima
kubwa hapa Barani na Kimataifa.
2. VIKOSI
VYA KULINDA AMANI KUTOKA TANZANIA
Tanzania imekuwa mstrari wa mbele katika masuala
mbalimbali yanayohusu harakati za ukombozi duniani. Tanzania imekuwa pia mstari
wa mbele kuchangia vikosi vya kulinda amani kwenye maeneo mbalimbali yenye
migogoro Barani Afrika na kwingineko. Hadi sasa Tanzania ina vikosi vya askari
huko Lebanon na askari huko Darfur, Sudan. Aidha, Tanzania ilishiriki
kikamilifu katika kufikia uamuzi wa kutuma Kikosi cha Kulinda Amani cha SADC
nchini DRC.
Tanzania
ilikuwa ni nchi ya kwanza kujitolea kutoa Kikosi Kimoja cha Wanajeshi (Force
Intervention
Brigade-FIB) huko Mashariki mwa DRC. Wanajeshi kutoka Tanzania ni takriban
1,283 kati ya Wanajeshi 3,069 kutoka Afrika Kusini na Malawi. FIB kwa
kushirikiana na vikosi kutoka Afrika Kusini, Majeshi ya Serikali ya DRC na
Vikosi vya MONUSCO mwezi Desemba 2014 walifanikiwa kukisambaratisha Kikosi cha
Waasi cha M23 na kuwezesha amani Mashariki mwa Kongo kurejea tena.
3. MGOGORO
WA TANZANIA NA MALAWI KUHUSU MPAKA KWENYE ZIWA NYASA
Mgororo huu kwa sasa uko chini ya usuluhishi wa Mhe. Joachim Chissano,
Mwenyekiti wa Jopo la Usuluhishi wa Jukwaa la Viongozi Wastaafu wa Afrika
Ukanda wa SADC.
Mnamo tarehe
27 Novemba, 2013 Tanzania na Malawi ziliwasilisha utetezi wa hoja zao kwa
Mwenyekiti wa Jopo la Usuluhishi ilikuliwezesha Jopo hilo kutafakari hoja za
pande zote mbili na kutoa uamuzi/ushauri wake kuhusu mgogoro huo.
Kwasasa
Tanzania na Malawi zinasubiri kuitwa na Jopo hilo ili kwenda kupokea
ushauri/uamuzi wa jopo hilo kuhusu mgogoro huo.
Tanzania
inapenda kuiomba Malawi kuendelea kutoa ushirikiano hadi hapo suala hili
litakapopatiwa ufumbuzi wa kudumu.
4. MGOGORO
WA SUDAN KUSINI
Sudani
Kusini ilikumbwa na mapigano mkubwa katikati ya Mwezi Desemba 2013 kati ya
vikosi vya serikali na waasi, ambao wanamuunga Makamu wa Rais wa zamani Bw.
Riek Machar. Mapigano hayo yalizuka baada ya Rais Kiir kumtuhumu Bw. Machar
kufanya Jaribio la kupindua Serikali.
Mapigano
hayo yalichukua sura ya ukabila kati ya kabila la Dinka analotoka Rais Kiir na
kabila la Nuer ambalo Bw. Machar anatoka. Hadi sasa zaidi ya watu 1000 wameuawa
na 700,000 kulazimika kukimbia makazi yao. Umoja wa Afrika kwa kushirikiana na
IGAD iliingilia kati na kuanzisha mazungumzo baina ya pande hizo mbilli.
Kufuatia
mazungumzo hayo, tarehe 2013 Januari 2014 pande hizo mbili zilisaini Mkataba wa
Kusitisha Mapigano mjini Addis Ababa, baada ya Serikali kukubali kuachia
wafuasi 7 kati ya 11 wa Bw. Machar, ambao Serikali ilikuwa ikiwashikilia kwa
tuhuma za kupanga Mapinduzi.
Duru ya Pili ya mazungumzo kati ya pande hizo ilianza tarehe 10
Februari, 2014 kwa lengo la kutafuta suluhu ya kudumu ya mgogoro huo. Upande wa
waasi bado unasisitiza kuachiliwa kwa wafuasi 4 waliobaki. Aidha, Waasi
wanataka majeshi yote ya nje yaliomo nchini humo kuondoka mara moja.
Wakati
mazungumzo hayo yakiendelea, kulikuwepo na taarifa za mapigano ya kushitukiza
baina ya Vikosi vya Serikali na Vikundi vya waasi kwenye baadhi ya maeneo ya
nchi hiyo. Tarehe 18 Mwezi huu, mapigano mapya yameibuka katika jimbo la Upper
Nile ambapo pande zote zinashutumiana kuvunja makubaliano ya kisitisha
mapigano.
Kwa upande
wake Vikosi vya Umoja wa Mataiifa (UNMISS), ambavyo mwezi Desemba 2013 idadi
yake iliongeka kutoka 7000 hadi 12,500 vimeendelea na jitihada za kuimarisha
amani. Tunaomba kuchukua fursa hii, kutaarifu kuwa Tanzania imeahidi kuchangia
vikosi vyake kujiunga na jeshi hili la Umoja wa Mataifa lililoko Sudani Kusini.
Pamoja na kuchangia vikosi hivyo Tanzania inaomba pande zinazopigana kusitisha
mapigano na kuendelea na mazungumzo ili kupata suluhu ya kudumu ya Mgogoro huo.
5. UHUSIANO
WA TANZANIA NA RWANDA
Kama
itakavyokumbukwa vyombo vingi vya habari viliripoti kudorora kwa uhusiano kati
ya Tanzania na Rwanda. Baada ya mazingumzo kati ya Rais Kikwete na Rais Kagame
yaliofanyika Mjini Kampala mwezi Septemba, 2013 hali ya uhusiano wetu
iliboreka.
Hata hivyo
hivi karibuni vyombo ya habari vya Rwanda lilikiwemo Gazeti la Serikali la
“News of Rwanda” Vimetoa taarifa za kuishutumu Tanzania na viongozi wake. Aidha
kumekuwepo na taarifa za kuishutumu Tanzania kufanya mazungumzo na viongozi wa
upinzani nchini Rwanda akiwemo ambapo Waziri Mkuu wa zamani wa Rwanda, Bw
Faustine Twagiramungu.
Serikali ilijibu shutuma hizo kwa kueleza kuwa Tanzania haisaidii
vikundi vyovyote vya waasi na pia haijawahi kufanya mazungumzo wala
kuwakaribisha viongozi wa Upinzani wa Rwanda.
Historia ya
Nchi yetu tangu uhuru inajulikana kuwa tumekuwa tukisisitiza Amani Barani
Afrika na hivyo hatuna sababu yoyote wa kusaidia waasi ili kuchochea migogoni.
Hivyo, tunaomba kuchukua nafasi hii kuwaonya wale wote wanaotaka kuchafua sifa
nzuri ya Tanzania kuacha mara moja.
Aidha
tunawaomba wanahabari kutoshabikia taarifa hizi za uzushi.
Tanzania siku
zote inataka uhusiano mzuri na jirani zake lakini tusingependa kupenda Amani
kwetu kuwe ndiyo sababu ya watu kutaka kutuchafua.
6. URAIA WA
NCHI MBILI (DUAL CITIZENSHIP) UTAMBULIWE NA KATIBA MPYA
Kama mnavyofahamu, Bunge Maalum la Katiba
limeanza vikao vyake Mjini Dodoma tarehe 18 Februari 2014. Wizara iliratibu
ushiriki wa Wanadiaspora katika Bunge hilo ili sauti na maoni yao yaweze
kujumuishwa katika Katiba Mpya.
Jitihada
hizo zimemwezesha mmoja wa Wanadiaspora, Bw. Kadiri Singo kuteuliwan na Mhe.
Rais Kikwete, ili kuweza kushiriki kikamilifu. Bw. Singo ameshawasili nchini na
kusajiliwa, tayari kushiriki katika Bunge hilo la Katiba Mpya.
Tunataka
Katiba ielekeze kutungwa kwa sheria ya uraia itakayofafanua vigezo na masharti
kuhusu haki na wajibu wa Raia wa Tanzania mwenye uraia wa pili; Katiba itamke
kuwa raia wa kuzaliwa wa Tanzania hatapoteza uraia wake kwa sababu tu amepata
uraia wa nchi nyingine na Katiba ilinde haki ya uraia wa kuzaliwa kwani ni haki
ya msingi ambayo haitakiwi kuvuliwa na mamlaka yoyote ile.
FAIDA ZA
URAIA WA NCHI MBILI
Tafiti zinaonesha kuwa, Uraia wa Nchi Mbili ni
nguzo kuu ya kuandaa mazingira nje ya nchi kuwawezesha raia hao kustawi
kielimu, kiafya, kiuchumi, kijamii na kisiasa kama ifuatavyo:
i. Elimu: Elimu ni chimbuko la mafanikio. Uraia wa
Nchi mbili utawawezesha kusoma katika shule za Serikali, kulipa ada za chini za
raia na kupata ufadhili wa masomo (scholarships).
ii. Ajira:
Kupata ajira zenye staha (decent employment). Nchi nyingi hutoa ajira nzuri (au
katika sekta rasmi) kwa raia pekee hata kama mgeni amesoma na kuwa na sifa sawa
au za juu zaidi. Vile vile watanufaika na malipo na huduma zingine uzeeni
wakiwa kama raia.
iii. Afya: Afya
katika nchi nyingi ni gharama kubwa sana hasa kwa wageni. Kama raia, Watanzania
nje ya nchi watanufaika na huduma za afya.
iv. Uchumi: Kama
raia, atakuwa na uwezo wa kujishughulisha na masuala ya kiuchumi kwa upana
zaidi, kama kupata mitaji mikubwa, kupata mikopo katika taasisi za fedha,
kupata zabuni za kibiashara, kumiliki ardhi na mali nyingine ambazo ni kwa raia
pakee.
Ushawishi na
kuitangaza nchi: Kama raia, Watanzania ughaibuni watakuwa na fursa nzuri na
UHAMASISHAJI
WA JAMII KUHUSU DIASPORA
Wizaraya
Mambo yaNje, kupitia Idara yake ya Diaspora imeanza mchakato wa kuhamasishawa
na nchi na kutoa elimu kuhusu masuala ya Diaspora. Hivi sasa, Wizara itaanza
kushirikiana na Vyombo vya Habari (radio, televisheni na mitandao ya kijamii)
kuongelea umuhimu wa Diaspora katika kukuza uchumi wa Tanzania.
Wizara
inasisitiza kuwa taifa lina jukumu la kulinda haki za Watanzania waishio nje
kama linavyowajibika kwa raia wanaoishi nchini.
7. MKUTANO KUHUSU KUPINGA BIASHARA HARAMU YA WANYAMAPORI ULIOFANYIKA
LONDON, UINGEREZA
Mhe. Rais Jakaya Mrisho Kikwete alihudhuria Mkutano wa Kimataifa wa
kuhusu biashara haramu ya wanyamapori. Mkutano huu ulifanyika jijini London,
Uingereza kuanzia tarehe 12-13 Februari 2014. Mkutano huu uliandaliwa na
serikali ya Uingereza na ulichagizwa na juhudi za Mwanamfalme Charles pamoja na
wanae William na Harry katika kushughulikia tatizo hili.
Mkutano uliikutanisha jumuiya ya kimataifa kwa lengo la kujadili na
kutafuta mbinu za kumaliza kabisa biashara hii haramu hasa ya pembe za ndovu na
faru. Biashara hii imekua sana siku za karibuni hasa kutokana na kuongezeka kwa
soko la pembe za ndovu na faru katika nchi za Asia. Uchunguzi wa kimataifa
umeonyesha kuwa biashara hii imechukua sura ya kimataifa na kushirikisha
magenge ya Kimataifa ya kihalifu kutokana na kuwa na faida kubwa sana.
Kutokana na
kushiriki kwa magenge ya kihalifu ya Kimataifa, biashara hii imehusishwa na
kufadhili shughuli za kigaidi, migogoro ya kisiasa na kijamii kwenye baadhi ya
maeneo hasa barani Afrika. Mwelekeo huu umeifanya jumuiya ya kimataifa kuanza
kuliangalia tatizo la ujangili sio tu kama tatizo la kiuhifadhi (conservation
problem) bali pia kama tatizo linalogusa usalama wa Kimataifa (international
security).
Tanzania ni
miongoni mwa nchi ambazo zimeathirika sana na biashara hii kutokana na kuwa
tembo na faru wengi sana. Ujangili umekuwa ni tatizo sugu kwa nchi yetu tangu
enzi za Uhuru mpaka leo. Katika kipindi chote hiki, serikali imeendelea
kupambana vikali na majangili kuhakikisha wanyama hawa adhimu wanalindwa na
hawapotei katika ardhi yetu. Kwa mfano, baada ya Uhuru Tanzania inakadiriwa
ilikuwa na tembo 350,000, kutoka na ujangili uliokithiri katika miaka ya 1980
idadi yao ilishuka na kufikia tembo 55,000 tu mwaka 1987.
Serikali ya
wakati huo ikaanzisha operesheni iliyojulikana kama “Operesheni Uhai” ili
kupambana na ujangili. Oparesheni hii ilikuwa na mafanikio makubwa na mafanikio
haya yalichagizwa pia na marufuku ya biashara ya pembe za ndovu na faru
iliyoweka mwaka 1989 na Mkataba wa Kimataifa wa Kuzuia Biashara ya Wanyama
walio katika tishio la kupotea(CITES). Kutokana na haya, idadi ya tembo
iliongezeka maradufu na kufikia 110,000 mwaka 2009 na ujangili ukawa
umedhibitiwa kwa kiwango kikubwa.
Kutokana na
kupanuka sana kwa soko la bidhaa hizi hasa kwenye nchi za Asia miaka ya
karibuni, wimbi la biashara hii limerudi kwa kasi kubwa sana. Biashara hii
imerejea ikiwa na changamoto nyingi sana ikiwemo utumiaji wa mbinu za kisasa
kabisa za ujangili. Kama ilivyokuwa huko nyuma kumekuwa na juhudi kubwa sana
kwa upande wa serikali kuhakikisha kuwa hali hii, kama ilivyokuwa huko nyuma,
inadhibitiwa. Katika juhudi hizo, hivi karibuni Mhe. Rais aliridhia utumiaji wa
jeshi letu katika kupambana na kudhibiti biashara hii na hivyo
“Oparesheni
Tokomeza” ikaanzishwa.
Kwa bahati mbaya sana kumekuwa na upotoshwaji mkubwa wa juhudi za
serikali za kupambana na bishara hii haramu. Baadhi ya magazeti ya Kimataifa
yamediriki kuihususha serikali yetu na bishara hii eti kutokana na wao
kutokuona uthabiti wa juhudi za serikali kupambana na bishara hii. Tumeenda
London kushiriki mkutano huu tukiwa na mambo matatu ya msingi:-
i. Tukiwa
miongoni mwa wahifadhi (custodians) wa tunu hii ya wanyama, tumeenda kuungana
na jumuiya ya Kimataifa kusaidia kutafuta mbinu za kudhibiti na kumaliza kabisa
bishara hii haramu na ambayo inatuathiri sana ukizingatia wanyama hawa nbi
kivutio kikubwa cha utalii ambao kwetu moja ya sekta zinazotuingizia fedha
nyingi za kigeni.
ii. Kubadilishana
mbinu na kuweka kumbukumbu sawa kwa kuelezea juhudi ambazo serikali yetu
inazifanya katika kudhibiti biashara hii.
iii. Kuomba
usaidizi wa kimataifa pale ambapo juhudi zetu binafsi zinakinzwa na uhaba wa
rasilimali, ukosefu wa mbinu za kisasa, ujuzi na uzoefu.
Mkutano ulikuwa na mafanikio sana ambapo Mhe Rais alopata fursa ya
kuhutubia. Katika hotuba yake aliungana na viongozi wa kimataifa kupongeza
juhudi za serikali ya Uingereza kuitisha mkutano huu muhimu kwenye muda
mnuafaka. Katika hotuba yake, pamoja na kuelezea juhudi ambazo serikali yake
inazifanya, alisisitiza umuhimu wa kuhakikisha kuwa soko la bidhaa hizi huko
katika nchi za Asia linatokomezwa kabisa kama moja ya njia za kuimaliza
biashara hii. Pia aliezea juhudi ambazo serikali ya Tanzania imekuwa ikifanya
kuhakikisha kuwa tembo na faru waliopo wanalindwa na wanapewa mazingira ya
kuzaliana.
Mkutano
ulikubaliana pamoja na mambo mengine, kuongeza ushirikiano wa Kimataifa katika
kudhibiti bishara hii; kupiga marufuku ya jumla ya bishara hii kimataifa bila
kutoa ahueni
(moratorium) kama ilivyokuwa inafanyika awali; kuhakikisha kuwa nchi
zinapitisha sheria kali dhidi ya ujangili na kuhakikisha kuwa hazina ya meno
yaliyohifadhiwa sasa hivi yanakosa thamani (putting stock pile beyond economic
use).
8.
MAANDALIZI YA MICHEZO YA JUMUIYA YA MADOLA
Michezo ya Jumuiya ya Madola (Commonwealth Games) itafanyika Glasgow,
Scotland kuanzia tarehe 23 Julai hadi 3 Agosti 2014.
Miongoni mwa
alama kuu za michezo hiyo ni Kifimbo cha Malkia (Commonwealth Queen’s
Baton)
ambacho hukimbizwa kwa nchi wanachama wa Jumuiya ya Madola kuashiria kuanza kwa
michezo hiyo. Kifimbo kicho kilikuja hapa nchini kuaniza tarehe 18 hadi 20
Januari 2014 na kupokelewa na Mhe. Jakaya Mrisho Kikwete, Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania.
No comments:
Post a Comment