ADV

ADV

ADVERTISEMENT CORNER

HUDUMA YA KUKATA TICKET ZA NDEGE ONLINE


SOMA HABARI

SOMA HABARI

Thursday, March 20, 2014

Shabiki afariki uwanja wa Taifa wakati wa mechi ya Yanga na Azam, aliishiwa nguvu wakati anashangilia goli la Yanga




  Shabiki afariki uwanja wa Taifa wakati wa mechi ya Yanga na Azam, aliishiwa nguvu wakati anashangilia goli la Yanga  
Katika hali isiyokuwa ya kawaida, shabiki mmoja aliyekuwa akishuhudia mechi katia ya Yanga na Azam, alifariki dunia jana jioni katika uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.
Shabiki huyo alizimia uwanjani mara baada ya Yanga kupata goli la kwanza na la pekee lililofungwa na Didier Kavumbagu.

Hata hivyo wasamaria wema walimbeba shabiki huyo na kisha kuwekwa kwenye machela na kupelekwa katika vyumba vya huduma ya kwanza.
Muda mchache baadae vipaza sauti vya Uwanja waTaifa vilisikika vikitangaza kwamba kuna mtu amezimia na kama kuna ndugu au mtu yoyote wa karibu na mtu huyo ajitokeze. 

Kwa mujibu wa Daktari Nassoro Matuzya shabiki huyo ambaye inasemekana ni wa timu ya Yanga alianza kuishiwa nguvu mara baada ya Yanga kupata bao ambako alisimama na kushangilia kwa nguvu.

Shabiki huyo alichukuliwa na watu wa msalaba mwekundu na kwenda kupewa huduma ya kwanza kwenye vyumba maalum uwanjani hapo na taarifa zimeeleza kuwa mtu huyo alifariki akiwa katika chumba cha huduma ya kwanza.

Taarifa za uhakika kutoka TFF kwa mtu ambaye hakutaka kutajwa jina lake kwa madai kuwa yeye sio msemaji, ameshuhudia mwili wa mtu huyo ambaye jina lake halikuweza kupatikana mara moja, na kwamba ulipelekwa katika hospitali ya Temeke.
Katika mechi hiyo iliyotoa matokeo ya 1-1, Yanga walianza kupata bao katika kipindi cha kwanza dakika ya 14.

Hata hiyvo Azam ilipambana vikali na kurudisha bao katika kipindi cha pili ikiwa ni dakika ya 82 wakiwa wachezaji kumi baada ya Erasto Nyoni kutolewa kwa kadi nyekundu kwa kosa la kumtukana muamuzi.

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...