Wanakijiji
wa Kijiji cha Maisha Plus ambao ni Vijana wa Maisha Plus pamoja na Mama
shujaa wa Chakula wakimsikiliza kwa makini Mkurugenzi wa Oxfam Tanzania
Jane Foster ambaye hayupo.
Kutoka Kulia ni Mkurugenzi
wa Oxfam Tanzania Jane Foster, Mkamiti Mgawe wa Oxfam na Babu kutoka
kijiji cha Maisha Plus Rajabu Msumi wakiongea na washiriki wa Maisha
Plus na Mama Shujaa wa Chakula.
Mkamiti Mgawe wa tatu kutoka kushoto akimtambulisha Malkia wa Kijiji cha Maisha Plus kwa Mkurugenzi wa Oxfam Tanzania Jane Foster.
Mkurugenzi wa Maisha Plus akioneshwa Shughuli mbalimbali zinazofanywa na wanakijiji wa Kijiji cha Maisha Plus.
Mkurugenzi
wa Oxfam Tanzania Jane Foster akioneshwa moja ya jiko lililotengenezwa
na akina mama Shujaa wa Chakula pamoja na Vijana wa Maisha Plus.
Mkurugenzi wa Oxfam Tanzania Jane Foster akioneshwa moja ya Ghala la kienyeji na imara kwa ajili ya kuhifadhia vyakula.
Mkurugenzi
wa Oxfam Tanzania Jane Foster akioneshwa shamba linalotumia kilimo hai
na cha kisasa katika kijiji cha Maisha Plus ambapo wahusika wa shughuli
hizo na uangalizi wa Shamba hilo ni Mama Shujaa wa Chakula na Vijana
washiriki wa Maisha Plus.
Mkurugenzi
wa Oxfam Tanzania Jane Foster akiendelea na ziara yake ndani ya kijiji
cha Maisha Plus na kujionea mambo mbalimbali yanayo endelea Kijijini
hapo.
**********************************
Chereko
na vifijo vilitawala katika kijiji cha Maisha Plus kuonyesha furaha kwa
kuwa Katika siku hii kijiji kilitembelewa na Mkurugenzi wa Oxfam
Tanzania Jane Foster akiongozana na mfanyakazi wa Oxfam Mkamiti Mgawe
ili kujionea miradi mbalimbali waliyobuni wanakijiji cha Maisha Plus.
Mkurugenzi
alifurahishwa sana na kazi zilizofanywa kwa usatadi na umahiri wa hali
ya juu na kujionea hazina za vipaji vya wanakijiji hao. Oxfam Tanzania
ni moja ya wadhamini na wadau wakuu wa Maisha Plus na Mama Shujaa wa
Chakula 2014.
Miradi
iliyotembelewa ni pamoja ya utengenezaji wa batiki, sabuni, kikapu cha
ajabu, bustani ya kuhama, jiko la gesi, aina mbalimbali za majiko ya
udongo wa mfinyanzi, ufugaji bora wa kuku na nyuki, bustani za mboga na
shamba linalotumia kilimo hai na kilimo cha kisasa.
Chereko
na vifijo vilitawala katika kijiji cha Maisha Plus kuonyesha furaha
waliyonayo na pia kusherehekea siku ya mama duniani ambayo huadhimishwa
kila ifikapo tarehe 11 Mei. Katika siku hii kijiji kilitembelewa na
Mkurugenzi wa Oxfam Tanzania Jane Foster akiongozana na mfanyakazi wa
Oxfam Mkamiti Mgawe kujionea miradi mbalimbali waliyobuni wanakijiji cha
Maisha Plus.
Mkurugenzi
alifurahishwa sana na kazi zilizofanywa kwa ustadi na umahiri wa hali
ya juu na kujionea hazina za vipaji vya wanakijiji hao.
Oxfam
Tanzania ni moja ya wadhamini na wadau wakuu wa Maisha Plus na Mama
Shujaa wa Chakula 2014. Miradi iliyotembelewa ni pamoja ya utengenezaji
wa batiki, sabuni, kikapu cha ajabu, bustani ya kuhama, jiko la gesi,
aina mbalimbali za majiko ya udongo wa mfinyanzi, ufugaji bora wa kuku
na nyuki, bustani za mboga na shamba linalotumia kilimo hai na kilimo
cha kisasa.
No comments:
Post a Comment