ADV

ADV

ADVERTISEMENT CORNER

HUDUMA YA KUKATA TICKET ZA NDEGE ONLINE


SOMA HABARI

SOMA HABARI

Saturday, December 20, 2014

Amtupa mjukuu nje ya basi likiwa katika mwendo


Saturday , 20th Dec , 2014
Mtoto mmoja mwenye umri wa miaka Sita amefariki dunia baada ya kutupwa na bibi yake nje ya basi kupitia dirishani wakati basi likiwa katika mwendo wa kasi mkoani Singida.
Bi. Lawaridi Saidi
Katika hali isiyo kuwa ya kawaida mama moja aliye kuwa akisafiri na  mtoto wake mmoja na wajukuu zake wawili, aliamua kumtupa mjukuu wake wa miaka sita dirishani huku basi likiwa katika mwendo kasi na kusababisha kifo chake baada ya kufikishwa katika hospitali ya mkoa wa Singida.
Akithibitisha kutokea kwa tukio hilo kamanda wa jeshi la polisi mkoani Singida ACP Thobias Sedoyeka, amesema mama huyo aliye tambulika kwa jina la Lawaridi Saidi mweye umri wa miaka 46 aliyekuwa akisafiri na basi namba T 981 ALS kampuni ya Salumu Clasc lilokuwa likitokea Dar-es-salaam na kuelekea Kigoma.
Amesema alipofika katika kijiji cha Iguguno wilaya ya Mkalama siku ya tarehe 18/12/2014 saa 2 usiku alimtupa mjukuu wake Mayasa meshaki dirisani huku basi likiwa katika mwendo kasi.
Kwa upande wake mganga wa zamu katika hospitali ya mkoa wa Singida Dkt Adamu Hussein amesema walimpokea mtoto huyo akiwa katika hali mbaya akiwa hapumui vizuri na damu kutoka katika masikio,baada ya kumpatia matibabu alilazwa na siku ya pili alifariki kutokana na kupasuka kwa fuvu la kichwa.
Akieleza jinsi alivyo mtupa mjukuu wake huku basi likiwa katika mwendo kasi  Lawaridi Saidi  ambaye ni mkazi wa  Kongowe jijini Dar-es-salaam amesema baada ya kuamka akiwa katika hali ya usingizi alijikuta akimchukuwa mjukuu wake Mayasa  na kumtupa dirishani na hatimaye abiria wakaanza kumpiga  na kuamuru basi lisimame na kumtafuta mtoto huyo.

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...