ADV

ADV

ADVERTISEMENT CORNER

HUDUMA YA KUKATA TICKET ZA NDEGE ONLINE


SOMA HABARI

SOMA HABARI

Thursday, January 29, 2015

Pinda abanwa kuhusu BVR, vitambulisho vya Taifa



Waziri Mkuu Mizengo Pinda akizungumza na Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe nje ya ukumbi wa Bunge mjini Dodoma 
Na Boniface Meena, Mwananchi

Posted  Alhamisi,Januari29  2015  saa 16:28 PM
Kwa ufupi
Katika kipindi cha maswali kwa Waziri Mkuu bungeni leo, Kiongozi wa Kambi ya Upinzani, Freeman Mbowe alimtaka Pinda kueleza Serikali ina mpango gani kuhakikisha hakuna tatizo litakalotokea katika uandikishaji wa daftari hasa ikizingatiwa muda uliopo hautoshi na majaribio ya uandikishaji kwa BVR umeibua kasoro nyingi.

Dodoma. Waziri Mkuu, Mizengo Pinda leo amebanwa bungeni kuhusu mkanganyiko uliopo katika mpango wa uandikishwaji wa daftari la wapigakura kutumia mashine za BVR na mgogoro uliopo kati ya Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa(Nida) na Tume ya Taifa ya Uchaguzi(Nec)  kuhusu vitambulisho vya kupigia kura.
Katika kipindi cha maswali kwa Waziri Mkuu bungeni leo, Kiongozi wa Kambi ya Upinzani, Freeman Mbowe alimtaka Pinda kueleza Serikali ina mpango gani kuhakikisha hakuna tatizo litakalotokea katika uandikishaji wa daftari hasa ikizingatiwa muda uliopo hautoshi na majaribio ya uandikishaji kwa BVR umeibua kasoro nyingi.
Mbowe alisema majaribio ya uandikishaji wa kutumia BVR katika jimbo la Kawe, Wilaya ya Mlele na Kilombero yameibuka na changamoto mbalimbali na huku nchi ikitakiwa kuandikisha wapigakura zaidi ya milioni 24.   
Pia alitaka kujua kama muda uliopangwa wa uandikishaji unatosha ikizingatiwa zimebaki siku 90 kufikia kwenye kura ya maoni.
Akijibu swali hilo Pinda alisema: “Aliyoyasema Mbowe Serikali haiwezi kuyapuuza hata kidogo na ni kweli mchakato huo umekuwa na matatizo kidogo hasa ya fedha na Serikali imekuwa ikipambana ili kuweza kufanikisha mchakato huo.
“Tatakwenda na ratiba kama Tume ilivyopanga na nakubaliana na Mbowe kwamba lazima kuwe na ushirikishwaji hasa wa vyama,”alisema Pinda.
Alisema kuwa BVR 250 zilizoingia kwa ajili ya majaribio ilikuwa ni za kupima uwezo wake na kweli kuna matatizo ya hapa na pale ambayo yanashughulikiwa ili yasiwepo wakati zoezi rasmi litakapoanza rasmi na kuweza kufika salama kwenye uchaguzi mkuu.
Akijibu suala la muda kutokutosha uandikishaji wa daftari hilo Pinda alisema kama ikitokea Nec ikitaka muda uongezwe  basi atawasilisha suala hilo bungeni.
Alisema mashine za BVR kwa taarifa alizopewa na Nec ni kwamba moja inaandikisha watu 70 kwa siku moja na siyo 22 kama alivyosema Mbowe.

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...