ADV

ADV

ADVERTISEMENT CORNER

HUDUMA YA KUKATA TICKET ZA NDEGE ONLINE


SOMA HABARI

SOMA HABARI

Thursday, March 12, 2015

Mama Maria asema Makongoro ana haki kugombea urais



Mke wa Baba wa Taifa, Mama Maria  Nyerere akizungumza na waandishi wa habari  nyumbani kwake Msasani jana, baada ya kuzushiwa kifo na watu wasiojulikana. Picha na Said Khamis 
Na Suzan Mwillo, Mwananchi

Posted  Jumatano,Marchi11  2015  saa 9:41 AM
Kwa ufupi
  • Asema pia mwanaye mwingine anataka kuwania nafasi hiyo

Dar es Salaam. Mke wa Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Nyerere, Mama Maria Nyerere amesema kuwa mtoto wake, Makongoro Nyerere ana haki ya kugombea nafasi ya urais katika Uchaguzi Mkuu wa Oktoba.
Ijumaa wiki iliyopita, Makongoro alilieleza gazeti hili kuwa uamuzi wake kuhusu kuwania kiti hicho utajulikana mara kipenga kitakapopulizwa na CCM.
Kauli ya Makongoro ilitokana na uvumi uliokuwa umeenea katika mitandao ya kijamii kuwa mtoto huyo wa tano wa mwalimu Nyerere alikuwa anaandaliwa na watu waliofanya kazi karibu na mwalimu awanie nafasi hiyo.
Akizungumza na waandishi ya habari nyumbani kwake Msasani  jana, Mama Maria alisema mwanaye ana haki ya kugombea.
Mama Maria aliyekuwa ameawaalika waandishi wa habari kuzungumzia uvumi uliosambaa kuwa amefariki dunia, alitoa kauli hilo baada ya kuulizwa kama uvumi huo unahusiana na habari kuwa mwanaye anataka kugombea urais.
Alisema, “Hapana. Hayo mambo hayahusiani na mwanangu kutaka kuwania urais… yeye ni raia wa Tanzania na hiyo ni haki yake ya msingi,”
Pia, alidokeza kuwa wakati akizungumza na mwanaye mwingine juzi baada ya uvumi wa kifo chake, naye alimwambia kuwa anataka kuwania nafasi hiyo.
Akitoa ufafanuzi kuhusiana na uvumi huo alisema kuwa, taarifa za uvumi wa kifo chake zilikuwa za furaha kwake na wala siyo za huzuni kama watu wengi walivyodhania.
 “Tumekuwa tukifanya maombi ya kusali na kufunga kwa siku 40 kabla ya kipindi hiki cha Kwaresima kwa ajili ya kuliombea taifa na dunia kwa ujumla. Na sasa tunafunga tena, hivyo kwangu jambo hilo ni majibu ya maombi tunayofanya. Nimefurahia kwa sababu naona maombi yanafanya kazi. Haya ni majibu, tunasema tumepita mashetani,”alisema Mama Maria huku akitania kuwa karne hii ni ya kisasa kweli, hata marehemu anaongea.
Aliongeza;  “Baada ya kupokea taarifa hizo, kwa kuwa nilikuwa nimelala nilichofanya niliamka nikasali…nadhani Watanzania wanahitaji sana kusali, sala na kazi. Kama Taifa pia tunahitaji kuwa na siku moja maalumu ya maombi.”
Licha ya kusema kuwa taarifa hizo zilikuwa za furaha kwake, Mama Maria alisema taarifa hizo zilizua hofu kubwa kwa familia yake na Taifa zima kwa ujumla.
Alisema juzi mchana alianza kupokea simu kwa wingi tofauti na ilivyo kwa siku za kawaida.

Source: Mwananchi

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...