
DAR ES SALAAM.

- Mhe. Dkt Mohammed Gharib Bilali – Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano,
- Mhe. Mizengo K. P. Pinda (Mb.) - Waziri Mkuu,
- Mhe. Seif Sharif Hamad – Makamu wa Kwanza wa Rais – Serikali ya Mapinduzi Zanzibar,
- Mhe. Balozi Seif Ali Iddi (Mb.) - Makamo wa Pili wa Rais - Serikali ya Mapinduzi Zanzibar,
- Mhe. Mathias Chikawe – Waziri wa Katiba na Sheria,
- Mhe. Abubakar Khamis Bakary - Waziri wa Katiba na Sheria wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar,
- Mhe. Jaji Frederick M Werema - Mwanasheria Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,
- Mhe. Othman Masoud Othuman - Mwanasheria Mkuu wa Zanzibar,
- Viongozi wa Vyama vya Siasa,
- Waheshimiwa Wajumbe wa Tume na Wajumbe wa Sekretarieti ya Tume ya Mabadiliko ya Katiba,
- Ndugu Wananchi,
- Wageni Waalikwa
- Waandishi wa Habari Mabibi na Mabwana.
- UTANGULIZI
Ndugu Wananchi,
Awali ya yote namshukuru mwenyezi mungu kwa kutuwezesha kufikia hatua hii ya leo ya kuzindua Rasimu ya Katiba. pia, niwashukuru ninyi nyote mliohudhuria halfa hii ikiwa ni mwendelezo wa mchakato muhimu wa Mabadiliko ya Katiba ya nchi yetu.