ADV

ADV

ADVERTISEMENT CORNER

HUDUMA YA KUKATA TICKET ZA NDEGE ONLINE


SOMA HABARI

SOMA HABARI
Showing posts with label Tanzania.. Show all posts
Showing posts with label Tanzania.. Show all posts

Wednesday, August 14, 2013

MBOWE AANIKA HADHARANI JINSI ANAVYOKOSWA KOSWA KUUAWA ATAJA LIST YA WANAOMUWINDA USIKU NA MCHANA


Mwenyekiti wa Chama cha demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) amesema amenusurika kuuawa katika matukio matatu yanayotokana na harakati zake za kisiasa.

Akihutubia umati mkubwa wa wananchi katika mji wa Meatu mkoani Simiu jana, Mbowe alisema hata kama atauawa hatasikitika na kwamba Watanzania wasimlilie.

Mbele ya umati huo akiwemo mbunge wa Maswa, John Shibuda, Mbowe alisema kuna watu ndani na nje ya CHADEMA ambao wamekuwa wakifanya kila mbinu kuwaangamiza viongozi na makada wa chama hicho.

Mbowe alisema viongozi wa CHADEMA akiwemo yeye mwenyewe wamekumbana na misukosuko mingi, ikiwemo yenye kuhatarisha maisha yao kutoka kwa wanasiasa wasioipenda nchi, lakini kwa neema ya Mungu wamenusurika.


“Leo hii hata kama nikiuawa, naomba Watanzania msinililie. Mbele ya jeneza langu, nizikeni huku mkisema Bwana Alitoa na Bwana Ametwaaa, Jina Lake Lihimidiwe.

“Leo CHADEMA sio ya Slaa wala ya Mbowe bali ya Watanzania iliyojengwa kwa misukosuko mingi na mkono wa Mungu.

“Mmeshuhudia namna viongozi wake walivyonusurika kuuawa na kufungwa, na watu kufunguliwa na kesi mbalimbali.

“Kwa hiyo yeyote awe kiongozi wa CHADEMA au watawala anayetamani kuibomoa chadema hataweza kamwe,” alisema.

Kiongozi huyo alisema wale wote wanaofanya hivyo, wajue kuwa wanapambana na mkono wa Mungu na wamelenga kuwaumiza Watanzania.

“CHADEMA ina baraka za Mungu na ndio maana imeshinda na kupita katika majaribu mengi ya watawala ambao wameshindwa kuifuta au kuibomoa,” alisema.

Mbowe na viongozi wengine wa CHADEMA wako katika ziara ya mikutano ya mabaraza ya wazi kujadili rasimu ya Katiba mpya ambayo itaendeshwa nchi nzima kwa nia ya kukusanya maoni ya Watanzania.

Tuesday, August 6, 2013

RAIS JAKAYA KIKWETE NA MARAIS WASTAAFU MZEE MWINYI NA MZEE MKAPA WAALIKWA FUTARI NYUMBANI KWA KATIBU MKUU KIONGOZI BALOZI OMBENI SEFUE


Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiwa na Rais Mstaafu wa awamu ya tatu Mhe Benjmani William Mkapa na Rais wa Awamu ya pili Alhaj Ali Hassan Mwinyi wakati wa futari iliyoandaliwa na Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Sefue (wa pili kushoto) nyumbani kwake Oysterbay jijini Dar es salaam Jumapili
 Katibu Mkuu kiongozi Balozi Ombeni Sefua akimshukuru Rais Jakaya Mrisho Kikwete na Rais Mstaafu wa awamu ya tatu Mhe Benjmani William Mkapa na Rais wa Awamu ya pili Alhaj Ali Hassan Mwinyi kwa kuhudhuruia  futari aliyoaiandaa nyumbani kwake Oysterbay jijini Dar es salaam Jumapili
 Shehe Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Alhaj Alhad akiongoza dua kwa waalikwa waliohudhuyruia  futari aliyoaiandaa nyumbani kwake Oysterbay jijini Dar es salaam Jumapili
 Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiwa na Rais Mstaafu wa awamu ya tatu Mhe Benjmani William Mkapa na Rais wa Awamu ya pili Alhaj Ali Hassan Mwinyi baada ya  futari iliyoandaliwa na Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Sefue Oysterbay jijini Dar es salaam Jumapili
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiwa na Rais Mstaafu wa awamu ya tatu Mhe Benjmani William Mkapa na Rais wa Awamu ya pili Alhaj Ali Hassan Mwinyi baada ya  futari iliyoandaliwa na Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Sefue (kushoto) nyumbani kwake Oysterbay jijini Dar es salaam Jumapili.Picha na IKULU

Saturday, July 27, 2013

RAPA KALA JEREMIAH AMWANDIKIA WARAKA MZITO WAZIRI MKUU MSTAAFU MHE.EDWARD NGOYAI LOWASSA


tANGAZO KWA UMMA

MIMI KALA JEREMIAH NILIKUWA MSANII WA KWANZA TANZANIA KUMSEMA MHESHIMIWA EDWARD LOWASA KUPITIA WIMBO WANGU UITWAO WIMBO WA TAIFA BAADA YA MHESHIMIWA KUKUMBWA NA KASHFA YA UFISADI WA RICHMOND.KWA KIPINDI KILE KILA MMOJA WETU ALIHAMAKI SANA NA KUONA KWELI MZEE WA WATU NI FISADI.KWENYE WIMBO HUO KUNA MISTARI NILISEMA. mi siyo mwana siasa sisubiri tume ichunguze nistaafu ka Lowasa.

KWA KUWA MIMI NI MZURI SANA KWENYE KUFANYA UCHUNGUZI BINAFSI NILITUMIA MUDA MWINGI SANA KULICHUNGUZA SWALA HILI LA KASHFA HII NA BAADAE NILIGUNDUA KUWA NI SWALA LA KISIASA.NA YALIKUWA NI MAPITO AMBAYO MWANADAMU YOYOTE HUPEWA MUDA WA KUPITIA MAGUMU ILI KUPIMWA IMANI YAKE KWA MUNGU.

BAADA YA KUGUNDUA HAYO MWAKA JANA NILITENGENEZA WIMBO UNAOITWA AZIMIO LA ARUSHA AMBAO UPO KWENYE ALBUM YANGU YA PASAKA AMBAYO IKO SOKONI TOKEA MWAKA JANA. KATIKA WIMBO HUO WA AZIMIO LA ARUSHA NILIANDIKA MISTARI IFUATAYO. walipiga dili waka msakizia lowasa ili kuficha siri kali.NILIANDIKA MSTARI HUU BAADA YA KUFANYA UCHUNGUZI NA KUJIRIDHISHA KUWA MHESHIMIWA NI KIONGOZI BORA SANA NA HASA KWA UAMUZI WAKE WA KUJIUZULU BILA SHINIKIZO KUBWA NA WAKATI KWA NAFASI ALIYOKUWA NAYO YA UWAZIRI MKUU ALIKUWA NA UWEZO WA KUGOMA KUJIUZULU NA HASA KWA KUWA HAKUWA FISADI KAMA ILIVYOSEMWA.

MWEZI WA TATU MWISHONI MWAKA HUU NILITOA WIMBO UNAOKWENDA KWA JINA LA KARIBU DAR AMBAKO NILISEMA dar es salam ingekuwa nchi Rais angekuwa Lowasa huku watu washashtukia kuna mchezo kwenye siasa HAPA NILIKUWA NAMAANISHA KUWA WATU WENGI WANAOISHI DAR WANAWAHI KUJUA MAMBO YA WANASIASA KWA KUWA WANASIASA WANAISHI HUKU LAKINI PIA WATAFITI WENGI WA MAMBO YA KISIASA WANAISHI HUKU KWA HIYO NI RAHISI ZAIDI KUUJUA UKWELI MAPEMA.

NAAMINI KUONDOKA KWA LOWASA KWENYE UWAZIRI MKUU KUMEZOROTESHA MAENDELEO YA TAIFA KWA KIASI FLANI

NDUGU ZANGU WATANZANIA NI WAZI KUWA LOWASA NI JEMBE TENA JEMBE LA KAZI KUMBUKENI BILA LOWASA KUSINGEKUWA NA SHULE ZA KATA TANZANIA,NA ANGEENDELEA KUWEPO MADARAKANI ALIKUWA NA MPANGO WA KUANZA MCHAKATO WA ZAHANATI ZA KATA.IKUMBUKWE PIA LOWASA NDIYE ALIYESIMAMIA UJENZI WA CHUO CHA UDOM TENA KWA PESA ZA KITANZANIA BILA KUOMBAOMBA VIMIKOPO.

MRADI WA MAJI KUTOKA MWANZA KWENDA SHINYANGA NI KAZI YA LOWASA. ZIPO KAZI NYINGI AMBAZO NIKIZITAJA ZOTE NAWEZA KUJAZA UKURASA.NACHOJARIBU KUSEMA HAPA NI KWA KUWA MIMI NI MSANII NA NI KIOO CHA JAMII NINGEOMBA WEWE MWANAJAMII CHUKUA HATUA YA KUFANYA UCHUNGUZI BINAFSI KUHUSU LOWASA.BILA KUFUATA MKUMBO WA KISIASA NAAMINI UTAKUBALIANA NA MIMI KUWA LOWASA NI JEMBE.

MIMI HUWA NAPENDA KUSOMA VITABU VYA WANAHARAKATI NA KUNA KITABU KIMOJA NILIKIPITIA CHA MWANAHARAKATI KUTOKA ITALY AITWAE NICCOLO MACHIAVELLI AMBAYE ALIZALIWA MWAKA 1469 NA KUFARIKI 1527. KATIKA ENZI ZA UHAI WAKE ALIWAHI KUANDIKA VITABU KADHAA LAKINI KATI YA VITABU HIVYO KITABU KIITWACHO THE PRINCE NDICHO KILIMPA HESHIMA KUBWA SANA KWA KUWA ALIIKOSOA SERIKALI YA KIFALME YA KIPINDI HICHO KITU AMBACHO HAKIKUWA RAHISI KWA MTU KUFANYA HASA IKIKUMBUKWA KUWA ENZI ZA UFALME ZILIKUWA ENZI ZA UBABE. KATIKA MANENO KUTOKA KWENYE KITABU HICHO AMBAYO NINGE PENDA KUKUSHIRIKISHA WEWE NDUGU YANGU MTANZANIA NI MANENO YAFUATAYO MACHIAVELLI ALIANDIKA HIVI. kuna kipindi ambacho mataifa yanapita katika vipindi vigumu. na kwa kipindi hicho kigumu mataifa hayo yatahitaji sana kupata kiongozi mwenye kuweza kuchukua maamuzi magumu,na ambaye hatakuwa chini ya sauti ya mtu mwingine, na ambaye ataweza kuyatekeleza maamuzi magumu kwa haraka hata kama ni kwa kuwaumiza wachache ili wengi wawe huru.atakayekuwa tayari kutekeleza jambo baya ili likapita na kusahaulika na atakayetekeleza mambo mazuri kwa muda mrefu na yakaendlea kukumbukwa.kiongozi huyo atatakiwa kuchagua kuogopwa ama kupendwa lakini ni bora akachagua kuogopwa lakini akitenda haki kwa wananchi husika.HAYO NI BAADHI YA MANENO ALIYOANDIKA MACHIAVELLI KWENYE THE PRINCE KITABU AMBACHO KILIMPELEKEA KUITWA NA MFALME NA KUPEWA NAFASI YA JUU YA UONGOZI KATIKA SERIKALI HIYO YA KIFALME.

KWA MAONI YANGU NADHANI TAIFA LETU LIMEPITIA VIPINDI VIGUMU KADHAA NA KWA MANENO YA BWANA MACHIAVELLI NADHANI KIONGOZI ANAYEFAA AMBAYE ANAWEZA AKACHUKUA MAAMUZI MAGUMU NA AMBAYE HAWEZI KUWA CHINI YA SAUTI YA MTU MWINGINE NI MHESHIMIWA EDWARD NGOYAI LOWASA.

tafakari chukua hatua

Saturday, July 20, 2013

Taarifa Maalum Kwa Umma Kutoka Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ):Miili ya Askari wa Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) waliopoteza maisha Jimboni Darfur nchini Sudan kutokana na shambulizi la ghafla, itawasili kwa ndege maalum katika uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Mwalimu J.K. Nyerere – Terminal one (Air Wing) saa tisa alasiri Julai 20, 2013


Miili ya Askari wa Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) waliopoteza maisha Jimboni Darfur nchini Sudan kutokana na shambulizi la ghafla, itawasili kwa ndege maalum katika uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Mwalimu J.K. Nyerere – Terminal one (Air Wing) saa tisa alasiri Julai 20, 2013  badala ya saa nne kama ilivyoelezwa hapo awali, waandishi wa habari wanaruhusiwa  kufika kuanzia saa saba Mchana.

Aidha, mara baada ya kuwasili miili hiyo itapelekwa katika hospitali ya rufaa ya Jeshi,  Lugalo, baada ya maandalizi,  miili hiyo itaagwa rasmi kwa heshima zote Julai 22, 2013 kuanzia saa tatu kamili asubuhi  katika viwanja vya Wizara ya Ulinzi na Jeshi la Kujenga, Upanga Jijini Dar es Salaam.

Waandishi wa habari mnaombwa kuhudhuria na kufanya ‘Coverage’ katika mapokezi na hatimaye siku ya kuaga miili hiyo ya mashujaa wetu waliopoteza maisha wakitetea amani duniani.
 
Imetolewa na Kurugenzi ya Habari na Uhusiano
Makao Makuu ya Jeshi, Upanga
SLP 9203, Simu:  0783 309963
Email: ulinzimagazine@yahoo.co.uk

Saturday, July 13, 2013

MESEJI INAYOHUSU RAISI KIKWETE KUMUUZIA NCHI OBAMA YASABABISHA WATU WAWILI KUKAMATWA





Jeshi la polisi Geita linawashikilia watu wawili kwa kosa la kusambaza ujumbe kwa njia ya simu usemao, UMEPOKEA SHILINGI 50,000.KUTOKA KWA RAIS KIKWETE KAMA SEHEMU YA MGAO WAKO BAADA YA KIKWETE KUMUUZIA OBAMA NCHI!!

Kamanda wa polisi mkoani hapo alisema kwamba watu hao walikamatwa baada ya kukutwa na msg hizo ktk simu zao za mikononi huku wakiwa wanasambaza kwa watu wengine.

Aliendelea kudai kua jeshi la polisi linatoa onyo kwa wale wote wanaowachafua viongozi wa kitaifa kwa njia za ujumbe kwa simu na kwamba watawachukulia hatua kali.

Source; Radio Free Afrika Matukio!

CHADEMA RED BRIGED NI LAZIMA IANZISHWE...MBONA CCM NA CUF WANA KUNDI LAO



 BENSON
Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kimesema hakitarudi nyuma katika mpango wa kutoa mafunzo ya ukakamavu kupitia kikundi chake cha red brigade.
Chama hicho kimesema, tayari Chama Cha Mapinduzi (CCM) na Chama cha Wananchi (CUF), vyote vikiwa miongoni mwa `vyama vikubwa nchini’, vina vikundi vya aina hiyo.

  Mkurugenzi wa Oganizasheni na Mafunzo Chadema, Singo Benson, ametoa msimamo huo jana wakati akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es salaam.
Tamko la Chadema kuanzisha mafunzo hayo, limeibua taharuki na kusababisha watu kadhaa akiwamo Rais Jakaya Kikwete, kutaka mpango huo usitishwe.

LENGO LA MAFUNZO

Benson alisema lengo la kuimarisha kikundi hicho, ni kujikinga dhidi ya mashambulizi yanayoelekezwa kwa viongozi, wanachama na wafuasi wake, ambapo CCM ikitajwa kuwa nyuma ya mashambulizi hayo.

Alisema Chadema, imekamilisha maandalizi ya mafunzo yatakayowajumuisha zaidi vijana, ili wapate mbinu za kujikinga na kuwalinda viongozi wao ikiwa ni pamoja na katika mikutano ya hadhara.

Hata hivyo, alisema mpango huo hauhusishi mafunzo ya kijeshi, akidai kwamba mafunzo kama hayo yanatolewa kwa vijana kupitia kambi maalum zinazoratibiwa na CCM.

MAKAMBI YA CCM

Benson alidai kuwa kabla ya kufanyika kwa uchaguzi mdogo wa Igunga mkoani Tabora mwishoni mwa 2011, CCM iliandaa makambi mbalimbali ya kufundisha vijana mbinu za kijeshi.

“Iweje Chadema tuambiwe kuwa ni haramu kwa mwaka huu, wakati mwaka jana vijana wa CCM walifanya mafunzo na paredi ya jeshi ambayo ni hatari kwa nchi,” alihoji.

Alidai kuwa moja ya matokeo ya kambi za vijana wa CCM kule Igunga, ni kupigwa hadi kuuawa kwa Mbwana Masoud na Msafiri Mbwambo waliotokea Arumeru Mashariki.

Alidai kuwa matukio hayo yanajulikana hadi kwa Inspekta Jenerali wa Polisi (IGP), Said Mwema, lakini hakuna hatua zilizochukuliwa.

AMGEUKIA MWIGULU

Benson alisema IGP Mwema anatakiwa kuanza kuwashughulikia Mbunge wa Iramba Magharibi Mwigulu Nchemba, kwa madai ya kuwa mmoja wa waasisi wa kuwabebesha vijana silaha za kwenda kushambulia raia wasiokuwa na hatia.

Hata hivyo IGP Mwema aliliambia gazeti hili jana kwamba atatoa tamko kuhusiana na sakata hilo Jumatatu ijayo.

“Kikwete (Rais Jakaya Kikwete) awaeleze hao vijana wa CCM wanafanyaje hayo mafunzo yao, na wamekuwa wakitumika kuwapiga viongozi wa Chadema mbele ya polisi na hakuna hatua zinazochukuliwa,” alisema.

Benson alisema kabla ya polisi kuanza kuwashughulikia Chadema, wanapaswa kuanzia CCM.

“Sasa Rais Kikwete aseme hao ni wajasiriamali ama wanajeshi, na kama ni wajasiriamali bunduki walizo nazo ni za nini,” alihoji Benson.

Hata hivyo, alisema kikundi chao walichokianzisha kipo kwa mujibu wa kikatiba na kwamba watafundishwa kulinda haki za Watanzania, kuwalinda viongozi na mikutano ya Chadema.

Alisema mafunzo ya kuimarisha kikundi cha ulinzi cha Chadema yatanza wiki ijayo katika mikoa mbalimbali.

Pia, Benson alisema leo, Chadema wanatarajia kuzindua msimamo wa chama kuhusu rasimu ya Katiba Mpya katika Shule ya Msingi ya Ukombozi iliyopo Manzese jijini Dar es Salaam.

UVCCM NAO WAIBUKA

Kwa upande wake, Jumuiya ya Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM), imeshutumu hatua ya Chadema kuanzisha mafunzo kwa kikundi hicho cha ‘Red brigade’.

Akizungumza jijini Dar es Salaam jana,  Katibu Mkuu wa UVCCM, Martine Shigela, alisema kuwa wana wasiwasi na mafunzo yatakayotolewa na Chadema, yatakuwa na ‘sura ya kigaidi’ kwa vile yatafanyika kwa siri.

 “Tunalaani  vikali mafunzo hayo, hayana tija yoyote kwa jamii yeyote,” alisema Shigela.

Kwa mujibu wa Shigela, UVCCM haifanyi kazi za ulinzi kama `red brigade’ badala yake wanaangalia ni jinsi gani vijana wanaboreshewa huduma mbalimbali za kijamii kupitia siasa.

WAISEMEA KATIBA MPYA
Shigela aliipongeza rasimu ya Katiba Mpya kupitia Mwenyekiti wake, Jaji Joseph Warioba, kwa kuwaandaa wabunge wenye umri mdogo, tofauti na ilivyokuwa awali.

“Rasimu ya Katiba Mpya inaainisha kwamba wagombea nafasi za ubunge wanatakiwa kuwa na umri wa miaka 21 hadi 25,ila awe anakidhi kiwango na sifa za ubunge, hili ni jambo jema”, alisema.

Monday, June 3, 2013

HOTUBA YOTE YA TUME YA MABADILIKO YA KATIBA

03HOTUBA YA MWENYEKITI WA TUME YA MABADILIKO YA KATIBA, JAJI JOSEPH S. WARIOBA, KATIKA MKUTANO WA WAANDISHI WA HABARI KUHUSU UZINDUZI WA RASIMU YA KATIBA TAREHE 03 JUNI, 2013 KWENYE VIWANJA VYA UKUMBI WA KARIMJEE,
DAR ES SALAAM.
04
  • Mhe. Dkt Mohammed Gharib Bilali – Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano,
  • Mhe. Mizengo K. P. Pinda (Mb.) - Waziri Mkuu,
  • Mhe. Seif Sharif Hamad – Makamu wa Kwanza wa Rais – Serikali ya Mapinduzi Zanzibar,
  • Mhe. Balozi Seif Ali Iddi (Mb.) - Makamo wa Pili wa Rais - Serikali ya Mapinduzi Zanzibar,
  • Mhe. Mathias Chikawe – Waziri wa Katiba na Sheria,
  • Mhe. Abubakar Khamis Bakary - Waziri wa Katiba na Sheria wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar,
  • Mhe. Jaji Frederick M Werema - Mwanasheria Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,
  • Mhe. Othman Masoud Othuman - Mwanasheria Mkuu wa Zanzibar,
  • Viongozi wa Vyama vya Siasa,
  • Waheshimiwa Wajumbe wa Tume na Wajumbe wa Sekretarieti ya Tume ya Mabadiliko ya Katiba,
  • Ndugu Wananchi,
  • Wageni Waalikwa
  • Waandishi wa Habari Mabibi na Mabwana.



  1. UTANGULIZI

Ndugu Wananchi,
Awali ya yote namshukuru mwenyezi mungu kwa kutuwezesha kufikia hatua hii ya leo ya kuzindua Rasimu ya Katiba. pia, niwashukuru ninyi nyote mliohudhuria halfa hii ikiwa ni mwendelezo wa mchakato muhimu wa Mabadiliko ya Katiba ya nchi yetu.

Sunday, June 2, 2013

KONGAMANO LA WAISILAMU JIJINI DAR, Sheikh Ponda aunguruma, Awasihi waisilamu kuwa na umoja, Nuru inakaribia.



Waumini wa dini ya Kiisilamu wakiwa kwenye Kongamano lililofanyika leo jijini Dar es Saalaam kwenye ukumbi wa Diamond Jubilee ambapo mada mbalimbali ziliwasilishwa na masheikh. Msimamo wa waisilamu juu ya Maendeleo ya mchakato wa katiba mpya, Dhulma na uonevu dhidi ya waisilamu pamoja na hatua za kuchukuwa kama madai yao yatapuuzwa.      
Hivi ndivyo Diamod ilivyofurika.
Waisilamu wa Rika na jinsi zote walikuwepo.
Imamu wa Msikiti wa Mtambani Imam Suleiman akimkaribisha Sheikh Ponda kuhutubia waisilamu kwenye Kongamano hilo.
Takibirrrrr zikafuatia baada ya kukaribishwa Sheikh Ponda.
Sheikh Konda Juma Bungo nae aliwasilisha mada.
Sheikh Ponda Issa Ponda  (kushoto) akihutubia waisilamu kwenye kongamano hilo.
Sheikh Ally Basaleh nae hakusita kuwaambia serikali kuwa kwenye daladala waliopanda watanzania kuna watu wamevaa ndala na kuna wengine wamevaa buti wenye ndala wanakanyagwa ndio maana wanasema! Kwahiyo badala ya kufanya hasira na kuchukua maamuzi ya nguvu bora wawasikilize wanaosema wanakanyagwa.
Amiri wa Jumuia na Taasisi za Kiisilamu Tanzania Sheikh Musa Kundecha nae aliwaambia waisilamu kuwa kwa kawaida mtu akilala ukimwamsha huamka lakini ukimwona amelala una mwamsha na haamki basi ujue hajalala ila anajifanya amelala dawayake ni kumkera mpaka aamke.
Jopo la Masheikh wa Meza kuu
           Na Mwandishi Maalum.
WAISILAM leo wametoa msimamo juu ya masuala mbalimbali yanayoendelea nchini wakati wa kongamano lililoandaliwa na jumuiya na Taasisi za Kiisilamu Tanzania jijini Dar es Salaam.
Kwenye kongamano hilo ambalo masheikh mbalimbali wakiwemo Sheikh Ponda Issa Ponda, Ally Basaleh, Mussa Kundecha na Kondo Juma Bungo waliwasilisha mada mbalimbali pamoja na kutangaza maazimio ya kongamano hilo.
Moja ya mambo yaliyozungumzwa ni mapendekezo waliyowasilisha kwenye Tume ya katiba mpya ambapo walisema iwapo mapendekezo waliyowasilishwa hayakuzingatiwa na kutupwa yote basi waisilamu watatangaza kusimamisha mchakato huo nchi nzima na kufanya maandamano usiku na mchana.
Hoja hiyo ilikuja baada ya kunukuliwa kauli ya Waziri wa nchi Sera na Uratibu wa bunge Wiliam Lukuvi, wakati akijibu swali la Mbunge Asumta Mshama aliyetaka kujua kwamba lini serikali itaacha kupanga siku ya kupiga kura kuwa Jumapili wakati wanajua siku hiyo ni siku ya ibada ya wakristo haioni inawadhulumu hakiyao yakufanya ibada?, Lukuvi kwenye jibu lake alisema suala hilo limekuwa likilalamikiwa na watu wengi tu lakini serikali kwenye hilo haina utaratibu maalum wa siku ya kupiga kura ila kwakuwa kuna mchakato wa katiba mpya hilo litazingatiwa.
“Hii ni kinyume kabisa na utaratibu wa tume ya katiba waziri huyu anataka tuamini kwamba  anayafahamu yatakayokuwemo kwenye katiba mpya kabra hata wananchi hawajapelekewa na hata haijaandikwa? Hivyo iweje waisilamu wanaodai siku ya ijumaa iwe ya mapimziko kwa miaka nenda rudi hawapewi wakristo wanakosa sikumoja tu ndani ya miaka mitano majibu yanapatikana kirahisi?” Alihoji sheikh Ponda.
“W aisilamu wamekuwa wakiomba ruhusa kwa mabosi wao siku ya ijumaa kwenda kufanya ibada na mara nyingine wananyimwa ruhusa hiyo lakini hakuna vurugu yeyote waliofanya na wanadai haki hiyo kwa miaka yote hii lakini hawapewi lakini wengine wanadai kirahisi na kujibiwa kwa uhakika.” Alifafanua.
Aidha heikh Ponda alifafanua kuwa waisilamu wavumilie wasubiri rasimu itakapotangazwa kwenye magazeti ya serikali kama mapendekezo waliyowasilishwa yatapuuzwa basi hakuna katiba mpya maandamano usiku na mchana mpaka kieleweke nchi nzima.
Sheikh Ally Basaleh alisihi Serikali kuwasikiliza waisilamu hoja zao wasiwapuuze.

MWILI WA MAREHEMU ALBERT MANGWEA HAUTAWEZA KUFIKA LEO JUMAPILI



Kamati ya msiba tunaomba kutoa taarifa kwamba mwili wa marehemu ndugu yetu Albert Mangwair hautafika siku ya Jumapili ya tarehe 02/06/2013 kama ilivyokuwa imepangwa hapo awali,hii ni kutokana na sababu zilizo nje ya uwezo wetu.
Kwa sasa tunasubiri taarifa kamili kutoka kwa wawakilishi 
waliopo Afika Kusini,maratutakapopata taarifa hizo tutawafahamisha zaidi.
Tunaomba radhi kwa watanzania wote kwa usumbufu wote uliojitokeza..tuendelee kuvumilia

 

Friday, May 24, 2013

Fezza Kessy likely to represent Tanzania on Big Brother Africa 8

In Tanzania here are some of the likely faces that might hit our screens in the eighth edition of Big Brother Africa. These names were chosen basing on the fact of one’s  ability  to speak English fluently and their passion for reality TV.
Multichoice recently announced call for entries from applicant s willing to take part in Big Brother Africa 8 competition to apply  both online or obtain hard copy application forms  Starting February 1, the forms will be vailable in all  multichoice offices of the participating countries, including Tanzania
download (1)
Feza Kessy, Nisha, Shaa and Lisa Jensen,
Most of the Tanzania hopefuls have been in showbiz circles and willing to use the Big Brother Africa platform to show case their unique character and talent. Who would you recommend for the show.

Sunday, May 19, 2013

Rais Jakaya Kikwete Akutana Kwa Mazungumzo na Askofu Mkuu wa Canterbury Justin Portal Welby katika ukumbi wa St.Gaspar mjini Dodoma


 Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akiwa katika mazungumzo na Askofu Mkuu wa Canterbury Justin Portal Welby katika ukumbi wa St.Gaspar mjini Dodoma jana
Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akiagana na Askofu Mkuu wa Canterbury Justin Portal Welby muda mfupi baada ya kufanya naye  mazungumzo katika ukumbi wa St.Gaspar mjini Dodoma jana.Askofu huyo alishiriki katika ibada ya kutawazwa kwa askofu mkuu mpya wa Kanisa la Anglikana nchini Tanzania Dkt.Jacob Erasto Chimeledya.Picha na Freddy Maro-IKULU

Friday, May 17, 2013

Rais Barack Obama Kutembelea Tanzania Mwezi ujao



 

 President Barack Obama greets children upon his arrival to Miami International Airport in Miami, Friday, March, 4, 2011. (AP Photo/Pablo Martinez Monsivais) 



Rais Barack Obama
 
Rais Barack Obama wa Marekani anatarajia kuanza ziara yake ya pili katika bara la Afrika mwishoni wa mwezi June, ziara ambayo itamfikisha Africa ya Kusini, Tanzania na Rwanda.
Katika ziara yake hiyo, atapitia Nigeria na kuongea na rais Goodluck Jonathan pamoja na waandamizi wa serikali ya Nigeria.
 Mpango wa awali ulikuwa kwamba rais Obama angetembelea Nigeria kwa siku mbili lakini kutokana na hofu ya usalama kutoka kwa magaidi wa Boko Haram Nigeria inaonekana kwamba itashindwa kutoa ulinzi wa kutosha wa rais huyo wa Marekani hivyo atalazimika kukaa Nigeria kwa muda mchache.
Habari kutoka Ikului ya White House zinadokeza kuwa usalama utazingatiwa sana katika ziara hiyo na kama kutakuwa na sababu yeyote ya kuwa na wasiwasi juu ya usalama wa Rais Obama basi ziara hiyo itakatizwa wakati wowote katika nchi ya Nigeria.
Mwaka 2009 Obama alitembelea Africa na alichagua nchi ya Ghana ambapo alikutana na Raisi (marehemu) John Atta mills, na akatoa hotuba katiba bunge la Ghana na kisha kutembelea Cape Coast Castle sehemu ambapo watumwa wa Trans Atlantic walikuwa wanapakiliwa kupelekwa Marekani wakati wa biashara ya utumwa.
Kwa sis watanzania, ziara hii ya kiongozi mkubwa duniani ina manufaa gani kibiashara, kiuchumi, kiusalama? Kuna fursa gani kwa Watanzania kama ilivyoluwa kwa Rais wa China? Ni matumaini yetu kuwa ziara hii itazidi kuliweka Taifa letu katika sura nzuri kimataifa na kitaifa. Ikumbukwe kwamba, Marais wa nchi kubwa kama Marekani wanachagua kutembelea nchi zile zinazofanya vizuri katika utawala bora, demokrasia madhubuti, uhuru wa haki za binadamu, uhuru wa vyombo vya habari, kusimamia na kutimiza vyema malengo ya millenium..... Hivyo kwa Tanzania kupata ugeni kama huu ni ishara nzuri na chachu ya kuendelea kufanya vizuri zaidi. Mungu Ibariki Tanzania
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...