ADV

ADV

ADVERTISEMENT CORNER

HUDUMA YA KUKATA TICKET ZA NDEGE ONLINE


SOMA HABARI

SOMA HABARI
Showing posts with label Padre Anselmo Mwangamba. Show all posts
Showing posts with label Padre Anselmo Mwangamba. Show all posts

Tuesday, September 17, 2013

‘Nilimwona aliyenimwagia tindikali’

padri_c4893.png
Paroko wa Parokia ya Roho Mtakatifu Cheju Zanzibar, akisaidiwa na Frateri, Richard Haki kupumzika kitandani baada ya kuzungumza na waandishi katika katika Wodi ya Kibasila iliyopo katika Hosipitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH) jijni Dar es Salaam jana.Picha Salim Shao
Padri wa Parokia ya Cheju ya Kanisa Katoliki Zanzibar, Anselmo Mwang'amba amesema kuwa alimwona mtu aliyemwagia tindikali na kumsababishia majeraha na kueleza kuwa anashangaa kuona polisi hawajamkamata hadi sasa.
Akizungumza jana katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili, kwenye Wodi namba 16, Kibasila alipolazwa, Padri Mwang'amba alisema baada ya kumwagiwa tindikali, alimwona mtu huyo akikimbia kuelekea katika nyumba moja jirani.(P.T)

"Kwa kuwa mimi nilikuwa na taharuki na maumivu, sikuweza kuendelea kumfuatilia, ila dereva aliyenikimbilia kunipa msaada aliniambia kwamba alimwona mhusika akikatiza kwenye uchochoro hadi alipoingia kujificha kwenye nyumba iliyopo jirani na eneo hilo," alisema.
Alisema majeraha aliyoyapata wakati akitokea katika duka la huduma za mawasiliano ya mtandao la Shine Shine saa 10.15 jioni, ambayo yanamsababishia maumivu makali, hayawezi kumfanya aikimbie Zanzibar, kwa kuwa hata Yesu Kristo wakati alipokuwa katika kazi za utumishi duniani alipata mateso makali kuliko yake.
"Nilisomea upadri nikiwa Zanzibar kuanzia mwaka 1976 hadi mwaka 1981 nilipopata upadrisho kamili. Niko huko kwa kazi ya Mungu wala si mwanadamu, kwa hiyo nikitoka hapa narejea hukohuko, siogopi, ingawa miaka hiyo nilipokuwa naanza kazi hii hakukuwa na mambo kama haya," alisema.
Aliwataka Wakristo wanaoishi Zanzibar kuendelea kuwa na umoja na upendo pamoja na kuwa makini kwa usalama wao licha ya matukio magumu yanayowakuta ikiwamo vitisho na kuchomwa moto kwa makanisa.
Pia aliunga mkono shinikizo la kutimuliwa kazi kwa Kamishna wa Polisi wa Zanzibar, Mussa Ali Mussa kutokana na kushindwa kuwakamata watu wanaomwagia watu tindikali.
"Huyu bwana alishindwa hata kunijulia hali wakati nikiwa hospitali huko Zanzibar, tofauti na nilipokuja Bara ambako Inspekta Jenerali wa Polisi, Said Mwema na Kamanda wa Polisi wa Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Suleiman Kova walifika kunijulia hali na kuzungumza nami hospitali.
"Kwa hali hii, naona kwamba tukio langu ni la kupangwa na litazungumzwa sana lakini baada ya muda halitashughulikiwa. Atajeruhiwa mwingine tena lakini hatua za dhati za kudhibiti ukatili huu usiendelee hazijachukuliwa. Mimi ni padri wa tatu kufanyiwa ukatili," alisema.
Mapadri wengine ni Ambros Mkenda aliyepigwa risasi na kujeruhiwa wakati Padri Evarist Mushi aliuawa kwa kupigwa risasi.
Chanzo:mwananchi

Friday, September 13, 2013

Majanga yaendelea kuwakumba Mapadre wa Kanisa Katoliki huko Zanzibar




Padri wa kanisa Katoliki Parokia ya Cheju Zanzibar, Joseph Mwangamba mara baada ya kumwagiwa tindikali
 
 
Padri Anselmo Mwang'amba akiwa kitandani kwenye wodi ya Mapinduzi Mpya, hospitali ya Mnazi mmoja mjini Zanzibar, Padri Mwang'amba alimwagiwa tindikali. Padri Anselmo Mwang'amba wa Kanisa Katoliki Parokia ya Mpendae Jimbo la Zanzibar leo katika eneo la Mlandege mjini Zanzibar majira ya saa 10 jioni.
  
ZANZIBAR, Tanzania
PADRI wa Kanisa Katoliki, Parokiya ya Cheju Anselmo Mwan'gamba amemwagiwa tindikali usoni na watu wasiojulikana wakati akitoka kupata huduma za mawasiliano ya Intaneti, eneo la Mlandege. 

Kamanda wa Polisi mkoa wa mjini Magharibi Unguja, Mkadam Khamis  alithibitisha kutokea kwa tukio hilo ambapo alisema uchunguzi wa kina umeanza.
'Tumepokea taarifa ya tukio lakini uchunguzi wa tukio hilo na kujuwa chanzo na mtandao wa wahalifu hawa umeanza'alisema.
Kwa mujibu wa taarifa za daktari wa hospitali ya Mnazi mmoja ambaye alimpokea padri huyo kwa ajili ya kupata matibabu ya kwanza Abdalla Haidari alisema ameumia sehemu ya uso pamoja na kifua.

'Padri Mwan'gamba amejeruhiwa na maji ambayo baada ya kuyafanyia uchunguzi tumegundua kuwa ni tindikali katika sehemu za uso na kifua'alisema.

Kwa mujibu wa maelezo ya padri Mwan'gamba alisema alishambuliwa na watu ambao hawafahamu wakati akitoka katika duka linalotoa huduma za mtandao wa mawasiliano ya Intaneti hapo Sunshine Mlandege katika majira ya jioni saa kumi.

'Wakati natoka katika duka la kupata huduma za mawasiliano ya Intenate nilimwagiwa maji makali ambayo nilihisi kwamba ni tindikali na kuamuwa kwenda moja kwa moja katika hospitali ya Mnazi mmoja'alisema.
Mfanyakazi mmoja wa duka linalotoa huduma za mawasiliano ya Intenate aliyejitambulisha kwa jina la Salma alikiri kutokea kwa tukio hilo ambapo mteja wake alipata huduma hapo. "Wakati anatoka baada ya kupata huduma mara namuona anarudi na kulalamika kwamba amemwagiwa tindikali katika sehemu za uso" alisema.

Hilo ni tukio la tano kwa watu mbali mbali kumwagiwa tindikali mjini hapa ambapo hadi sasa hakuna mtu aliyekamatwa kuhusika na ukatili huo. Padri Mwangamba ni mkuu wa kituo cha malezi cha vijana kiliopo Cheju mkoa wa kusini Unguja ambacho hutunza vijana kwa ajili ya kuwapatia mafunzo mbali mbali.
 
 
BBC
Polisi huko visiwani Zanzibar wanachunguza tukio la kasisi wa kanisa katoliki kushambuliwa kwa tindikali.
Imeelezwa kuwa Kasisi huyo Anselmo Mwang'amba, alimwagiwa tindikali akitoka mgahawa mmoja wa kutumia mtandao mjini Zanzibar. Tukio hilo linatokea ndani ya mwezi mmoja tangu wasichana wawili wa kiingereza kushambuliwa.
Hili ni janga jingine kwa Zanzibar ambayo imekuwa ikizongwa na matukio ya aina hii kwa muda sasa.
Mkurugenzi wa upelelezi wa Zanzibar, Yusufu Ilembo ameieleza BBC kuwa bado hawajakamata mtu yoyote kuhusika na tukio hilo ingawa amethibitisha kuwa uchunguzi tayari umeanza.
Ameeleza kuwa Kasisi Mwang'amba aliungua usoni na mabegani na kwamba anaendelea kutibiwa.
Katika miaka ya karibuni Zanzibar imekabiliwa na mikasa ya watu kushambuliwa hivi na kuzua hisia kuwa chuki za kidini.
Mapema mwaka huu kasisi mwingine wa kanisa katoliki alishambuliwa kwa risasi na kuuawa.
Mwezi uliopita Zanzibar ilitikisika kutokana na wasichana wawili wangereza kushambuliwa kwa tindikali na watu wasiojulikana.
Kiongozi mmoja wa dini ya kiislamu pia alimwagiwa tindikali na watu wasiojulikana.
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...