Padri Anselmo Mwang'amba akiwa
kitandani kwenye wodi ya Mapinduzi Mpya, hospitali ya Mnazi mmoja mjini
Zanzibar, Padri Mwang'amba alimwagiwa tindikali. Padri Anselmo
Mwang'amba wa Kanisa Katoliki Parokia ya Mpendae Jimbo la Zanzibar leo
katika eneo la Mlandege mjini Zanzibar majira ya saa 10 jioni.
ZANZIBAR, Tanzania
PADRI wa Kanisa Katoliki, Parokiya
ya Cheju Anselmo Mwan'gamba amemwagiwa tindikali usoni na watu
wasiojulikana wakati akitoka kupata huduma za mawasiliano ya Intaneti,
eneo la Mlandege.
Kamanda wa Polisi mkoa wa mjini Magharibi Unguja, Mkadam Khamis alithibitisha kutokea kwa tukio hilo ambapo alisema uchunguzi wa kina umeanza. 'Tumepokea taarifa ya tukio lakini uchunguzi wa tukio hilo na kujuwa chanzo na mtandao wa wahalifu hawa umeanza'alisema.

Kwa mujibu wa taarifa za daktari
wa hospitali ya Mnazi mmoja ambaye alimpokea padri huyo kwa ajili ya
kupata matibabu ya kwanza Abdalla Haidari alisema ameumia sehemu ya uso
pamoja na kifua.
'Padri Mwan'gamba amejeruhiwa na maji ambayo baada ya kuyafanyia uchunguzi tumegundua kuwa ni tindikali katika sehemu za uso na kifua'alisema.
Kwa mujibu wa maelezo ya padri Mwan'gamba alisema alishambuliwa na watu ambao hawafahamu wakati akitoka katika duka linalotoa huduma za mtandao wa mawasiliano ya Intaneti hapo Sunshine Mlandege katika majira ya jioni saa kumi.
'Wakati natoka katika duka la kupata huduma za mawasiliano ya Intenate nilimwagiwa maji makali ambayo nilihisi kwamba ni tindikali na kuamuwa kwenda moja kwa moja katika hospitali ya Mnazi mmoja'alisema.
Mfanyakazi mmoja wa duka linalotoa huduma za mawasiliano ya Intenate aliyejitambulisha kwa jina la Salma alikiri kutokea kwa tukio hilo ambapo mteja wake alipata huduma hapo. "Wakati anatoka baada ya kupata huduma mara namuona anarudi na kulalamika kwamba amemwagiwa tindikali katika sehemu za uso" alisema.
Hilo ni tukio la tano kwa watu mbali mbali kumwagiwa tindikali mjini hapa ambapo hadi sasa hakuna mtu aliyekamatwa kuhusika na ukatili huo. Padri Mwangamba ni mkuu wa kituo cha malezi cha vijana kiliopo Cheju mkoa wa kusini Unguja ambacho hutunza vijana kwa ajili ya kuwapatia mafunzo mbali mbali.

BBC
Hili ni janga jingine kwa Zanzibar ambayo imekuwa ikizongwa na matukio ya aina hii kwa muda sasa.
Mkurugenzi wa upelelezi wa Zanzibar, Yusufu Ilembo ameieleza BBC kuwa bado hawajakamata mtu yoyote kuhusika na tukio hilo ingawa amethibitisha kuwa uchunguzi tayari umeanza.
Ameeleza kuwa Kasisi Mwang'amba aliungua usoni na mabegani na kwamba anaendelea kutibiwa.
Katika miaka ya karibuni Zanzibar imekabiliwa na mikasa ya watu kushambuliwa hivi na kuzua hisia kuwa chuki za kidini.
Mapema mwaka huu kasisi mwingine wa kanisa katoliki alishambuliwa kwa risasi na kuuawa.
Mwezi uliopita Zanzibar ilitikisika kutokana na wasichana wawili wangereza kushambuliwa kwa tindikali na watu wasiojulikana.
Kiongozi mmoja wa dini ya kiislamu pia alimwagiwa tindikali na watu wasiojulikana.
Polisi huko visiwani Zanzibar wanachunguza tukio la kasisi wa kanisa katoliki kushambuliwa kwa tindikali.
Imeelezwa kuwa Kasisi huyo Anselmo Mwang'amba,
alimwagiwa tindikali akitoka mgahawa mmoja wa kutumia mtandao mjini
Zanzibar. Tukio hilo linatokea ndani ya mwezi mmoja tangu wasichana
wawili wa kiingereza kushambuliwa.Hili ni janga jingine kwa Zanzibar ambayo imekuwa ikizongwa na matukio ya aina hii kwa muda sasa.
Mkurugenzi wa upelelezi wa Zanzibar, Yusufu Ilembo ameieleza BBC kuwa bado hawajakamata mtu yoyote kuhusika na tukio hilo ingawa amethibitisha kuwa uchunguzi tayari umeanza.
Ameeleza kuwa Kasisi Mwang'amba aliungua usoni na mabegani na kwamba anaendelea kutibiwa.
Katika miaka ya karibuni Zanzibar imekabiliwa na mikasa ya watu kushambuliwa hivi na kuzua hisia kuwa chuki za kidini.
Mapema mwaka huu kasisi mwingine wa kanisa katoliki alishambuliwa kwa risasi na kuuawa.
Mwezi uliopita Zanzibar ilitikisika kutokana na wasichana wawili wangereza kushambuliwa kwa tindikali na watu wasiojulikana.
Kiongozi mmoja wa dini ya kiislamu pia alimwagiwa tindikali na watu wasiojulikana.
No comments:
Post a Comment