ADV

ADV

ADVERTISEMENT CORNER

HUDUMA YA KUKATA TICKET ZA NDEGE ONLINE


SOMA HABARI

SOMA HABARI
Showing posts with label TFF. Show all posts
Showing posts with label TFF. Show all posts

Sunday, May 11, 2014

Real Madrid kucheza mechi ya kirafiki na nyota wa Tanzania Agost 21


KIKOSI cha wachezaji wakongwe wa timu ya Real Madrid kutoka Hispania kinatarajia kuja nchini kucheza mechi ya kirafiki na nyota wa soka wa Tanzania mchezo utakaofanyika Agosti 23 kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.
Ofisa Habari wa kampuni ya TSN, Dennis Ssebo, alisema kuwa kikosi wawakilishi kutoka Real Madrid ‘Legend Team’.
Timu hiyo ya Real Madrid Legend iliwakilishwa na Mchezaji Mkongwe na kapteni wa timu hiyo Ruben de la Red alieambatana na mchezaji mwingine mkongwe Rayo Garcia pamoja na Isaac Recarey Sanchez anaehusika na maswala ya mahusiano ya Real Madrid Legend Club.
Mwakilishi wa Real Madrid Legends Team, Ruben de la Red kulia akibadilishana nakala za mikataba ya ziara ya timu hiyo nchini leo na Mkurugenzi wa TSN Group, Farough Baghoza katika Mkutano na Waandishi wa Habari ukumbi wa Kivukoni 4, hoteli ya Serena, Dar es Salaam.

Akizungumza na wana habari mwakilishi huyo wa TSN alisema timu hiyo itawakilishwa na wachezaji 25. Wanatazamiwa kuja kwa siku tatu wakiwa na ratiba mbali mbali. ‘Nje ya mechi ya kirafiki na timu yetu ya Taifa, wachezaji hawa wakongwe ambao bado wako fiti na wanacheza wanatazamia kutembelea mbuga za wanyama kwa minajili ya kuendelea kutangaza utalii wa Tanzania.’ Ratiba ya timu hiyo ni kama ifwatayo:
Naye mwakilishi na kepteni wa timu ya Real Madrid Legend aliishukuru kampuni ya TSN kwa kuwapa nafasi ya kuja kuona Tanzania. Wanatambua nchi ya Tanzania ni moja ya nchi yenye washabiki wa Soka wengi sana na ana amini mechi yao na vijana wa Tanzania itakua kali na mashabiki watakaohudhuria watafurahia. Pia aliwashauri vijana wa timu ya Tanzania kujifua maana yaweza kuwa hawachezi tena kila siku lakini bado wako fiti na wembe mkali.
Rais wa Shirikisho la Soka nchini (TFF) bwana  Jamal Malinzi aliipongeza kampuni ya TSN kwa hatua hii nzuri itakayoongeza tija kwa soka nchini, machoni mwa ulimwengu wa soka duniani na kuahidi kutoa ushirikiano kamili kwa TSN kwa ujio huu. “TSN wamefanya jambo la busara sana kwa soka nchini. Ujio wa timu hii utatupa mafunzo mengi na uzoefu walionao wachezaji hawa lakini pia watasaidia kuitangaza nchi kwa ujumla. TFF inaahidi kutoa ushirikiano kamili kwa TSN ili kufanikisha ziara hii”.
TSN imesaini mkataba na wawakilishi wa Real Madrid leo katika hoteli ya Serena. Kwa upande wa TSN Mkurugenzi Mtendaji wa makampuni hayo Ndugu Farough Baghoza alitia saini kwenye mkataba huo na kapteni wa timu hiyo Ruben De La Red alisaini kwa niaba ya Real Madrid Legends Club.

Saturday, June 8, 2013

TAIFA STARS WAFANYIWA 'UMAFIA' MOROCCO,WALIPOTAKA KUFANYA MAZOEZI UWANJANI

 

Na Mahmlud Zubeiry, Marakech, IMEWEKWA JUNI 8, 2013 SAA 8:00 USIKUTIMU ya soka ya taifa ya Tanzania, Taifa Stars usiku huu imekiona cha moto mbele ya askari wa Uwanja wa Marakech, baada ya kufanyiwa vurugu na kuzimiwa taa ishindwe kufanya mazoezi kwenye Uwanja huo siku moja kabla ya mchezo wao na wenyeji wao Morocco kesho, kuwania tiketi ya kucheza Fainali za Kombe la Dunia. Sheria za FIFA zinasema timu mgeni, itapewa fursa ya kufanya mazoezi katika Uwanja utakaotumika kwa mechi dhidi ya wenyeji katika muda ambao mechi itachezwa, lakini leo msafara wa Stars ulipofika Uwanja wa Marakech ulizuiwa kuingia ndani na askari wa uwanjani hapo. Juhudi za Kocha mkuu wa Stars, Kim Poulsen kuwaelewesha askari wa Uwanja huo sheria ili wairuhusu timu kuingia uwanjani hazikuzaa matunda na ikabidi viongozi wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) waingilie kati, nao pia wakachemsha.
Thomas Ulimwengu kulia nje ya geti, askari kushoto
Dk Dau getini
Mtanzania anaruka geti ili kufungua mlango Stars ikafanye mazoezi
Baadhi ya wachezaji wa Stars, kutoka kulia Juma Kaseja, Amri Kiemba, Mrisho Ngassa na Salum Abubakar baada ya kuingia uwanjani
Kutoka kulia Mwinyi Kazimoto, Athumani Iddi 'Chuji' na Kevin Yondan
Crescentius Magori kushoto akishuhudia marefa wa mchezo huo wakikagua pasipoti za wachezaji wa Stars
Wasiwasi; Kutoka kulia DK Dau, Mh Zitto Kabwe, Mh Mohamed Dewji na Magori wakijadiliana uwanjani
Ikawadia zamu ya viongozi wa Kamati ya Ushindi ya Stars, inayodhaminiwa na Kilimanjaro Premum Lager, ambao nao walichemsha- ndipo baadhi wa Watanzania waishio hapa na wachache waliosafiri kutoka Dar es Salaam walipoongeza nguvu.Walikwenda kufungua geti kwa nguvu, wakawaweka kando askari waliokuwa wanawazuia na kuiingiza timu uwanjani kufanya mazoezi. Hata hivyo, Stars ilipofika uwanjani ililazimika kusubiri tena, kwani wenyeji Simba wa Atlasi walikuwa wakiendelea na mazoezi.Baada ya nusu saa, Morocco walimaliza awamu yao na Stars wakaanza kupasha misuli moto. Hata hivyo, baada ya dakika 34, taa za Uwanja huo zilizimwa na uwanjani kuwa giza totoro, lakini viongozi wa TFF wakaenda kuomba, zikawashwa na timu ikafanya mazoezi kwa dakika 10 zaidi. Naibu Waziri wa Habari Utamaduni na Michezo, Mh. Amos Makalla aliyekuwapo wakati wa vurumai zote hizo, alisikitishwa mno na kitendo hicho akisema si cha kiungwana na si cha kiunamichezo.
Makipa mazoezini; Juma Kaseja amedaka, Ally Mustafa 'Barthez' anamshuhudia kushoto
Shomary Kapombe anayeteleza, Erasto Nyoni akipitisha mpira
Mtanzania amemdhibiti askari wachezaji waingie uwanjani
Watanzania wamefanikiwa kufungua geti
Ahmad Mgoyi wa TFF akipambana na askari kufungua geti 
Mpambano, Kim Poulsen na askari, nyuma ni Mgoyi 
Makamu wa Rais wa TFF, Athumani Nyamlani alisema Morocco walikuja kucheza Dar es Salaam walipokewa vizuri na wakahudumiwa vizuri hadi wanaondoka, ajabu leo wanaifanyia ‘unyama’ Tanzania.Mkuu wa Msafara wa Stars hapa, Crescentius John Magori alisema watapeleka malalamiko FIFA, waandaji wa michuano ya kufuzu kwa Kombe la Dunia na kwa kuwa ushahidi upo, anaamini Morocco watachukuliwa hatua.Mwenyekiti wa Kamati ya Usajili ya Simba SC, Zacharia Hans Poppe alishauri Stars icheze chini ya angalizo kwa kuwasilisha barua FIFA mapema ili wakae wanajua kuhusu hali halisi Morocco.Kwa ujumla kilichotokea leo kimewatia woga Watanzania wengi waliopo hapa kuelekea mchezo wa kesho, ambao Stars inahitaji ushindi ili kujiimarisha katika mbio za kuelekea Brazil 2014. Hata ulinzi wa msafara wa Stars kutoka hotelini hadi uwanjani hakuwa wa kutosha na ilishuhuidiwa mara kadhaa ukiingiliwa na magari mengine barabarani wakati timu ikienda uwanjani kwa mazoezi.Wenyeji nchini Morocco wanasema inapowadia mechi, huwa wanaogopa kwa sababu mara nyingi hutokea vurugu ya damu kumwagika.Kwa ujumla Stars inaingia katika mchezo wa kesho katika hali ya wasiwasi na woga mkubwa. Stars itashuka dimbani saa 3:00 usiku kesho kwa saa za hapa sawa na saa 5:00 za Tanzania kucheza na Morocco.Stars inashika nafasi ya pili katika Kundi C, ikiwa na pointi sita nyuma ya Ivory Coast yenye pointi saba, ambayo kesho itakuwa ugenini ikimenyana na Gambia katika mchezo mwingine wa kundi hilo.
Mrisho Ngassa anamiliki mpira
Thomas Ulimwengu anakwenda
Mbwana Samatta kulia na mpira
Wachezaji Stars Uwanja wa Marekch
Stars ilitua hapa Jumatatu ikitokea Ethiopia ambako iliweka kambi ya wiki moja na kucheza mchezo wa kirafiki dhidi ya Sudan, ulioisha kwa sare ya bila mabao.Kabla ya kuja hapa, Stars iliweka kambi ya wiki moja katika hoteli ya Tansoma, Dar es Salaam ikijifua Uwanja wa Karume na siku chache kabla ya kuondoka ilialikwa Ikulu na Rais Jakaya Kikwete, aliyewapa hamasa kwa hotuba nzuri.

Thursday, May 23, 2013

KIKWETE AKUTANA NA WACHEZAJI WA TIMU YA TAIFA IKULU JIJINI DAR



Rais Jakaya Kikwete akiwaaga wachezaji wa Timu ya Taifa Stars Nadir Haroub 'Canavaro' baada ya kukutana nao leo Ikulu Jijini Dar es salaam na kuwahamasisha washinde mchezo dhidi ya timu ya Taifa ya Moroco utakaochezwa Juni 7 mwaka huu, ikiwa ni sehemu ya Taifa Stars kutafuta ticketi ya kucheza mashindano ya Kombe la Dunia.
Meneja wa Timu ya Taifa Stars, Tasso Mukebezi, akiteta jambo na Nahodha wa Timu ya Taifa Stars, Juma Kaseja, Ikulu jijini Dar es salaam walipokutana na Rais Jakaya Kikwete leo mchana.
Rais Jakaya Kikwete akiwa katika Picha ya Pamoja na wachezaji wa Timu ya Taifa , Taifa Stars, viongozi wa Wizara ya Habari, Vijana ,Utamaduni na Michezo na Viongozi wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF).
Rais Jakaya Kikwete akiwa katika Picha ya pamoja na wachezaji wa timu ya Taifa , Taifa Stars Ikulu jijini Dar es salaam. Picha na Aron Msigwa – MAELEZO.
***************************************************
Rais Jakaya Kikwete, akizungumza na wachezaji wa timu ya Taifa, Taifa Stars leo Ikulu jijini Dar es salaam, alipokutana nao na kuwapa hamasa waweze kupata ushindi katika mchezo wao dhidi ya Moroco utakaochezwa Juni 7, na michezo mingine ikiwa ni hatua ya kuiwezesha timu hiyo kukata tiketi ya kushiriki mashindano ya kombe la dunia mwaka 2014.
***************************************
Na. Veronica Kazimoto –MAELEZO.
Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete leo amekutana na timu ya Taifa (Taifa stars) kwa lengo la kuitia moyo katika mechi ijayo kati yake na timu ya Moroco ikiwa ni harakati za Tanzania kutafuta tiketi ya kucheza fainali za kombe la Dunia kwa mara ya kwanza mwaka 2014.

Rais Kikwete ameiambia timu hiyo kuwa ina uwezo mkubwa wa kusonga mbele kutokana na uwezo mkubwa waliouonesha katika mchezo wao dhidi ya Gambia ambapo walifanikiwa kupata ushindi wa bao 2-0.

“Maadamu mara ya kwanza mliwashinda Gambia, hakikisheni pia mnapata ushindi dhidi ya Moroco, mkishinda tunafurahi sana na mkishindwa tunanyong’onyea sana,” amesema Rais Kikwete.

Aidha amempongeza kocha wa timu hiyo Kim Poulsen pamoja na Kamati ya Taifa ya ushindi ya Taifa stars kwa kuisaidia timu hiyo kiasi cha shilingi milioni 30 ikiwa ni mkakati wa kuiongezea nguvu kwa hatua iliyofikia na kuwataka wachezaji kujituma ili kuwafurahisha watanzania ambao hivi sasa wanaipenda timu yao ya Taifa.

Nae Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Fenera Mukangara amesema Serikali itaendelea kushirikiana na wadau mbalimbali wa michezo nchini ili kuondoa changamoto zinazoikabili timu hiyo.

Kwa upande wake Kocha Poulsen, amemshukuru Rais Kikwete kwa kuwakaribisha na kuwatia moyo ambapo ameahidi kuifundisha vizuri timu hiyo ili kuhakikisha kuwa wanapata ushindi.

Akizungumza kwa niaba ya wachezaji wenzake kaptaini wa timu hiyo Juma Kaseja amemshukuru Rais Kikwete na kuahidi kujituma kwenye mazoezi na hatimaye kuibuka washindi kwenye mechi zijazo.

Taifa stars ambayo inakamata nafasi ya pili katika kundi C inatarajia kucheza ugenini na Morocco mnamo Juni 7 mwaka huu.
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...