ADV

ADV

ADVERTISEMENT CORNER

HUDUMA YA KUKATA TICKET ZA NDEGE ONLINE


SOMA HABARI

SOMA HABARI
Showing posts with label Jakaya Mrisho Kikwete. Show all posts
Showing posts with label Jakaya Mrisho Kikwete. Show all posts

Friday, October 4, 2013

Rais Jakaya Kikwete Azindua Uwanja wa Ndege Mafia

  Vijana wa Scout wakimvisha skafu Rais Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete muda mfupi baada ya kuwasili katika uwanja wa ndege wa Mafia jana asubuhi ambapo alifungua uwanja wa ndege wa Mafia na kuzindua Gati la Mafia.Rais Kikwete yupo katika ziara ya kikazi ya mkoa wa Pwani.

Monday, June 3, 2013

President Kikwete and former Japanese Prime Minister Yoshiro Mori speaks on Efforts to Fight Infectious Diseases


8E9U1089
A cross section of the participants to the high level panel on ““Accelerating the Global Fight against Infectious Diseases,” held as TICAD V official side event in Yokohama, Japan this morning claps as President Jakaya Mrisho Kikwete concludes his keynote address. 8E9U1096
President Dr.Jakaya Mrisho Kikwete speaks during a high level panel on “Accelerating the Global Fight against Infectious Diseases,” held as TICAD V official side event in Yokohama, Japan this morning.
 8E9U1127
President Dr.Jakaya Mrisho Kikwete and former Japan Prime Minister Yoshiro Mori shortly after they participated in a high level panel on” Accelerating the Global fight against Infectious Diseases,” held in Yokohama this morning(photos by Freddy Maro) 8E9U1142
President Dr.Jakaya Mrisho Kikwete and former Japan Prime Minister Yoshiro Mori shortly after they participated in a high level panel on” Accelerating the Global fight against Infectious Diseases,” held in Yokohama this morning(photos by Freddy Maro)

Thursday, May 23, 2013

KIKWETE AKUTANA NA WACHEZAJI WA TIMU YA TAIFA IKULU JIJINI DAR



Rais Jakaya Kikwete akiwaaga wachezaji wa Timu ya Taifa Stars Nadir Haroub 'Canavaro' baada ya kukutana nao leo Ikulu Jijini Dar es salaam na kuwahamasisha washinde mchezo dhidi ya timu ya Taifa ya Moroco utakaochezwa Juni 7 mwaka huu, ikiwa ni sehemu ya Taifa Stars kutafuta ticketi ya kucheza mashindano ya Kombe la Dunia.
Meneja wa Timu ya Taifa Stars, Tasso Mukebezi, akiteta jambo na Nahodha wa Timu ya Taifa Stars, Juma Kaseja, Ikulu jijini Dar es salaam walipokutana na Rais Jakaya Kikwete leo mchana.
Rais Jakaya Kikwete akiwa katika Picha ya Pamoja na wachezaji wa Timu ya Taifa , Taifa Stars, viongozi wa Wizara ya Habari, Vijana ,Utamaduni na Michezo na Viongozi wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF).
Rais Jakaya Kikwete akiwa katika Picha ya pamoja na wachezaji wa timu ya Taifa , Taifa Stars Ikulu jijini Dar es salaam. Picha na Aron Msigwa – MAELEZO.
***************************************************
Rais Jakaya Kikwete, akizungumza na wachezaji wa timu ya Taifa, Taifa Stars leo Ikulu jijini Dar es salaam, alipokutana nao na kuwapa hamasa waweze kupata ushindi katika mchezo wao dhidi ya Moroco utakaochezwa Juni 7, na michezo mingine ikiwa ni hatua ya kuiwezesha timu hiyo kukata tiketi ya kushiriki mashindano ya kombe la dunia mwaka 2014.
***************************************
Na. Veronica Kazimoto –MAELEZO.
Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete leo amekutana na timu ya Taifa (Taifa stars) kwa lengo la kuitia moyo katika mechi ijayo kati yake na timu ya Moroco ikiwa ni harakati za Tanzania kutafuta tiketi ya kucheza fainali za kombe la Dunia kwa mara ya kwanza mwaka 2014.

Rais Kikwete ameiambia timu hiyo kuwa ina uwezo mkubwa wa kusonga mbele kutokana na uwezo mkubwa waliouonesha katika mchezo wao dhidi ya Gambia ambapo walifanikiwa kupata ushindi wa bao 2-0.

“Maadamu mara ya kwanza mliwashinda Gambia, hakikisheni pia mnapata ushindi dhidi ya Moroco, mkishinda tunafurahi sana na mkishindwa tunanyong’onyea sana,” amesema Rais Kikwete.

Aidha amempongeza kocha wa timu hiyo Kim Poulsen pamoja na Kamati ya Taifa ya ushindi ya Taifa stars kwa kuisaidia timu hiyo kiasi cha shilingi milioni 30 ikiwa ni mkakati wa kuiongezea nguvu kwa hatua iliyofikia na kuwataka wachezaji kujituma ili kuwafurahisha watanzania ambao hivi sasa wanaipenda timu yao ya Taifa.

Nae Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Fenera Mukangara amesema Serikali itaendelea kushirikiana na wadau mbalimbali wa michezo nchini ili kuondoa changamoto zinazoikabili timu hiyo.

Kwa upande wake Kocha Poulsen, amemshukuru Rais Kikwete kwa kuwakaribisha na kuwatia moyo ambapo ameahidi kuifundisha vizuri timu hiyo ili kuhakikisha kuwa wanapata ushindi.

Akizungumza kwa niaba ya wachezaji wenzake kaptaini wa timu hiyo Juma Kaseja amemshukuru Rais Kikwete na kuahidi kujituma kwenye mazoezi na hatimaye kuibuka washindi kwenye mechi zijazo.

Taifa stars ambayo inakamata nafasi ya pili katika kundi C inatarajia kucheza ugenini na Morocco mnamo Juni 7 mwaka huu.

Sunday, May 19, 2013

Rais Jakaya Kikwete Akutana Kwa Mazungumzo na Askofu Mkuu wa Canterbury Justin Portal Welby katika ukumbi wa St.Gaspar mjini Dodoma


 Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akiwa katika mazungumzo na Askofu Mkuu wa Canterbury Justin Portal Welby katika ukumbi wa St.Gaspar mjini Dodoma jana
Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akiagana na Askofu Mkuu wa Canterbury Justin Portal Welby muda mfupi baada ya kufanya naye  mazungumzo katika ukumbi wa St.Gaspar mjini Dodoma jana.Askofu huyo alishiriki katika ibada ya kutawazwa kwa askofu mkuu mpya wa Kanisa la Anglikana nchini Tanzania Dkt.Jacob Erasto Chimeledya.Picha na Freddy Maro-IKULU

Friday, May 17, 2013

Rais Barack Obama Kutembelea Tanzania Mwezi ujao



 

 President Barack Obama greets children upon his arrival to Miami International Airport in Miami, Friday, March, 4, 2011. (AP Photo/Pablo Martinez Monsivais) 



Rais Barack Obama
 
Rais Barack Obama wa Marekani anatarajia kuanza ziara yake ya pili katika bara la Afrika mwishoni wa mwezi June, ziara ambayo itamfikisha Africa ya Kusini, Tanzania na Rwanda.
Katika ziara yake hiyo, atapitia Nigeria na kuongea na rais Goodluck Jonathan pamoja na waandamizi wa serikali ya Nigeria.
 Mpango wa awali ulikuwa kwamba rais Obama angetembelea Nigeria kwa siku mbili lakini kutokana na hofu ya usalama kutoka kwa magaidi wa Boko Haram Nigeria inaonekana kwamba itashindwa kutoa ulinzi wa kutosha wa rais huyo wa Marekani hivyo atalazimika kukaa Nigeria kwa muda mchache.
Habari kutoka Ikului ya White House zinadokeza kuwa usalama utazingatiwa sana katika ziara hiyo na kama kutakuwa na sababu yeyote ya kuwa na wasiwasi juu ya usalama wa Rais Obama basi ziara hiyo itakatizwa wakati wowote katika nchi ya Nigeria.
Mwaka 2009 Obama alitembelea Africa na alichagua nchi ya Ghana ambapo alikutana na Raisi (marehemu) John Atta mills, na akatoa hotuba katiba bunge la Ghana na kisha kutembelea Cape Coast Castle sehemu ambapo watumwa wa Trans Atlantic walikuwa wanapakiliwa kupelekwa Marekani wakati wa biashara ya utumwa.
Kwa sis watanzania, ziara hii ya kiongozi mkubwa duniani ina manufaa gani kibiashara, kiuchumi, kiusalama? Kuna fursa gani kwa Watanzania kama ilivyoluwa kwa Rais wa China? Ni matumaini yetu kuwa ziara hii itazidi kuliweka Taifa letu katika sura nzuri kimataifa na kitaifa. Ikumbukwe kwamba, Marais wa nchi kubwa kama Marekani wanachagua kutembelea nchi zile zinazofanya vizuri katika utawala bora, demokrasia madhubuti, uhuru wa haki za binadamu, uhuru wa vyombo vya habari, kusimamia na kutimiza vyema malengo ya millenium..... Hivyo kwa Tanzania kupata ugeni kama huu ni ishara nzuri na chachu ya kuendelea kufanya vizuri zaidi. Mungu Ibariki Tanzania
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...