ADV

ADV

ADVERTISEMENT CORNER

HUDUMA YA KUKATA TICKET ZA NDEGE ONLINE


SOMA HABARI

SOMA HABARI
Showing posts with label World Bank. Show all posts
Showing posts with label World Bank. Show all posts

Saturday, May 25, 2013

Benki ya Dunia: Bandari ya Dar es Salaam ni kichocheo cha uchumi

dar d73b6
Tanzania na mataifa jirani ya Afrika Mashariki yanatajwa kuwa yanaweza kuboresha pato la ndani la mwaka – GDP – kama yatachukua hatua za kuboresha ubora wa bandari ya Dar es Salaam.
Kwa mujibu wa ripoti mpya iliyopewa kichwa cha ‘Opening the Gates: How the port of Dar es Salaam can transform Tanzania’ iliyoandikwa na Jacques Morisset, mchumi mkuu wa Benki ya Dunia kwa Tanzania, Uganda na Burundi, Tanzania na majirani zake wanaweza kuongeza pato lao la ndani kwa kiwango kikubwa.
Ripoti hiyo inasema Tanzania inaweza kuongeza pato lake la ndani kwa kiasi cha dola bilioni 1.8  na nchi jirani zinaweza kupandisha pato la ndani kwa dola milioni 830 kwa mwaka, kiwango ambacho kinaelezewa ni hasara iliyotokea mwaka 2012.
Ripoti hiyo inasema kuwa bandari ya Dar es Salaam iko katika njia kuu ya biashara ya Tanzania kwa asilimia 90, na inashughulikia bidhaa zinazogharimu dola bilioni 15 kwa mwaka, sawa na asilimia 60 ya pato la ndani la Tanzania kwa mwaka 2012.

Bandari hiyo pia inaelezewa kuwa inatumiwa na majirani sita wa Tanzania, ambao nchi zao hazina bandari, nchi hizo ni Malawi, Zambia, Burundi, Rwanda, Uganda na mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo.

Mwaka 2012 pekee, ripoti inasema hasara ya jumla inayoelezewa ambayo imetokea katika bandari hiyo imefikia dola bilioni 1.8 kwa uchumi wa Tanzania na dola milioni 830 kwa nchi jirani. Hasara ambayo ni sawa na asilimia saba ya pato la ndani la mwaka la Tanzania, na kwa kiasi kikubwa imeathiri wanunuzi wa ndani, biashara na mashirika ya serikali.

Moja ya sababu ambazo inaelezewa zimechangia katika hasara hii ni utendaji mbaya wa bandari ya Dar es Salaam ambao umezigharimu nchi nyingine jirani nazo kupata hasara, na hivyo kulazimika kulipa fedha zaidi kwa bidhaa zinazoagiwa kutoka nje, ikiwemo bidhaa za msingi kama vile mafuta ghafi, simenti, mbolea na madawa.

Moja ya vigezo  vilivyoelezewa katika ripoti ambavyo vinachangia katika kusababisha  hasara ni pamoja na uchelewesho unaozikabili meli ambazo zinafika katika bandari ya Dar es Salaam.  Katikati ya mwaka 2012, meli zilisubiri kwa takriban siku 10 ili kuweza kuruhusiwa kutia nagan na siku 10 nyingine za ziada ili kuweza kushusha mizigo. 

Rushwa pia imetajwa kuwa ni kigezo kingine kinachochangia katika utendaji mbaya wa Bandar, kama chanzo cha utendaji mbaya na kusababisha hasara kubwa. Chanzo: Voaswahili

Monday, April 22, 2013

Vipaumbele vya Maendeleo ya Tanzania vyajadiliwa kati ya Ujumbe wa Tanzania na Benki ya Dunia ya Dunia



Ujumbe wa Tanzania ukiongozwa na Waziri wa Fedha Mhe. Dkt. Wiliam Mgimwa akitoa ufafanuzi wa vipaumbele kwa ujumbe wa Benki ya Dunia.
Ujumbe wa Tanzania pamoja na ujumbe wa Benki ya Dunia wakijadili namna ya kuendeleza na kuboresha sekta mbalimbali zilizopewa vipaumbele kwa Tanzania ambavyo ni pamoja na Nishati, Usafirishaji na masuala mazima ya MKUKUTA.
Makamu wa Rais wa Benki ya Dunia kanda ya Afrika Bw. Makhtar Diop aliyekaa katikati, akitoa ufafanuzi wa mikakati wa vipaumbele hivyo. Kutoka kushoto ni Mwakilishi mkazi wa Benki ya Dunia Tanzania, Rwanda, Uganda na Burundi Bw. Philippe Dongier na kulia ni Mkurugenzi wa Sekta ya kupunguza umasikini na masuala ya Uchumi kanda ya Afrika Bw. Marcelo Giugale.
Kutoka kushoto ni Mchumi wa Benki Kuu ya Tanzania (BOT) Dkt. Dickson Lema, Mchumi wa BOT Bi. Haika Mbaga, Kaimu Balozi Ubalozi wa Tanzania Washington DC Bibi Lily Munanka, Kamishna wa Fedha za Nje Wizara ya Fedha Zanzibar Bi. Bihindi Nassor na Mchumi wa BOT Bi. Sauda Msemo wakifuatilia majadiliano hayo.
Kutoka kushoto ni Mchumi wa Wizara ya Fedha Bw. Patrick Pima, Naibu Katibu Mtendaji Ofisi ya Rais Tume ya Mipango Prof.  Longinus Rutasitara, Afisa Mwambata anayeratibu masuala ya uchumi, biashara na uwezeshaji ya Benki ya Dunia na Shirika la Fedha la Kimataifa Bw. Paul Mwafongo wakiandika majadiliano hayo. 
Kutoka kushoto ni Mkurugenzi wa Mipango na Uratibu kanda ya Afrika Bw. Jan Walliser, Meneja wa Social Protection kanda ya Afrika Bi. Lynne D-Sherburne – Benz na baadhi ya wafanyakazi wa Benki ya Dunia wakifuatilia majadiliano hayo.
Wafanyakazi wa Benki ya Dunia wakifuatilia majadiliano.
Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania Prof. Benno Ndulu akijibu hoja kwa ujumbe wa Benki ya Dunia huku Waziri wa Fedha Mhe. Dkt. Wiliam Mgimwa akimsikiliza kwa makini.
Kutoka kushoto ni Meneja wa Ubinafsishaji Sekta ya Maendeleo kanda ya Afrika Bi. Irina Astra Khan, Mkurugenzi wa Mipango na Uratibu kanda ya Afrika Bw. Jan Walliser akijibu hoja katika majadiliano hayo. Kulia ni Mwakilishi mkazi wa Benki ya Dunia Tanzania, Rwanda, Uganda na Burundi Bw. Philippe Dongier akisikiliza kwa makini.(Picha zote na Bi. Ingiahedi Mduma na Bi. Eva Valerian – Washington DC).
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...