Ujumbe
wa Tanzania ukiongozwa na Waziri wa Fedha Mhe. Dkt. Wiliam Mgimwa
akitoa ufafanuzi wa vipaumbele kwa ujumbe wa Benki ya Dunia.
Ujumbe
wa Tanzania pamoja na ujumbe wa Benki ya Dunia wakijadili namna ya
kuendeleza na kuboresha sekta mbalimbali zilizopewa vipaumbele kwa
Tanzania ambavyo ni pamoja na Nishati, Usafirishaji na masuala mazima ya
MKUKUTA.
Makamu
wa Rais wa Benki ya Dunia kanda ya Afrika Bw. Makhtar Diop aliyekaa
katikati, akitoa ufafanuzi wa mikakati wa vipaumbele hivyo. Kutoka
kushoto ni Mwakilishi mkazi wa Benki ya Dunia Tanzania, Rwanda, Uganda
na Burundi Bw. Philippe Dongier na kulia ni Mkurugenzi wa Sekta ya
kupunguza umasikini na masuala ya Uchumi kanda ya Afrika Bw. Marcelo
Giugale.
Kutoka
kushoto ni Mchumi wa Benki Kuu ya Tanzania (BOT) Dkt. Dickson Lema,
Mchumi wa BOT Bi. Haika Mbaga, Kaimu Balozi Ubalozi wa Tanzania
Washington DC Bibi Lily Munanka, Kamishna wa Fedha za Nje Wizara ya
Fedha Zanzibar Bi. Bihindi Nassor na Mchumi wa BOT Bi. Sauda Msemo
wakifuatilia majadiliano hayo.
Kutoka
kushoto ni Mchumi wa Wizara ya Fedha Bw. Patrick Pima, Naibu Katibu
Mtendaji Ofisi ya Rais Tume ya Mipango Prof. Longinus Rutasitara, Afisa
Mwambata anayeratibu masuala ya uchumi, biashara na uwezeshaji ya Benki
ya Dunia na Shirika la Fedha la Kimataifa Bw. Paul Mwafongo wakiandika
majadiliano hayo.
Kutoka
kushoto ni Mkurugenzi wa Mipango na Uratibu kanda ya Afrika Bw. Jan
Walliser, Meneja wa Social Protection kanda ya Afrika Bi. Lynne
D-Sherburne – Benz na baadhi ya wafanyakazi wa Benki ya Dunia
wakifuatilia majadiliano hayo.
Wafanyakazi wa Benki ya Dunia wakifuatilia majadiliano.
Gavana
wa Benki Kuu ya Tanzania Prof. Benno Ndulu akijibu hoja kwa ujumbe wa
Benki ya Dunia huku Waziri wa Fedha Mhe. Dkt. Wiliam Mgimwa akimsikiliza
kwa makini.
Kutoka
kushoto ni Meneja wa Ubinafsishaji Sekta ya Maendeleo kanda ya Afrika
Bi. Irina Astra Khan, Mkurugenzi wa Mipango na Uratibu kanda ya Afrika
Bw. Jan Walliser akijibu hoja katika majadiliano hayo. Kulia ni
Mwakilishi mkazi wa Benki ya Dunia Tanzania, Rwanda, Uganda na Burundi
Bw. Philippe Dongier akisikiliza kwa makini.(Picha zote na Bi. Ingiahedi Mduma na Bi. Eva Valerian – Washington DC).
No comments:
Post a Comment