Mourinho alinaswa na Camera akisema maneno mabaya kwa Eto`o kuwa umri wa nyota huyo unaweza kuwa zaidi ya umri wake halisi.
Eto’o,
ambaye aliifungia Chelsea magoli 12 alishangilia moja ya bao lake kwa
staili ya kibabu kinachotembelea mkongojo na kurudia kuwa bado anao
uwezo wa kuendelea kucheza ligi za barani Ulaya.
“Napenda
kusema kuwa siendi Marekani wala mashariki ya mbali,” alisema Eto`o
ambaye amemaliza mkataba wake wa mwaka mmoja aliosaini katika klabu ya
Chelsea akitokea Anzhi Makhachkala.
“Nitaendelea kucheza `levo` za juu. Nitaendekea kucheza ligi ya mabingwa. Bado nina mapenzi makubwa na mashindano haya”.
“Sitawaambieni ni wapi, lakini bado nitakuwa `levo` za juu. Nina miaka 33 na bado nina makombe mawili ya dunia sijacheza”.
“kabla yangu mimi kuna wachezaji waliocheza mpaka miaka 41. Kwahiyo namimi naweza”.
Eto’o aliifungia mabao mengi Chelsea msimu uliopita na kuwazidia vijana
Mapema mwezi huu, Mourinho alipachikwa jina la `Mjinga` na Mcameroon, Samuel Eto`o
No comments:
Post a Comment