ADV

ADV

ADVERTISEMENT CORNER

HUDUMA YA KUKATA TICKET ZA NDEGE ONLINE


SOMA HABARI

SOMA HABARI

Tuesday, October 30, 2012

Financial IQ na mikate iliyotupwa jalalani

 
Mikate iliyotupwa jalalani maeneo ya Mwenge Msikitini leo asubuhi
Uchafu  ambao uko karibu sana na mfereji wa maji machafu ambapo mvua ikinyesha matakataka huingia mtaroni na kuziba njia za maji


Ukuta unaoonekana ni wa AGIP House ambapo wataalamu wetu wa mambo ya usanifu wa majengo wanafanya shughuli zao. Jalala hili limekuwa kikwazo kikubwa kwa ufanisi wa kazi zao


Rundo la mikate iliyotupwa katika jalala la Mwenge

Trekta la Manispaa ya Kinondoni likiwa tayari kupakia takataka. Hii ina maana mradi huu unatambuliwa na kubarikiwa na Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni

Nina mambo matatu ambayo yamenifanya kuandika makala hii asubuhi ya leo
La kwanza ni namna ambavyo nimeshindwa kunywa chai yangu na mkate leo asubuhi baada ya kushuhudia lundo la mikate iliyotelekezwa jalalani karibu na makazi ya watu. Kwangu mimi, mkate ni chakula muhimu sana kwa sababu pamoja na kutumia mkate kama kifungua kinywa, huwa pia mara kadhaa natumia mkate kama chakula changu cha jioni. Hivyo mkate kwangu ni chakula muhimu sana. Kuona mikate mingi kiasi hiki jalalani kumenifanya nijisikie kichefuchefu kuendelea kupata kifungua kinywa cha mkate na pengine jioni nitashindwa kuendelea kula mkate kutokana na hali hii ya hapa jalalani. Wataalamu wa Saikolojia wanaiita "stinking thinking"
Je, aliyetupa mikate hiyo hapo jalalani ametilia maanani kwamba kuna wengine wanaweza kuchukia kula mkate moja kwa moja kutokana na hali hiyo? Na kama hatutakula mikate ataweza kupata tija katika biashara yake ya mikate?

Jambo la pili lililonifanya kufikiria sana hadi kuamua kupiga picha na kuandika makala kuhusu mikate hii ni namna ambavyo mwenye hicho kiwanda cha mikate ameathirika na uharibifu wa mikate hii. Mathalan ni mjasiriamali kama mimi, ni hasara kiasi gani amepata. Kwa kuangalia tu, mikate iliyotupwa ni zaidi ya vipande mia mbili ukiachilia mbali skonzi na burns nyingine nilizoziona hapo. Mikate mia mbili yenye ukubwa ule inauzwa kati ya 1,500 hadi 1800. Ukizidisha kwa 200 ni 360,000/= Huyu mjasiriamali ataweza kuendelea kurudisha  mkopo wa benki au saccoss? Ni hasara kubwa. Ni kwa nini aruhusu hasara kama hiyo katika mradi wa mikate? Hapa ndipo wazo la rafiki yangu Albert Sanga la makala yake ya Financial IQ likanijia. Sanga aliandika makala nzuri sana iliyokuwa na kichwa cha habari

"Kiwango Cha Maisha Yako Ya Uchumi Kinapima Financial IQ Uliyonayo"

Katika makala yake alieleza mengi ikiwa ni pamoja na "mfumo wa fikra zako katika kupata, kuongeza na kutumia fedha. Kwa lugha rahisi ni kuwa kuna watu wa aina mbili. Kundi la kwanza ni wale wanaopata fedha na kuzitumia “zooote”. Kundi la pili ni wale ambao kila wapatapo fedha hufikiria namna bora ya kuzizalisha ziongezeke kabla ya kuzitumia. Kundi la pili wana “financial IQ” kubwa wakati kundi la kwanza wana “financial” IQ ndogo." Financial IQ” mtu huzaliwi nayo isipokuwa unajifunza kwa kuwa na mtazamo na maamuzi sahihi kuhusu fedha.

Nikijaribu kuweka financial IQ ya huyu mjasiriamali aliyetupa hii mikate...... labda ningeacha wasomaji waamue wenyewe ana Financial IQ ya aina gani. 

Jambo la tatu na la mwisho ni kuhusu majalala yanayoendelea kuibuka kila kona za manispaa ya Kinondoni. Sijaelewa ni nini kimetokea miwzi ya hivi karibuni kuibuka kwa majalala katika makazi ya watu na katikati ya mabarabara. Mfano jalala hili lililopo karibu na maofisi, biashara makazi na hata nyumba ya ibada yaani Msikiti wa Mwenge limepigiwa kelele sana. Cha kushangaza ndiyo kwanza linazidi kunawiri. Kuna nini jamani manispaa ya kinondoni? Hapa ni karibu na TRA, ni karibu na flat za Jeshi ambapo watu wengi wanaishi kwa pamoja lakini hakuna anayejali. Watu wa afya wako wapi? Mvua zikinyesha mitaro ikaziba tutasemaje? Wananchi wakipata kipindupindu tutamlaumu nani? Kuweka takataka katika maeneo ya barabara na karibu na makazi ya watu sio ustaarabu hata kidogo. Wahusika wachukue hatua.

hapa nitakua picha nyingine zaidi za maeneo ya Kinondoni ambayo matakataka yamezagaa barabarani.

  












No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...