Mitt Romney na Rais Barack Obama.
Rais wa Marekani
Barack Obama na mpinzani wake wa Republican Mitt Romney wametofautiana
kuhusu sera ya kigeni ya Marekani katika mdahalo wao wa mwisho wa
runinga kabla ya uchaguzi ujao wa Urais.
Romney alimlaumu Rais Obama kwa kushindwa kutoa uongozi unaofaa kwa dunia na ameruhusu amanimashariki ya kati kuvurugika.
Hata hivyo Obama alimkosoa Romney akisema amekuwa akipinga sera zote kuu za marekani ikijumuisha kuivamia Iraq.
Wagombea hao wamezungumzia sana kuhusu swala tete la harakati za mageuzi katika nchi za kiarabu,sawa tete la ran, Israel na China.
Bwana Obama alisema mpinzani wake hana uelewa kuhusu sera ya kigeni lakini Romney naye akamwambia kuwa ameruhusu vurugu kukumba Mashariki ya kati.
Mjadala huo uliofanyika katika chuo kikuu cha Boca Raton, haukuwa na ubishi kama mjadala wa pili wiki jana ambapo rais Obama alijitokeza kisabuni kuonyesha wapiga kura kuwa ye ndiye kiongozi anayestahili
kuchaguliwa mwaka ujao.
Lakini ubishi ulijitokeza mara kwa mara hasa ambapo Obama alitaka kuonyesha wapiga kura kuwa Mit Romney hana uelewa mzuri kuhusu sera ya kigeni na kwamba hawezi kuwa kiongozi mzuri.
Ukitaka kupata DVD za speeches zote za Obama, Romney, Biden, Ryan, Michelle ... piga zimu 0716391060
No comments:
Post a Comment